PRESHA YA KUSHUKA NA MATIBABU YAKE
Presha ya kushuka mara nyingi haina dalili za kutisha, pia haina shida sana ukilingnisha na presha ya kupanda. Kama unahisi dalili za presha ya kushuka kama kizunguzungu, kichwa kuwa chepesi wakati unaposimama na kuamka, huku mgandamizo wa damu kupunguwa hii hali inatambulika kama postural hypotension.Kugundua presha ya kushuka daktari atakupima kwa kipimo maalumu. Pia vipo vipimo vngine kama vitahitajika zaidi, kama vile electrocardiogram (ECG), ultrasound pia kipimo cha damu kuangalia kiwango cha sukari kwenye damu na kuangalia kama kuna upungufu wa damu.Utaratibu wa kuishi ukiwa na presha ya kushuka.
Ningependa tu kukujulisha kuwa unaweza kuishi vyema ukiwa na presha ya kushuka, hata bila ya kutumia dawa za mahospitali. Kabla hatujaona dawa za mahospitali sasa nanakwenda kukueleza utaratibu wa lishe kwa mwenye prsha ya kushuka.1.Kula chakula chenye chumvi zaidi
2.Kula vyakula vyenye majimaji mengi kama matunda na mfano wake
3.Punguza kunywa vilevi
4.Kunywa maji mengi hasa wakati wa joto
5.Fanya mazoezi ya mara kwa mara
6.Unapolala tumia mto, yaani sehemu ya kichwa chako iwe juu
7.Jizuie kubeba vitu vizito
8.Washa kukaa maeneo yenye joto sana ma kuoga maji ya moto kwa muda mrefu.
9.Acha kusimama wima sehemu moja kwa muda mrefu.Dawa zinazotumika kutibu presha ya kushuka (hypotension)
A.Fludrocortisone, zungumza na daktari kabla ya kutumiadawa hii.
B.Midodrine.Hakikisha dawa hizi humezi kiholela. Kabla ya kutumia dawa yeyote kwanza zungumza na daktari kwanza. Hii ni kwa ajili ya afya yako.