image

Ibada ya hija, faida zake, lengo lake, nguzo zake na ni zipi aina za hija?

Hijjah.

Ibada ya hija, faida zake, lengo lake, nguzo zake na ni zipi aina za hija?

NGUZO ZA UISLAMU: HIJA

Hijjah.
Umuhimu na Nafasi ya Hijjah katika Uislamu.
i.Hijjah ni nguzo ya tano ya Uislamu.
Baada ya shahada, swala, zakat na funga, nguzo muhimu na ya mwisho ya Uislamu ni Hijjah.
Rejea Qur’an (3:97).

ii.Hijjah ni amri ya Mwenyezi Mungu (s.w).
Kama ilivyofaradhi kwa nguzo zingine, Hijjah ni ibada ya lazima kwa waislamu wenye uwezo wa kimali na afya.
Rejea Qur’an (3:97).

iii.Kutoenda Hija makusudi ni kustahiki adhabu za Mwenyezi Mungu.
Kwa kila muislamu mwenye uwezo, akipuuza kutekeleza ibada ya Hijah basi anastahiki adhabu hapa duniani na Akhera pia.
Rejea Qur’an (3:97).

iv.Kutekeleza ibada ya Hija hupelekea kupata msamaha Duniani na Akhera.
Kwa kila mwenye kutekeleza ibada ya Hijjah ipasavyo, basi husamehewa madhambi yake yaliyotangulia.


Lengo la Hijjah.
Kuwa askari Mcha-Mungu aliyekuwa tayari kutumia mali na nafsi yake katika kuipigania Dini ya Mwenyezi Mungu (s.w) kutawala maisha ya jamii.
Rejea Qur’an (48:18) na (3:96-97).


Matendo ya ibada ya Hijjah na Mafunzo yatokanayo.
Kabla na wakati wa kutekeleza ibada ya Hijjah, kuna mafunzo na hatua za kuzingatia kama ifuatavyo;

i.Maandalizi na Safari ya Hijjah.
Ni lazima muislamu kabla ya kwenda Hijjah afanye maandalizi ikiwa ni pamoja na kuzidisha ucha-Mungu, kuandaa gharama, mahitaji, n.k.
Rejea Qur’an (2:197)

ii.Ihram.
Ni hali ya kuwa katika vazi rasmi na miiko kwa mwanaume mwenye Kuhiji au kufanya Umrah.
Funzo (49:13):
- Vazi la Ihram linatufunza usawa baina ya wanaadamu wote.

iii.Talbiya.
Ni kuitikia wito wa Mwenyezi Mungu (s.w) kwa kusema yafuatayo, “Labbayka Allahumma Labbayka. Labbayka laashariika laka labbayka. Innal-hamda Wanni’imata laka wal-mulka, laashariika laka”

Mafunzo (22:27) na (48:18):
-Talbiya inatufunza kumuitikia Mwenyezi Mungu (s.w) kufuata maamrisho na kuacha makatazo yake.
- Talbiya inatufunza umoja na usawa baina ya waislamu wote.

iv.Tawaf.
Ni kitendo cha kuizunguka Ka’aba mara saba kuanzia jiwe jeusi kwa mwelekeo wa kinyume na saa kwa kulibusu au kuligusa au kuashiria.

Mafunzo:
-Kuchukua ahadi ya utii kwa Mwenyezi Mungu (s.w).
-Kumtaja na kumtukuza Mwenyezi Mungu (s.w) kwa wingi.
-Inatufunza umoja, udugu na usawa baina ya wanaadamu wote.

v.Sai.
Ni kitendo cha kutembea mara saba baina vilima viwili, Saffaa na Marwaa, kwa kuanzia Saffaa na kumalizia Marwaa.

Mafunzo:
-Inatufunza utii kwa Mwenyezi Mungu (s.w).
-Inatufunza ushujaa na uhodari katika kupigania Uislamu.
-Inatufunza kuwa tayari kuhangaika kwa ajili ya kupigania Uislam

vi.Kupiga Kambi Mina, Mwezi 8 Dhul-Hijah.
Ni kitongoji kilichopo baina ya Mji wa Makkah na bonde la Arafah. Mahujaji hulala hapo na kuondoka kesho yake kuelekea Arafa asubuhi.

Mafunzo:
-Huwafunza mahujaji kuwa askari waliotayari kuacha kila chaokwa ajili ya kupigania Uislamu.
-Huwafunza mahujaji kuwa askari wanatiifu kwa Muumba wao.

vii.Kusimama Arafah, Mwezi 9 Dhul-Hija.
Arafa ni bonde lililo baina ya vilima vitatu. Mahujaji husimama humo tangu Swala ya Adhuhuri hadi Magharibi na kuomba dua mbali mbali.

Mafunzo:
-Huwakumbusha mahujaji mkutano mkuu wa siku ya Kiama.
-Hutufunza kuwa hakuna aliyebora ila amchae Mungu zaidi.
-Kisimamo cha Arafa kinatufunza usawa baina ya wanaadamu.

viii.Kupiga Kambi Mzidalfah.
Mzidalfa ni kitongoji kilicho baina ya Mina na Arafa. Mahujaji huswali Magharib na Isha hapo na kuelekea Mina mara tu baada ya swala Alfajir.

