Ugonjwa wa upele na matibabu yake

Ugonjwa wa upele na matibabu yake

Posti hii inahusu zaidi ugonjwa wa upele na matatibabu yake, ni ugonjwa unaosabavishwa na mdudu kwa kitaalamu huitwa mites sarcoptes scrabie mdudu huyu usababisha miwasho kwenye ngozi.

Ugonjwa wa upele.

1. Kwanza kabisa tunapaswa kujua kuwa ugonjwa huu wa upele unashambulia sana watoto  na wazee pamoja na wale wenye kinga kidogo mwilini. Kwa sababu ya uangalizi mdogo wa wazee na watoto ndo maana wanakuwa waanga wa kwanza wa ugonjwa huu.

 

2. Ugonjwa huu unaweza kusambaa kutoka kwa mtu  mmoja kwenda kwa mwingine kwa kugusana au kutumia nguo Moja yaani mwenye maambukizi ana vaa nguo na asiye na maambukizi naye anavaa kwa kufanya hivyo ugonjwa huu unaweza kusambaa sana, pia kwa wale watu wanaotumia shuka Moja wakati wa kulala wanaweza kupata ugonjwa huo kwa hiyo ni vizuri kuwa makini katika matumizi ya nguo na vitu Ili kuendelea kupambana na ugonjwa huu wa upele.

 

3. Ugonjwa huu ukitokea unaweza kitibiwa kwa dawa zifuatazo permethrin, parathyroid na pia Kuna dawa ya oral livermectin na yenyewe inasaidia kwenye matibabu, na pia tunaweza kutumia anti histamine Ili kupunguza miwasho kwa sababu Kuna wakati mwingine miwasho inakuwa mingi na yenye nguvu kwa hiyo ni vizuri kutumia dawa hiyo hata kama unatumia zingine walau miwasho ipungue.

 

4. Pia Kuna wakati mwingine usafi tu ndo dawa kama Kuna upele kwenye familia pamoja na kutumia dawa ni vizuri kabisa kufanya usafi kwa kupga kila siku kwa maji masafi na sababu pia ni lazima kifua nguo na kuzinyoosha na kihakikisha kuwa mashuka nayo yanafuliwa na ikiwezekana kuto vitu nje pamoja na magodoro walau mara Moja kwa wiki Ili kuweza kupunguza na kuondoa maambukizi.

 

5. Vile vile kwa matumizi ya dawa ni vizuri kabisa kutumia dawa hizo kwa ushauri wa wataalamu wa afya Ili kuepuka matumizi ya kiholela, kwa hiyo ni vizuri kabisa kupambana na ugonjwa huu kwa sababu unaweza kuisha kabisa.

 

6. Pia kwa wale wenye maambukizi au kinga yao inashuka hata kama wakifanya usafi ni vigumu kupona ugonjwa huu kwa hiyo wanapaswa kuwaona wataalamu wa afya Ili kuweza kupata ushauri na kupima afya zao na kuondokana na ugonjwa huu. Piaa Kuna wale wenye aleji na vitu na wanapata upele na wenyewe wanapaswa kutafuta matibabu Ili kuepuka na ugonjwa huu.

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: magonjwa Main: Post File: Download PDF Views: 4576

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉2 Simulizi za Hadithi Audio     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 kitabu cha Simulizi     👉5 Dua za Mitume na Manabii     👉6 Madrasa kiganjani    

Post zinazofanana:

Homa ya matumbo (Typhoid): Dalili na jinsi inavyoambukizwa.

​Homa ya matumbo, inayojulikana kitabibu kama Typhoid Fever, ni ugonjwa hatari wa kuambukiza unaosababishwa na bakteria aina ya Salmonella Typhi. Makala hii inatoa mwongozo wa kina kuhusu namna bakteria hawa wanavyosambaa kupitia vyakula na maji yaliyochafuliwa, dalili za kliniki unazopaswa kuzizingatia, pamoja na umuhimu wa usafi wa mazingira na chanjo katika kuzuia maambukizi haya. Lengo letu ni kukupa elimu itakayokusaidia kujilinda wewe na jamii yako dhidi ya maradhi haya yanayoweza kuzuilika.

Soma Zaidi...
Matibabu ya vidonda vya tumbo

Makala hii inakwenda kukufundisha kuhusu matibabu ya vidonda vyatumbo. Pia utajifunza kwa nini kunakuwa na vidonda vya tumbo sugu.

Soma Zaidi...
Aina ya kisukari inayojulikana kama Diabety type 1

Post hii inahusu zaidi ugonjwa wa kisukari Aina ya kwanza ambapo kwa kitaalamu huitwa Diabetes type 1, ni hali ambayo utokea ambapo mwili ushindwa kutengeneza insulini ambayo uweka sukari kwenye hali ya usawa.

Soma Zaidi...
Kulegea kwa mwili na uchovu wa mara kwa mara: Chanzo chake.

Uchovu wa mara kwa mara na hali ya kulegea kwa mwili ni malalamiko ya kawaida yanayoweza kuashiria changamoto za kifizikia, kisaikolojia, au mtindo wa maisha. Makala haya yanachunguza visababishi vya ndani na nje vya hali hii, umuhimu wa utambuzi sahihi, na mikakati ya kitaalamu ya kurejesha nishati na ustawi wa mwili.

Soma Zaidi...
Ugonjwa wa Saratani ya ini.

Saratani ya ini ni Saratani inayoanzia kwenye seli za ini lako.

Soma Zaidi...
Ujuwevmv ugonjwa Nimonia na dalili zake

Nimonia ni Hali ya kuvimba pafu inayoathiri hasa vifuko vya hewa viitwavyo Alveoli, husababishwa na Maambukizi ya virusi

Soma Zaidi...