FAHAMU DAWA YA AMINOPHYLLINE KUTIBI MAAMBUKIZI KWENYE MFUMO WA UPUMUAJI


image


Post hii inahusu zaidi dawa ya aminophylline katika kutuliza maambukizi kwenye mfumo wa upumuaji.


Fahamu dawa ya kutibu au kutuliza maumivu kwenye mfumo wa upumuaji.

1. Aminophylline ni mojawapo ya dawa ambayo ufanya kazi katika mfumo wa upumuaji kwa matibabu hasa ya asthma na pia kwa watu wenye tabia ya kubanwa na vifua wakati hali ya hewa inapobadilika na matatizo ya upumuaji kwa ujumla pia dawa hii utolewa kwa kupitia kwenye mishipa ya damu Ili kuweza kufanya kazi kwa haraka kwa mgonjwa.

 

2. Pia kwa mara chache huwa kwenye mfumo wa vidonge na pia wakati mwingine uweza kutolewa kwa kupitia kwenye matako na paja ila kwa upande wa matako na paja usababisha maupeke na maumivu na pia kwa kupitia kwenye damu utolewa taratibu walau kwa mda wa dakika ishilini au zaidi kidogo.

 

3. Dawa hii Ina kuwa na milligrams mia mbili hamsini na pia mills kumi na utolewa kwa utaratibu na pia dozi ubadilika kulingana na umri pamoja na Uzito.

 

4. Dawa hii huwa na maudhi madogo madogo kama vile kichefuchefu na kutapika, kizunguzungu, mapigo ya moyo kwenda mbio na pia inawezekana kuwepo kwa degedege hasa kwa watoto wadogo na kwa watu wazima ni mara chache sana 

 

 5. Iwapo kama Kuna matokeo ya kuwepo kwa degedege ni vizuri kutumia dawa ya diazepam Ili kuweza kutuliza hiyo degedege, kwa hiyo dawa hii inapaswa kueleweka kwamba Kuna watu ambao hawapaswi kutumia dawa hii ni wale wenye aleji na dawa hii na pia kwa wale wenye tatizo la kifafa wanapaswa kuitumia dawa hii kwa uangalizi maalumu na ikibidi wanapaswa kuitumia kwa uangalizi Fulani.

 

6. Pia dawa hii haipaswi kutumiwa kiholela au kwa mazoea Bali kwa utaratibu wa wataalamu wa afya Ili kuepuka madhara zaidi ambayo yanaweza kutokea.



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Hadiythi za alif lela u lela       ðŸ‘‰    2 Magonjwa na afya       ðŸ‘‰    3 Mafunzo ya php       ðŸ‘‰    4 Maktaba ya vitabu       ðŸ‘‰    5 Madrasa kiganjani       ðŸ‘‰    6 Mafunzo ya html kwa kiswahili    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS



Post Nyingine


image Fahamu zaidi kuhusiana na Dawa ya Moyo DIGOXIN
Digoxin ni nini? Digoxin inatokana na majani ya mmea wa digitalis. Digoxin husaidia kufanya mapigo ya moyo kuwa na nguvu na kwa mdundo wa kawaida zaidi. Digoxin hutumiwa kutibu kushindwa kwa moyo. Digoxin pia hutumiwa kutibu mpapatiko wa atiria, ugonjwa wa mdundo wa moyo wa atiria (vyumba vya juu vya moyo vinavyoruhusu damu kutiririka ndani ya moyo). Soma Zaidi...

image Ifahamu dawa ya isoniazid katika kupambana na ugonjwa wa TB
Post hii inahusu zaidi dawa ya isoniazid katika mapambano na kifua kikuu, tunafahamu kabisa kwamba kifua kikuu ni hatari katika jamii kwa hiyo dawa ya isoniazid ni mkombozi katika mapambano na kifua kikuu. Soma Zaidi...

image Fahamau madhara ya flagyl (Metronidazole)
Flagyl ni nini? Flagyl (metronidazole) ni antibiotic. Inapigana na bakteria katika mwili wako. Flagyl hutumiwa kutibu maambukizo ya bakteria ya uke, tumbo, ngozi, viungo na njia ya upumuaji. Soma Zaidi...

image Kazi za Dawa ya Artesunate katika kutibu Malaria
Posti hii inahusu zaidi kazi za dawa ya Artesunate katika kutibu Malaria kali, ni dawa ambayo inatumika sana kutibu Malaria kali. Soma Zaidi...

image Fahamu dawa ya kuzuia enzymes zinazotengenezwa na bakteria
Post hii inahusu zaidi dawa ya cloxacillin ambayo Iko kwenye kundi mojawapo la penicillin ambalo uzuia enzymes zinazotengenezwa na bakteria. Soma Zaidi...

image Fahamu dawa za kisukari
Post hii inahusu zaidi dawa za kisukari, kwa sababu ya kuwepo kwa ugonjwa wa kisukari vilevile kuna dawa zake ambazo utumika kurekebisha sukari kama imepanda au kushuka. Soma Zaidi...

image Fahamu kazi za homoni katika kupamba na kansa.
Post hii inahusu zaidi homoni mbalimbali ambazo upambana na kansa, hizi homoni zikitumika vizuri matokeo yake huwa na mazuri pia kwa wagonjwa wa kansa. Soma Zaidi...

image Mebendazole kama dawa ya kutibu Minyoo.
Post hii inahusu zaidi dawa ya Mebendazole kama Dawa ya kutibu Minyoo, ni dawa inayotumiwa na watu wengi pale wanapokuwa na minyoo, walio wengi wamefanikiwa kupona kwa kutumia Dawa hii. Soma Zaidi...

image Faida za dawa za NMN
Posti hii inahusu zaidi faida za dawa za NMN maana yake ni Nicotinamide mononucleotide ni dawa ambazo usaidia kutibu magonjwa mbalimbali kama vile. Soma Zaidi...

image Fahamu dawa za kutuliza magonjwa ya akili inayoitwa Chlorpromazine
Post hii inahusu zaidi dawa zinazosaidis katika kutuliza magonjwa ya akili, dawa hii kwa kitaamu huiitwa chlorpromazine ni dawa ambayo utumiwa na watu wenye tatizo la magonjwa ya akili na kwa kiasi kikubwa huwa sawa. Soma Zaidi...