Dawa ya kutibu minyoo
Zijuwe aina za minyoo na tiba yake. Dawa 5 za kutibu minyoo ya aina zote
DAWA YA MINYOO
Minyoo ni wadudu aina ya parasite ambao wanaingia kwenye miili ya kiumbe hai kama wanyama na binadamu, na wanajipatia chakula chao humo na kuishi. Kwa binadamu kuna minyoo aiina nyingi sana inayo weza kuwaathiri. Ila zipo aina tatu ambazo zinaonekana ni zaidi kuathiri binadamu. Nazo ni kama:-
1.Minyoo aina ya Roundworms hawa wanaingia kwenye miili yetu kupitia vyakula tunavyokula ama vinywaji endapo hivyo vyakula ama vinywaji vitakuwa na mayai yao. Minyoo hawa wanataga na kuishi kwenye utumbo. Minyoo hawa ni pamoja na threadworm, ascaris, hookworm na trichuris.
2.Minyoo aina ya tapeworm, hawa hishi kwenye tumbo, mara nyingi tunaweza kuwapata minyoo hawa kwa kula chakula ambacho hakikupikwa ama hakikuwiva vyema kama nyama, mihogo mibichi n.k
3.Flukeworms, minyoo hawa huingia mwilini mwetu na kuishi kwenye damu, tumbo, mapafu ama kwenye ini. Unaweza kuwapata minyoo hawa kwa kuogelea ama kuoga kwenye maji yenye minyoo hawa. Mimnyoo hawa husababisha pia ugonjwa ujulikanao kama kichocho (schistosomiasis).
Ni dawa gani hutibu minyoo?
Kwa ufupi tiba ya minyoo hutofautiana kulingana na aina ya minyoo na kiasi cha athari ndani ya mwili. Kwa kiasi kikubwa dawa aina ya Mebendazole imekuwa ikitumika kwa kiasi kikubwa sana maeneo mengi. Na hii ni kwa sababu dawa hii inatumika sana kutibu minyoo aina ya threadworm ambao minyoo hawa ndio wanaathiri watu zaidi. Pia inaweza kutibu aina nyinginyingi za minyoo. Dawa nyingine za kutibu minyoo ni:-
1.Levamisole
2.Tiabendazole
3.Ivermectin
4.Niclosamide
5.Praziquantel
6.Albendazole
7.Diethylcarbamazine
Dawa hizi zinafanyaje kazi?
Yes hili ni swali zuri sana. Sasa inakupasa ujuwe namna ambavyo dawa hizi zitakusaidia kutibu minyoo. Dawa hizi zinafanya kazi kama ifuatavyo:-
A.Mebendazole, albendazole na tiabendazole hizi kuzuia minyoo isifyonze chakul (sugar) kutoka kwenye miili yetu. Hivyo wanaweza kufa kwa njaa. Ila dawa hii itauwa minyoo lakini sio mayai yao ambayo wameyataga tayari.
B.Praziquantel na ivermectin, dawa hizi husaidia kuwazubaisha minyoo kwenye utumbo, hivyo wanaweza kutolewa kwa njia ya haja kubwa.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Madrasa kiganjani 👉2 ai web app 👉3 Kitabu cha Afya 👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉5 Dua za Mitume na Manabii 👉6 Kitau cha Fiqh
Post zinazofanana:
Dawa ya chango na maumivu ya hedhi
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu dawa ya chango na maumivu ya hedhi
Soma Zaidi...Fahamu dawa ya carvedilo katika matibabu ya magonjwa ya moyo
Post hii inahusu zaidi dawa ya carvedilo katika matibabu ya magonjwa, ni mojawapo ya dawa kwenye kundi la beta blockers na pia uhusika katika matibabu ya magonjwa ya moyo kama nyingine.
Soma Zaidi...Fahamu kundi la veta blockers katika matibabu ya magonjwa ya moyo.
Post hii inahusu zaidi kundi la beta blockers katika matibabu ya magonjwa ya moyo,hili kundi lina dawa mbalimbali ambazo utumika katika matibabu ya magonjwa ya moyo na kila dawa tutaiongelea tofauti tofauti ili kuweza kujua kazi zake.
Soma Zaidi...Neno la awali
Asalaamu alykum warahmatullah wabarakaatuh Sifanjema zinamstahikia Allah Mola wa viumbe, muumba wa mbingu na ardhi na vilivyomo.
Soma Zaidi...Fahamu kuhusu dawa za magonjwa ya moyo
Post hii inahusu zaidi dawa za magonjwa ya moyo, ni dawa ambazo utumika kusaidia pale moyo kama umeshindwa kufanya kazi ipasavyo.
Soma Zaidi...Fahamu dawa ya kutibu maumivu ya mgongo (back none pain) na kiuno
Fahamu dawa ya back bone pain kwa matibabu ya mgongo, ni mojawapo ya dawa ambayo imependekezwa kutuliza maumivu ya mgongo.
Soma Zaidi...