Huduma kwa wanawake wenye mahitaji maalum.
Posti hii inahusu huduma kwa wanawake wenye mahitaji maalum, ni wanawake ambao wana shida ya akili, walionyanyaswa kijinsia, wakimbizi na wote wenye matatizo mbalimbali.
Huduma kwa wanawake wenye matatizo mbalimbali.
1.Tunajua kuwa hawa wanawake wanahitaji uangalizi kwa karibu kwa hiyo tunapaswa kuwasaidia katika kujieleza, katika kutembea labda wengine ni walemavu, katika kujifanyia mambo ya kawaida ya usafi na namna ya kufanya usafi na katika maamuzi maana wengine wana shida ya kutoa uamuzi.
2.Pia inabidi kuwasaidia katika wakati uliopo kwa tatizo lililopo kwa mfano kama mama anahitaji huduma za vipimo anapaswa kusaidiwa kwa sababu wakati mwingine hawezi kufika sehemu za vipimo na kuweza kujieleza kwa hiyo anapaswa kusaidiwa na kuhakikisha kuwa anapata kila kitu anachokihitaji.
3.Kumsaidia Mama kujua umuhimu wa kupima virus vya ukimwi na magonjwa ya zinaa na namna ya kuzuia magonjwa hayo kwa hiyo hawa akina Mama wanapaswa kupewa elimu ili waweze kupima na kujua afya zao na kama wana Maambukizi wanapaswa kujua namna ya kuwalinda watoto wao na matumizi ya dawa za ARV.
4.Kuwasaidia hawa wakina Mama wenye matatizo kuchagua aina bora ya uzazi wa mpango kwa kadiri ya hali yake na kuwasaidia namna ya kutumia njia hizo na kuwa na idadi ya watoto wanaowahifadhi kwa hiyo hawa akina Mama wanapaswa kuwa na uangalizi wa karibu zaidi katika kutumia uzazi wa mpango.
5.Pia jamii inapaswa kuwahudumia hawa wajawazito wenye mahitaji maalum ili waweze kujifungua salama na kuepuka imani potovu ya kutoa mimba kwa wajawazito ambao wana kifafa na wenye matatizo kwa kuepuka kulea watoto wao kwa hiyo wanapaswa kutumia njia za uzazi wa mpango ili wasizae sana, kwa hiyo jamii inapaswa kuwapokea watu hawa kwa sababu nao ni binadamu wanahitaji haki zote kama walivyo binadamu wengine.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Kitabu cha Afya 👉2 kitabu cha Simulizi 👉3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉4 Bongolite - Game zone - Play free game 👉5 Dua za Mitume na Manabii 👉6 Simulizi za Hadithi Audio
Post zinazofanana:
Madhara ya ugonjwa wa madonda ya koo usipotibiwa
Posti hii inahusu zaidi madhara ya ugonjwa wa madonda ya koo usipotibiwa, ugonjwa huu usipotibiwa unaweza sababisha madhara mbalimbali kama ifuayavyo.
Soma Zaidi...Fangasi watambulikao kama invasive candidiasis
Hawa huweza kuingia kwenye mfumo wa damu na kuenda maeneo mengine nyeti sana ya mwili.
Soma Zaidi...Namna ya kujikinga na ugonjwa wa madonda ya koo
Post hii inahusu zaidi namna ya kuzuia ugonjwa wa madonda ya koo,ni njia ambazo usaidia katika kujikinga na ugonjwa wa madonda ya koo.
Soma Zaidi...FIKRA POTOFY KUHUSU VIDONDA VYA TUMBO
FIKRA POTOFY KUHUSU VIDONDA VYA TUMBO Vidonda vya tumbo huja na maoni mengi potofu.
Soma Zaidi...Kulegea kwa mwili na uchovu wa mara kwa mara: Chanzo chake.
Uchovu wa mara kwa mara na hali ya kulegea kwa mwili ni malalamiko ya kawaida yanayoweza kuashiria changamoto za kifizikia, kisaikolojia, au mtindo wa maisha. Makala haya yanachunguza visababishi vya ndani na nje vya hali hii, umuhimu wa utambuzi sahihi, na mikakati ya kitaalamu ya kurejesha nishati na ustawi wa mwili.
Soma Zaidi...Matatizo ya kisaikolojia kwa watoto (mfano, ADHD): Dalili zake.
Afya ya akili ya watoto ni msingi wa maendeleo yao ya baadaye. Katika ulimwengu wa sasa, matatizo ya kisaikolojia kama ADHD (Upungufu wa Umakini na Usikivu) yanazidi kuongezeka, lakini mara nyingi huchanganyikiwa na utovu wa nidhamu. Makala haya yanalenga kutoa mwongozo wa kitaalamu kuhusu dalili za matatizo ya kisaikolojia kwa watoto, yakigusia kwa kina hali ya ADHD na jinsi wazazi wanavyoweza kutofautisha kati ya tabia za kawaida za utotoni na changamoto zinazohitaji msaada wa kisaikolojia.
Soma Zaidi...