- Uislamu ulieneza nadharia kuwa wanaadamu wote ni sawa na wote ni watumwa mbele ya Mwenyezi Mungu (s.
- Uislamu ulieneza nadharia kuwa wanaadamu wote ni sawa na wote ni watumwa mbele ya Mwenyezi Mungu (s.w).
- Uislamu ulijenga uhusiano wa udugu na upendo baina ya watu bila kujali hadhi, nafasi, rangi, taifa la mtu.
- Uislamu ulisisitiza kuwa ubora wa mtu unatokana na ucha-Mungu wake na pia mtumwa au mtu huru anastahiki kuwa kiongozi na kutiiwa ipasavyo
Rejea Qurโan (49:13) na (4:25).
- Utumwa katika Uislamu ulikuwa jambo la kupita na sio taasisi ya kudumu inayojenga matabaka ndani ya jamii.
- Uislamu uliweka mikakati ya kulinda haki, utu na hadhi ya watumwa kwa kuwafanyia wema na ihsani kama wanaadamu wengine.
Rejea Qurโan (4:36) na (49:13).
- Watumwa walikuwa na haki ya kuamini na kufuata mila au dini waipendayo bila kushurutishwa.
Rejea Qurโan (2:256).
- Watumwa walikuwa wanapata huduma za kijamii kama mavazi na malazi sawa na mabwana au wanaadamu wengine.
- Mtumwa alikuwa akikosea alisamehewa badala ya kuadhibiwa, Mtume (s.a.w) alisema mtumwa asamehewe hata mara sabini kwa siku.
- Mtumwa alistahiki kuwa kiongozi na kutiiwa ipasavyo maadamu ni muislamu na Mcha-Mungu. Mtume (s.a.w) amesema โmsikilizeni na mtiini kiongozi hata akiwa ni mtumwa wa kutoka uhabeshi, maadam anafuata njia ya hakiโ
- Uislamu unalinda hadhi ya mtumwa kwa kutomuita โEwe mtumwa wanguโ badala yake anaitwa โEwe kijana wanguโ.
- Watumwa walikuwa na haki ya kujikomboa na huru kwa njia mbali mbali zikiwemo:
1. Kulipa kiasi fulani cha pesa au mali yeyote inayokubalika.
2. Kubadilishana na mateka Waislamu waliokamatwa na maadui.
3. Kulipa fidia kwa kufanya jambo fulani lenye manufaa kwa jamii ya waislamu.
Rejea Qurโan (47:4).
- Mtume (s.a.w) na Maswahaba waliwaachia watumwa huru na kuwakomboa wengine kisha kuwaacha huru kama ifuatavyo:
1. Mtume (s.a.w) mwenyewe aliwaacha huru watumwa 63.
2. Bi Aisha (r.a) mkewe Mtume (s.a.w) aliwaacha huru watumwa 67.
3. Ibn Abbas aliwaachia huru watumwa 70.
4. Abdallah bin Umar aliwaacha huru watumwa 1,000.
5. Abdul-Rahman bin Auf alinunua watumwa 30,000 na kuwaacha huru.
Mpaka kufikia mwisho wa uongozi wa Makhalifah wa nne Waongofu, suala la Utumwa lilibakia kuwa historia katika ulimwengu wa Kiislamu.
Umeionaje Makala hii.. ?
ุนููู ุฃูุจูู ููุนูููู ุดูุฏููุงุฏู ุจููู ุฃูููุณู ุฑูุถููู ุงูููู ุนููููู ุนููู ุฑูุณูููู ุงูููููู ุตูู ุงููู ุนููู ู ุณูู ููุงูู: "ุฅููู ุงูููููู ููุชูุจู ุงููุฅูุญ...
Soma Zaidi...Huu ni utaratibu unaotakiwa kufanyika baada ya kuzika.
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukupa orodha ya vitu vilivyo najisi.
Soma Zaidi...Nguzo za uislamu, masharti ya utoaji wa zakat na sadaqat (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Haki na uadilifu katika uislamu (EDK form 3: Dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...