Sababu za wanawake kuwa na maumivu kwenye kiuno

Posti hii inahusu zaidi sababu za wanawake kuwa na maumivu kwenye viungo, ni ugonjwa unaowapata na wanaume ila kwa wanaweza unaowapata sana ukilinganisha na wanaume.

Sababu za wanawake kuwa na maumivu kwenye kiuno.

1. Kwanza kabisa ni kwa sababu ya kuwepo kwa matatizo ya hedhi, nayo uchangia kwa kiasi kikubwa kwa sababu kusudi hedhi kuwepo Kuna maumivu yanayoambatana na maumivu kwenye kiuno.

 

2. Uvimbe kwenye mayai.

Kwa sababu ya kuwepo kwa uvimbe kwenye mayai usababisha na maumivu ya kiuno kwa sababu ni vigumu kumtambua Ila mpaka kuwepo na wataalamu wa afya Ili kuweza kugundua chanzo cha maumivu ya kiuno yanayosababishwa na uvimbe kwenye mayai.

 

3. Kuwepo kwa saratani ya ovaries au fibroids kwenye uterus.

Kwa sababu ya kuwepo kwa matatizo haya usababisha pia kuwepo kwa maumivu kwenye kiuno. Kwa hiyo ni vizuri kutafuta matibabu Ili kuepuka na matatizo haya.

 

4. Pengine ni matatizo mbalimbali ya kimwili, nayo pia yanaweza kusababisha maumivu makali kwenye kiuno, matatizo hayo ni pamoja na Osteomyelitis yaani maambukizi kwenye mifupa.

 

5. Kuharibika kwa diski zilizomo Kati kati ya pingili za Uti wa mgongo ( kama vile kufuatia osteoporosis) kwa sababu mwili kwa ujumla huwa viungo vyake vinawasiliana unaweza kukuta unaumwa mgongo kumbe ni kwa sababu ya kuwepo kwa maambukizi kwenye pingili za mgongo.

 

6. Kuwepo kwa maambukizi kwenye tyuma ya uti wa mgongo.

Kwa hiyo tyuma hiyo usababisha na maumivu kwenye kiuno.

 

7. Kuwepo kwa ugonjwa wa baridi yabisi.

Pia na ugonjwa huu usababisha akina Mama kupata maumivu kwenye kiuno.

 

8. Pengine inawezekana kuwepo kwa ajali mbalimbali.kwa mfano mtu anaweza kupata ajali na kuumia sehemu ambayo imeunganika na Uti wa mgongo kwa hiyo usababisha maumivu kwenye kiuno.

 

9. Kwa hiyo tunaona wazi kuwa maumivu kwenye kiuno yanasababishwa na mambo mengi kwa hiyo ni vizuri kabisa kujua sababu ni ipi Ili kuweza kufanya matibabu ya uhakika ,  kama ni matatizo kwenye kizazi, au kama ni ajali au kama ni matatizo kwenye Uti wa mgongo, baada ya kujua tatizo na matibabu ni rahisi kufanyiwa.



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/07/11/Monday - 12:31:19 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1083


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-