Mbinu za kupunguza Kichefuchefu


image


Point hii inahusu zaidi mbinu za kupunguza Kichefuchefu hasa kwa wagonjwa na watumiaji wa madawa mbalimbali yanayoweza kusababisha kichefuchefu.


Mbinu za kupunguza Kichefuchefu.

1. Kutumia vyakula vigumu vigumu.

Kama mtu anayetumia dawa zinazosababisha kichefuchefu au mgonjwa wanapaswa kutumia vyakula vigumu kama vile mkate chapati na vyakula kama mihogo iliyopikwa, viazi na vyakula vigumu kwa ujumla na pia mwenye Kichefuchefu anapaswa kuachana na vyakula ambavyo havipendi akiwa mzima kwa sababu vinaweza kusababisha kichefuchefu.

 

2. Kunywa na kula kidogo kidogo.

Mwenye kichefuchefu anapaswa kula na kunywa kidogo kidogo kwa sababu akila na kunywa kidogo kidogo na kwa mda mwingi hawezi kutapika kuliko yule anayekula chakula kingi Yuko kwenye hatari ya kutapika. Kwa hiyo mgonjwa anapaswa kula kidogo kidogo mara nyingi na kunywa kidogo kidogo kwa mara nyingi.

 

3. Mwenye kichefuchefu anapaswa kukaa wima baada ya kula.

Baada ya kula chakula mwenye kichefuchefu anapaswa kukaa wima maana akikaa wima hawezi kuruhusu chakula kupita lakini akiinama anaweka chakula katika mfumo wa kukiruhusu chakula na kuweza kupita kwa hiyo wauguzi na wote wanaoudumia wagonjwa wanapaswa kuwasaidia wale ambao hawajiwezi Ili kuwafanya wasiiname pindi wanapomaliza kula Ili kuepuka kichefuchefu.

 

4. Tumia Tiba asili ya kubonyeza sehemu mbalimbali za mwili.

Kuna wakati mwingine watu ubonyeza kwenye sehemu za mkono Ili kuzuia kichefuchefu kwa kufanya hivyo wanaweza kuzuia kichefuchefu na walio wengi wameitumia njia hiyo na wamefaulu kwa hiyo Kuna Tiba za asili ambazo watu wanazitumia na kufanikisha kupunguza Kichefuchefu.

 

5. Kwa hiyo tunapaswa kujua kuwa kichefuchefu ni dalili kubwa ya kutaka kutapika kwa hiyo tunapaswa kuwasaidia wagonjwa wetu kutibu kichefuchefu na kuzuia kutapika Ili kufanya matibabu yaende vizuri kwa hiyo tusiwanyanyapae wale wenye tatizo hilo kwa maana ni la kawaida na uwapata watu wengi hasa wenye matumizi ya madawa na wagonjwa.



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Download App zetu hapa ujifunze zaidi       ðŸ‘‰    2 Tunakukaribisha kwenye Maktaba yetu       ðŸ‘‰    3 Jifunze Fiqh       ðŸ‘‰    4 Madrasa kiganjani offline    


Je una maswali, maoni ama ushauri, tutumie sms ✉ bofya hapa hapa, ama wasiliana nasi kwa WhatsApp bofya hapa



Post Nyingine


image Dalili na ishara za jeraha kwenye ngozi
Posti hii inaonyesha dalili,sababu na mbinu za kutoa huduma ya kwanza kwa aliyepata jeraha kwenye ngozi kwa kuingiliwa na kitu Kama mwiba,Pini,sindano n.k Soma Zaidi...

image Maumivu ya kiuno na dalili zake
Posti hii inahusu zaidi maumivu ya kiuno na dalili zake, ni maumivu ambayo utokea kwenye kiuno na kusababisha madhara mbalimbali katika mwili, Soma Zaidi...

image Madhara ya Tiba mionzi
Post hii inahusu zaidi madhara ya Tiba mionzi kwa wagonjwa wa saratani, ni madhara yanayotokea kwa wagonjwa wanaotumia mionzi katika matibabu ya saratani. Soma Zaidi...

image Njia za kuingiza chanjo mwilini
Posti hii inahusu njia mbalimbali ambazo utumika kupitisha chanjo, njia hizo utegemea na kazi ya chanjo kama ifuatavyo. Soma Zaidi...

image Vyakula vya kuoambana na mafua
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu vyakula vya kuoambana na mafua Soma Zaidi...

image Dalili za malaria
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu baadhi ya dalili za maralia Soma Zaidi...

image Dalili za saratani ya mapafu
Saratani ya Mapafu ni aina ya Kansa inayoanzia kwenye mapafu. Mapafu yako ni viungo viwili vya sponji kwenye kifua chako ambavyo huchukua oksijeni unapovuta na kutoa kaboni dioksidi unapotoa nje. Soma Zaidi...

image Huduma ya Kwanza kwa aliyekazwa na misuli
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu aliyekazwa na misuli Soma Zaidi...

image Ugonjwa wa UTI
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu ugonjwa wa UTI Soma Zaidi...

image Mabadiliko ya ngozi wakati wa ujauzito.
Posti hii inahusu zaidi mabadiliko kwenye ngozi wakati wa ujauzito, ni mabadiliko yanayotokea kwenye ngozi ya Mama wakati wa ujauzito. Soma Zaidi...