Aina 12 za swala za sunnah na idadi ya rakaa zake wakati wa usiku na mchana
Aina za Swala za Sunnah.
Aina 12 za swala za sunnah na idadi ya rakaa zake wakati wa usiku na mchana
Aina za Swala za Sunnah.
Rejea Kitabu cha 1, EDK, Shule za Sekondari, Uk. 150-165.
Swala za Sunnah ni nyingi, tutaangalia baadhi tu kama ifuatavyo:
i.Swala ya Maamkizi ya Msikiti.
- Huswaliwa rakaa mbili muda wowote mara tu muislamu aingiapo msikitini kabla ya kukaa.
ii.Swala za Qabiliyyah na Ba’adiyyah.
- Hizi huswaliwa kabla (Qabiliyyah) na Baada (Ba’adiyyah) ya swala za Faradh.
- Ziko aina mbili; ‘Mu’akkadah’ (zilizokokotezwa) na ‘Ghairu Mu’akkadah’ (Hazikukokotezwa).
iii.Swala ya Witiri.
- Huswaliwa rakaa kwa idadi ya witiri; 1, 3, 5, 7, 9 na 11 katika theluthi ya mwisho wa usiku au mara tu baada ya swala ya Ishaa.
- Witiri imekokotezwa mwisho wa usiku zaidi na huambatanishwa kwa dua ya Qunuti katika rakaa ya mwisho.
iv.Swala ya Tahajjud (Qiyaamul-layl).
- Huswaliwa rakaa 8 usiku wa manane kwa rakaa mbili mbili na kumalia 3 za witiri na kutimia rakaa 11.
- Huswaliwa kwa kisimamo na kisomo kirefu cha Qur’an.
Rejea Qur’an (17:79), (25:64), (39:9) na (73:1-4).
v.Swala ya Tarawehe (Qiyaamu Ramadhan).
- Ni swala ya kisimamo na Kisomo kirefu cha Qur’an, Juzuu 1 kila siku inayoswaliwa mwezi wa Ramadhani tu baada ya Ishaa au kabla ya swala ya Alfajir.
- Kuna hitilafu kwa idadi ya rakaa, kauli zinasema ni rakaa 8, 11, 20, 36, n.k.lakini yenye nguvu ni rakaa 8 na 3 za witiri na kuwa jumla rakaa 11.
vi.Swala ya Idil-Fitr na Al-Udhuhaa.
- Zote huswaliwa rakaa mbili, Idil-Fitr huswaliwa mwezi 1 Shawwal baada ya kumalizika funga ya mwezi wa Ramadhani.
- Idil-Al-Udhuhaa huswaliwa mwezi 10 Dhul-Hija baada ya kukamilika ibada ya Hija kila mwaka.
vii.Swalatudh-Dhuhaa.
- Huswaliwa kila siku baada ya Jua kupanda kiasi cha mita tatu kutoka kuchomoza kwake.
- Huswaliwa rakaa mbili mbili hadi kutimia nane, lakini kwa uchache huswaliwa rakaa mbili.
viii.Swalatul-Istikharah.
- Ni swala inayoswaliwa muda wowote kwa ajili ya kuomba msaada na mwongozo kwa Allah juu ya uamuzi au utatuzi wa jambo lolote zuri.
ix.Swala ya Kukidhi Haja.
- Ni swala inayoswaliwa muda wowote kwa ajili ya kuomba msaada au utatuzi wa tatizo lililotokea au unalohitajia.
x.Swalatut – Tawbah.
- Huswaliwa rakaa mbili muda wowote kwa ajili ya kutubia baada ya muislamu kufanya kosa.
Rejea Qur’an (3:135-136).
xi.Swala ya Kupatwa kwa Jua na Mwezi.
- Huswaliwa kwa jamaa, rakaa mbili, rukuu mbili kwa kila rakaa moja. Huswaliwa kwa kisimamo na kisomo kirefu mpaka Kupatwa kuondoke.
xii.Swala ya Kuomba (Swalatul-Istisqaa).
- Ni swala ya rakaa mbili kwa ajili ya kuomba mvua baada ya kuzidi dhiki na ukame, kwa jamaa na uwanjani.
- Swala hii ina khutuba mbili na takbira kama inavyoswaliwa swala za Idi.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Dua za Mitume na Manabii 👉2 Kitau cha Fiqh 👉3 web hosting 👉4 kitabu cha Simulizi 👉5 Bongolite - Game zone - Play free game 👉6 Simulizi za Hadithi Audio
Post zinazofanana:
Vipi funga yaani swaumu itapelekea uchamungu na kutekeleza lengo
Funga inavyomuandaa mtu kuwa mcha-Mungu.
Soma Zaidi...Jinsi ya kufanya suluhu kati ya mume na mke.
Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu jinsi ya kufanya suluhu katika ndoa.
Soma Zaidi...Maandalizi kwa ajili ya kifo
Mwanadamu anatakiwa aishi huku akikumbuka kuwa ipo siki atakufa. Hivyo basi inatupata lujiandaa mapema kwa ajili ya kifo.
Soma Zaidi...