Mafunzo:
-Huwafunza mahujaj kuwa askari waliojiandaa kupambana na maadui wa Mwenyezi Mungu (s.w).
-Kuomba dua hutufunza kuwa ushindi ni kwa nusura ya Mungu tu.

ix.Kutupa Mawe Mina katika Minara Mitatu, Mwezi 10, Dhul-Hija.
Ni kitendo kinachofanyika kuanzia Mwezi 10-13, Dhul-Hija kwa kutupa vijiwe saba kila Mnara.

Mafunzo:
- Zoezi hili huwafunza mahujaj ujasiri wa kupambana na maadui zao.
- Huwafunza mahujaj pia mbinu na silaha katika kupigana na maadui.

x.Kuchinja mnyama Mwezi 10, Dhul-Hija.
Katika siku hii Hajj atanyo nywele, kuchinja mnyama, kutupa mawe kwenye Minara mitatu na kutufu Tawaful-Ifaadha (tawafu ya nguzo).

Mafunzo:
- Zoezi hili linawafunza mahujaj utiifu kwa Mwenyezi Mungu (s.w).
- Tunajifunza kuwa tayari kuua au kuuawa kwa ajili ya Mungu.
- Inatufunza kuwa na subira na kujitoa muhanga katika kunusuru dini
Rejea Qur’an (22:37) na (37:111).

xi.Siku za Tashriiq Mwezi 11-13, Dhul-Hija.
Ni kilele cha ibada ya Hija, ambapo mahujaj hupumzika kambini na kutathmini vitendo vyote walivyovifanya.

Mafunzo:
- Huwafunza mahujaj kumkumbuka Mungu baada ya kazi ngumu.
- Huwafunza askari kuwa na mazingatio na yale waliojifunza kwayo.

xii.Tawaf ya Kuaga (Tawaful-Widaa).
Ni Tawafu ya kuaga baada ya ibada ya Hija kukamilika na kujiandaa kurejea nyumbani kwa mahujaji.


Mafunzo:
-Huwafunza mahujaj kuwa viongozi (makhalifa) katika ardhi.
-Kuwa askari waliochukua mafunzo tayari kwa kuyatekeleza.
-Kuchukua ahadi ya utiifu kwa Mwenyezi Mungu (s.w).


Kwa nini wengi wanaohiji hawafikii lengo la Hijah zao?
Pamoja na mkusanyiko wa mamilioni wa mahujaj katika Mji wa Makka kila mwaka lakini matunda ya Hija hayafikiwi. Zifuatazo ni baadhi ya sababu;

i.Kuhiji kwa chumo la haramu.
Waislamu wengu hufunga safari ya kwenda hija kwa fedha za pato la haramu ambazo ni kikwazo cha kupata matunda ya hija zao.

ii.Kutochunga miiko, nguzo na sharti za Hijah.
Pamoja na kufunga safari ya Hijah au Umrah, mahujaj wengi hawachungi miiko, nguzo na masharti ya Hijah au Umrah ipasavyo.
Rejea Qur’an (2:197).

iii.Kutokuwa na elimu na ujuzi sahihi juu ya ibada ya Hijah.
Mahujaji wengi hufunga safari ya kwenda Hija au Umrah ili hali hawana ujuzi wowote wa ibada watakazozitekeleza ila kufuata mkumbo tu.

iv.Kutojulikana kwa lengo halisi la Hijah au Umrah.
Waislamu wengi hufunga safari ya Hijah au Umrah kwa lengo la kupata thawabu na kufutiwa madhambi tu na sio kuwa askari wa kupigania dini.
Rejea Qur’an (51:56).

v.Kufunga safari ya Hijah kwa Malengo mengine.
Waislamu wengi hufunga safari kwa ajili ya biashara, utalii au kutafuta umaarufu wa kujiita majina ya Al-Hajj ambayo ni nje na lengo la Hijah.



                   





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1380


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Hoja juu ya hitajio la kuzibiti uzazi na uzazi wa mpango
Soma Zaidi...

Jinsi ya kuoga josho la kiislamu ( janaba, hedhi na nifasi)
Post hii inakwenda kukufundisha jinsi ya kuoga josho kisheria. Soma Zaidi...

Hadathi ya kati na kati
Posti hiibinakwenda kukufundisha kuhusu hadathi ya kati na kati. Soma Zaidi...

malezi ya mtoto mchanga baada ya talaka
Soma Zaidi...

ijuwe maawe maan ya kusimamisha swala
Soma Zaidi...

Mambo yenye kufunguza swaumu (funga)
Soma Zaidi...

kuletewa ujumbe
(c)Kuletewa Ujumbe na Malaika kutoka kwa Allah (s. Soma Zaidi...

Hali ya kuzuiliana kurithi katika uislamu
KuzuilianaTumeona kuwa wanaume wenye kurithi ni 15 na wanawake wanaorithi ni 10. Soma Zaidi...

Uislamu unakataza mtu kulaani hovyo
20. Soma Zaidi...

Umuhimu wa swala yaani kuswali kwa mwanadamu
Kwa nini ni muhimu kuswali? Post hii itakwenda kukufundisha kuhusu umuhimu wa kusimamisha swala. Soma Zaidi...

Hukumu ya Talaka kabla ya kufanya jimai
Talaka Kabla ya Jimai:Mwanamume au mwanamke anaweza kughairi na kuamua kuvunja ndoa mapema kabla ya kufanya tendo Ia ndoa. Soma Zaidi...

Jinsi ya kiswali swala ya haja
Post hii itakufundisha kuhusu swala ya haja na jisi ya kuiswali. Soma Zaidi...