Posti hii inahusu zaidi dalili za mimba inayotaka kutoka yenyewe, Kuna wakati mwingine mama anabeba mimba na mimba hiyo I atishia kutoka na huwa inaonyesha dalili mbalimbali kwa hiyo zifuatazo ni dalili za mimba kutaka kutoka yenyewe.
1. Kwanza kabisa Mama anakuwa hapati siku zake za mwezi kama kawaida ya Mama wajawazito na pia Mama uhisi maumivu kwenye tumbo hasa hasa chini ya tumbo na kwa wakati mwingine tumbo huwa na mikwaluzo Fulani ambayo ni tofauti na maumivu ya kawaida.
2.kwa wakati mwingine Mama ananza kuona damu zinatoka kwenye uke, damu hizo uanza kidogo kidogo ila kadri ya mda unavyoingezeka damu hizo pia uongezeka, kwa hiyo Mama Mjamzito anapaswa kuwahi hospital Ili kuweza kupata matibabu na msaada zaidi kwa sababu hii siyo dalili nzuri wakati wa uja uzito.
3. Kwa wakati mwingine Mama anahisi dalili za kujifunguea yaani dalili za uchungu zinaanza na wakati mimba inakuwa bado, hii dalili ya uchungu inaweza kutambuliwa hasa hasa na akina Mama ambao wamejifungua zaidi ya mara Moja ila kwa wale wanaoanza wanaweza wasitambue kama ni dalili za uchungu au la.
4. Uchafu kutoka kwenye sehemu za Siri
Kwa wakati mwingine Kuna kipindi ambapo uchafu unaanza kutoka kwenye sehemu za Siri unaweza kuwa na harufu mbaya au ya kawaida kwa hiyo uchafu huo unaweza kutumia mda mrefu au mfupi au unaweza kuwa kidogo au kiwango kikubwa.
5.mlango wa kizazi unakuwa bado umefungwa.
Kwa kawaida mimba inayotishia kutoka mlango wa kizazi kwa mara nyingi unakuwa bado umefungwa ingawa Kuna maji maji na damu ambavyo uweza kupita ila wenyewe unafunga bado.
6.Kwa hiyo kiu ambacho tunapaswa kuelewa ni kwamba mimba inayotishia kutoka ikiwa Mjamzito amewahi hospital anaweza kitibiwa na kupatiwa msaada na mimba hiyo ikahudumiwa na isitokea ila kwa wale wanaochekewa kwenda hospitalini wanaweza kupata tatizo la kupoteza mimba kwa hiyo ni vizuri kabisa kwenda hospital baada ya kuhisi dalili kama hizi wakati wa uja uzito.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi kuwepo kwa maziwa kwa akina Mama wakati wa ujauzito ni kawaida kwa sababu ya kuzaliwa kwa homoni ambayo usaidia kutoa maziwa.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu mwanamke mwenye HIV akiwa mjamzito ama anaenyonyesha
Soma Zaidi...Uchungu wa uzazi hutokana na kubana nakuachia kwa misuli hii husababishwa kufunhuka kwa mlango wa tumbo la uzazi pamoja na shingo ya kizazi na kumuongezea mama uchungu wakati wa kujifungua(during labour) Pia kubana na kuachia huanza polepole wakati wa
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi madhara ambayo yanaweza kutokea kwa sababu ya kutumia vidonge vya uzazi wa mpango kwa akina dada.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi njia za uzazi wa mpango kwa mama aliyejifungua kuanzia miezi sita mpaka mwaka mmoja.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi tatizo la kutanuka kwa tezi dume, ni tatizo ambalo linawakumba wanaume wengi kwa wakati huu kwa sababu ya kuwepo kwa maaambukizi kwenye tezi ambayo Usababishwa na vitu mbalimbali kama tulivyoona.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili za hatari kwa Mama mjamzito, ni Dalili ambazo ujitokeza kwa Mama mjamzito, hizi Dalili zisipofanyiwa kazi mapema zinaweza kuleta shida kwa Mama kwa hiyo jamii nzima inapaswa kujua Dalili hizi na kuchukua hatua endapo zitajio
Soma Zaidi...inaweza kutokea kuwa mtoto aliye tumboni akaishiwa maji hata kabla ya kuzaliwa. yes hali hii huweza kuwapata baadhiya watoto.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi uchafu unaotoka ukeni na rangi zake, kwa kawaida ukeni utolewa uchafu, uchafu huo unaweza kuwa kawaida na unaweza kuwa na rangi mbalimbali kutokana na kuwepo kwa Maambukizi.
Soma Zaidi...