Nguzo za uislamu (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
Kwa nini wengi wanaohiji hawafikii lengo la Hijah zao?
Pamoja na mkusanyiko wa mamilioni wa mahujaj katika Mji wa Makka kila mwaka lakini matunda ya Hija hayafikiwi. Zifuatazo ni baadhi ya sababu;
Kuhiji kwa chumo la haramu.
Waislamu wengu hufunga safari ya kwenda hija kwa fedha za pato la haramu ambazo ni kikwazo cha kupata matunda ya hija zao.
Kutochunga miiko, nguzo na sharti za Hijah.
Pamoja na kufunga safari ya Hijah au Umrah, mahujaj wengi hawachungi miiko, nguzo na masharti ya Hijah au Umrah ipasavyo.
Rejea Quran (2:197).
Kutokuwa na elimu na ujuzi sahihi juu ya ibada ya Hijah.
Mahujaji wengi hufunga safari ya kwenda Hija au Umrah ili hali hawana ujuzi wowote wa ibada watakazozitekeleza ila kufuata mkumbo tu.
Kutojulikana kwa lengo halisi la Hijah au Umrah.
Waislamu wengi hufunga safari ya Hijah au Umrah kwa lengo la kupata thawabu na kufutiwa madhambi tu na sio kuwa askari wa kupigania dini.
Rejea Quran (51:56).
Kufunga safari ya Hijah kwa Malengo mengine.
Waislamu wengi hufunga safari kwa ajili ya biashara, utalii au kutafuta umaarufu wa kujiita majina ya Al-Hajj ambayo ni nje na lengo la Hijah.
Umeionaje Makala hii.. ?
Endapo mke na mume wameachana na hali ya kuwa mke ana watoto wachanga. Je uislamu unasemaje kuhusu taratibu za malezi?
Soma Zaidi...Je unadhani ni kwa nini waislamu wanaelekea kibla, na jinsi gani utaweza kukipata kibla.
Soma Zaidi...