Posti hii inahusu zaidi madhara ambayo yanaweza kutokea kwa sababu ya matumizi ya sindano za kuzuia mimba kwa vijana ambao hawajafikilia mpango wa kuanza kujifungua watoto.
1. Kwanza kabisa tunapaswa kufahamu maana ya uzazi wa mpango ni njia inayotumiwa na wenza Ili kupata idadi ya watoto wanaowahitaji au kuwapatia nafasi kutoka kwa mtoto mmoja kwenda kwa mwingine ila Kuna wasichana ambao hawana mpango wa kuanza kujifungua karibuni ila wanatumia njia ya uzazi wa mpango kwa mda mrefu na Kuna madhara yake kama ifuatavyo.
2. Kubadilika kwa hedhi.
Kwanza kabisa kama msichana anatumia siku tatu wakati wa hedhi anaweza kuanza kutumia siku tano ,sita Saba na kuendelea hali inayosababisha upungufu wa damu mwilini au pengine damu inakuwa ni nzito au nyepesi kuliko kawaida kwa sababu ya matumizi ya sindano kwa mda mrefu.
3. Maumivu ya kichwa ya mara Kwa mara.
Kwa sababu ya kuwepo au kubadilika kwa homoni usababisha maumivu ya kichwa ya mara Kwa mara au kwa sababu ya kutokwa na damu nyingi nayo usababisha maumivu ya kichwa ya mara Kwa mara.
4. Kuwepo kwa kizungu zungu.
Kwa kawaida kwa sababu ya kutumia dawa za sindano usababisha kuongezeka kwa homoni au kubadilika kwa mwili kwa hali isiyo ya kawaida au kitendo cha kupungua kwa damu mwilini nacho usababisha kuwepo kwa kizungu zungu kwa akina dada.
5. Kuwepo kwa kichefuchefu.
Hali hii utokea kwa sababu ya kuongezeka kwa homoni nyingine kutoka kwenye sindano na Ile hali ya kuvurugika kwa mfumo wa hali ya mwili kwa sababu ya sindano.
6. Kuwepo kwa uzito usio wa kawaida.
Kwa wakati mwingine kunakuwepo na uzito usio wa kawaida kwa sababu ya sindano na meongezeko wa homoni.
7. Kuwepo kwa uvimbe kwenye kizazi.
Kwa sababu ya sindano za kila mwezi na kuharibu mfuko mzima wa mwili usababisha kuwepo kwa uvimbe kwenye kizazi.
8. Kwa hiyo dalili hizi si kwa akina dada tu zinaweza kutokea hata kwa baadhi ya akina Mama kwa hiyo tunaenda kuwataarifu akina dada kusubiri wakati wao ufike ndo wajiingize kwenye matumizi ya uzazi wa mpango.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inaelezea kuhusiana na nguvu za kiume zinavyopungua na Ni Mambo gani yanayofanya zipungue
Soma Zaidi...Njoo ujifunze vyakula vya kuboresha mbegu za kiume na nguvu za kiume.
Soma Zaidi...Mimba haipatikani kila siku, na pia mimba huingia kwa siku moja na katika muda mmoja. Baada ya mimba kutungwa hakuna tena nafasi ya kutungwa mimba nyingine.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi Ugonjwa wa kifafa cha mimba ambapo kwa kitaalamu huitwa eclampsia, utokea pale ambapo Mama anapokuwa na degedege wakati wa mimba na baada ya kujiunga.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi njia ambazo tunaweza kutumia ili kuweza kupunguza tatizo hili la kutanuka kwa tezi dume, kwa hiyo tunaweza kutumia njia zifuatazo ili kuweza kupunguza tatizo hili kwenye jamii kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...