Utajifunza dalili za fangasi mdomoni na ulimini, sababu za fangasi wa mdomoni na ulimini, matibabu yeke na njia za kukabiliana nao
Dawa ya fangasi kwenye mdomo na ulimi
Fangasi wanaweza kuathiri sehemu yeyote kwenye ngozi ya mtu. Kuanzia vidole, kichwa, kwapa, sehemu za siri na mapajani. Hutokea fangasi wakaathiri mdomo na ulimi. Hapa hali inaweza kuwa mbaya pale mtu akishindwa kula. Bila shaka ni maumivu, lakini leo nitakwenda kukutajia tiba yake.
Nini sababu ya fangasi wa mdomo na ulimi?
Fangasi hawa husababishwa na aina ya fangasi inayoitwa Candida albicans (C.albicans). hawa fangasi ni kawaida kupatikana kwenye mdomo. Kwa mtu ambaye kinga yake ipo imara hakuna shida yeyote anaweza kuipata kwa kuwa na fangasi hawa. Ila endapo watazidi kupitiliza ndipo inaweza kuleta shida.
Dalili za fangasi kwenye mdomo na ulimi
1.Vijidoma vyeupe au njano kwenye shavu kwa ndani, finzi, midomo na kwenye ulimi
2.Kuvuja kwa damu wa finzi
3.Vidonda kwenye mdomo
4.Kuhisi kama kuna pamba kwenye mdomo (vinyuzinyizi)
5.Ukavu wa kona za mdomo pamoja na mipasuko
6.Taabu katika kumeza
7.Mdomo kuwa na ladha mbaya
8.Kupotesa ladha ya unachokila.
Fangasi wa mdomoni wanaweza kuambukiza?
Yes wanaweza kuambukizwa kwa mfano ukimkisi (denda) mtu anaweza kupata fangasi hawa kama na wewe unao.
Dawa ya fanasi kwenye mdomo na ulimi
1.Fluconazole hiini ya kumeza
2.Clotrimazole (Mycelex Troche) ni kidonge pia cha kumumunyikia mdomoni
3.Nystatin (Nystop, Nyasta) ni ya kuosha mdomo
4.Itraconazole (Sporanox) ni ya kumeza, hupewa wale wenye usugu ama wenye HIV
5.Amphotericin B (AmBisome, Fungizone) hutumika kutibu hali mbaya zaidi ya fangasi wa mdomoni.
Nini ufanye ukiwa unatumia dawa hizi
1.Piga mswaki kwa mswaki ulio mlaini
2.Badili mswaki baada ya kumaliza dozi
3.Usitumie dawa za kuosha mdomo mpaka daktari akuambie.
4.Osha mdomo kwa maji ya chumvi
5.Changanya maji na juisi ya limao kisha knywa
Umeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi kazi ya paracetamol katika kutuliza maumivu, ni Aina ya dawa ambayo utumiwa sana katika kutuliza maumivu kwa wagonjwa.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa mbalimbali za kutibu minyoo, tunafahamu kabisa minyoo ni ugonjwa ambao uwapata watu mbalimbali hasa watoto.
Soma Zaidi...Post hii inahusu dawa ya kaoline katika kutibu au kuzuia kuharisha ni dawa ambayo imependekezwa kutumiwa hasa kwa wale walioshindwa kutumia dawa ya loperamide.
Soma Zaidi...Fahamu dawa ya back bone pain kwa matibabu ya mgongo, ni mojawapo ya dawa ambayo imependekezwa kutuliza maumivu ya mgongo.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ya loperamide ni dawa ambayo inazuia kuharisha ni dawa inayofanya kazi kuanzia kwenye utumbo na pia usaidia kutuliza maumivu ya tumbo
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi tiba ya jino,ni tiba ya kawaida kwa watu walio na matatizo ya meno, kwa kawaida tunafahamu kwamba jino huwa halina dawa ila dawa yake huwa ni kungoa lakini Leo nawaletea habari njema kwamba jino sio kungoa tena ila Kuna tiba ambayo
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa za Doxorubicin and Daunorubicin katika kupambana na kansa.
Soma Zaidi...Lasix (Furosemide) iko katika kundi la dawa zinazoitwa vidonge vya maji (loop diuretics) vidonge vya maji. Lasix hutumiwa kupunguza uvimbe mwilini unaosababishwa na kushindwa kwa moyo, ugonjwa wa ini, au ugonjwa wa figo. Kwa matibabu ya dalili nyingi.La
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa zinazofanya kazi ya kupunguza maumivu kwa kawaida dawa hizi ufanya kazi kwa kupitia kwenye mfumo wa fahamu.
Soma Zaidi...