Navigation Menu



image

Dawa ya kiungulia na njia za kuzuia kiungulia

utajifunza njia za kuzuia kiungulia, dalili za kiungulia na dawa ya kutibu kiungulia.

Dawa ya kiungulia na njia za kuzuia kiungulia

NJIA ZA KUZUIA KIUNGULIA




Kiungulia hutokea pale tindikali zilizopo tumboni zinapanda juu na kufikia koo sehemu ambayo inaunganisha tumbo na koo la chakula. Kiungulia sio shida sana kiafya kwani huwa kiaondoka chenyewe. Hata hivyo kuna watu wapo hatari kupata kiungulia cha mara kwa mara.



Je na wewe ni mmoja katika wanaopata kiungulia mara kwa mara. Je kiungulia ni kikali kiasi cha kuharibu ratiba na uhuru wako? Makala hii ni kwa ajili yako. Hapa nitakuletea njia ambazo zitakusaidia kuzuia kiungulia cha mara kwa mara.



Njia za kuzuia kiungulia
1.Usile chakula kingi kupitiliza
2.Punguza uzito ulio nao
3.Punguza unywaji wa pombe
4.Usinywe sana chai ya majani ya chai yenye caffein kwa wingi
5.Tafuna bigjii zisizo na sukari nyingi
6.Wacha kutumia kitunguu kisichopikwa kama kwenye kachumbari
7.Epuka vinywaji vyenye carbonate. Soma lebo ya kinywaji chako kama ni soda ama maji kama kuna carbonate
8.Usinywe kwa wingi juisi zilizotokana na vitu vya uchachu kama limao
9.Punguza kula chokoleti kwa wingi
10.Unapolala inuka kichwa chako kwa mfano tumia mto
11.Usilale ndani ya masaa matatu baada ya kula
12.Ukilala lalia upande wa kushoto usilalie upande wa kulia.



Dawa za kutibu kiungulia
Unaweza kutibu kiungulia kwa kutumia antacid kama vile Tums, Rolaids na Maalox. Dawa ambazo zimetengenezwa kwa madini ya calcium carbonate au magnesium ni nzuri pia. Magnesium si nzuri kama ujauzito upo mwishoni.



Madaktari wengi wanakataza kwa wajawazito matumizi ya antacid ambazo zimechanganywa na sodium, ama zila lebo ya aluminium carbonate kwani zinawza kupelekea kukosa choo. Pia dawa hizi za kiungulia zinakatazwa kwa wajawazito Alka-Seltzer.





                   








           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Vyakula Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 2305


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Simulizi za Hadithi Audio     👉4 Kitabu cha Afya     👉5 Kitau cha Fiqh     👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    

Post zifazofanana:-

Faida za vitamin C mwilini
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za vitamini C mwilini Soma Zaidi...

Vyakula vyenye vitamini C kwa wingi
Vitamini C kwa wingi hupatikana kwenye machungwa, maembe, mananasi, limao na ndimu Soma Zaidi...

Faida za kula kabichi
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula kabichi Soma Zaidi...

Vyakula vya protini na kazi zake
Soma Zaidi...

Yafahamu magonjwa nyemelezi kwa watoto chini ya miaka mitano
Posti hii inahusu zaidi magonjwa nyemelezi kwa watoto wadogo chini ya miaka mitano,. Ni magonjwa yanayowapata watoto wadogo kwa sababu kinga Yao bado ni ndogo. Soma Zaidi...

Faida za kula Chungwa
Je unazijuwa faida za kula chungwa kiafya? soma makala hii hadi mwisho Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula Palachichi
Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula Pensheni
Soma Zaidi...

Upungufu wa vitamini C na dalili zake mwilini
makala Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula Embe
Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula maboga
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula maboga Soma Zaidi...

Faida kula fenesi
Somo hili linakwenda kukuletea faida za kiafya za kula fenesi Soma Zaidi...