Dalili za tezi dume na sababu za kutokea kwa tezi dume.

dalili za ugonjwa wa tezi dume, na sababu za kutokea kwa tezi dume, maana ya tezi dume na athari zake

Dalili za tezi dume na sababu za kutokea kwa tezi dume.

TEZI DUME SIO BUSHA, ZIJUWE DALILI ZA TEZI DUME



Watu wengi wamekuwa wakidhania kuwa tezi dume ni busha ama ngiri maji kwa jina jinngine. Hapana hii sio sahihi kabisa. Mpenzi msomaji tambuwa kuwa tezi dume sio busha na haifananni kabisa na busha. Tezi dume isipotibiwa kwa haraka inaweza kuwa hatari sana kwani ina maumivu makali sana. Sasa nini hasa hii tezi dume?. katika makala hii nitakwenda kukupa mwangaza kuhusu tezi dume., dalili za tezi dume na athari za tezi dume kwa afya ako.


Nini maana ya tezi dume
Tezi hii kitaalamu hufahamika kama prostate gland. Hii ni tezi inayopatikana katika mfumo wa uzazi wa kiume. Tezi hii inapatikana jirani na kibofu cha mkojo na mirija ya mkojo. Tezi hii ina kazi ya kuzalisha majimaji ambayo hubeba mbegu za kiume. Majimaji haya ndio yale anayotoa mwanaume anapofikia kilele. Hivyo tezi hii ni muhimu sana katika mfumo wa kizazi wa mwanaume. Tezi hii si kubwa saana inapata sentimita zisizozidi 5. lakini tezi hii hukuwa kadiri umri unavyoenda.


Kwa ufupi wa maneno ni kuwa tezi dume ipo zini ya kibofu karibu na shingo ya kibofu. Na imezunguka mrija unaotoa mkojo kutoka kwenye kibofu kuja nje (urethra). hivyo mkojo unapotoka kwenye kipofu hipitia katikati kwenye tezi dume ukiwa kwenye mrija wa urethra. Urethra ndio mrija unaotoa mkojo kutoka kwenye kibofu.


Vipi ugonjwa wa tezi dume hutokea?
Kama ulivyojifunza hapo juu mkojo ukiwa kwenye mrija hupita katikati ya tezi tume. Sasa tezi hii ina kawaida ya kukuwa kadiri mtu anavyopata umri zaidi. Hivyo basi kadiri tezi hii inapoongezeka ukubwa ndivyo inavyoanza kuminya mirija ya kupitisha mkojo na hatimaye huanza tatizo la ugonjwa wa tezi dume. Tatizo hili kitaalamu hufahamika kama Benign Prostatic Hyperplasia (BPH).


Nini sababu za kutokea kwa tezi duma?
Kama ilivyokwisha kutajwa hapo juu, tezi hii hukuwa kadiri mtu anavyokuwa. Kwa baadhi ya watu inapokuwa huwa kubwa kiasi cha kuanza kuminya mirija ya mkojo na kuleta shida kwenye mfumo wa mkojo. Tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa miongoni mwa mambo yanayohatarisha uwezekano wa kupata ugonjwa huu ni haya yafuatayo:-



1.Umri, kikawaida tezi dume huwapata watu wenye umri kuanzia miaka 40. ni mara chache sana kuwapata walio chini ya umri huo. Pia tezi dume kwa kiasi kikubwa huwapata walio kati ya miaka sitini na kuendelea. Hususan robo tatu ni wale walio na miaka kuanzia 60,na nusu yao ni wale walio na miaka kuanzia 80.



2.Tatizo la tezi dume pia huweza kurithiwa. Yaani kama baba yako ana tezi dume ama yeyote katika damu yako hapo mwanzo alikuwa na tezi dume, hivyo upo uwezekana na wewe kurithi tatizo hili.



3.Pia inaonakana kuwa baadhi ya rangi huathiriwa sana na tatizo la tezi dume. Tafiti zinaonesha kuwa watu walio katika bara la Asia si sana kupatwa na tezi dume kuliko watu weusi na wazungu. Hata hivyo kwa watu weusi upo uwezekano wa kupatwa na tatizo hili katika umri mdogo kuliko wengine.



4.Maradhi, tafiti zinaonyesha kuwa kuna baadhi ya maradhi huweza kupelekea kupatwa na tatizo la tezi dume. Kwa mfano watu wenye maradhi ya sukari, na maradhi ya moyo wapo hatarini kupatwa na tezi dume ukilinganisha na watu wengine.
5.Staili za maisha. Tafiti pia zinaonyesha kuwa watu wenye kiribatumbo na wasiofanya mazoei wapo hatarini kupatwa na tatizo la tezi dume.


Ni zipi dalili za ugonjwa wa tezi dume?
Dalili za tezi dume zinaweza kuwa kali ama hafifu kutoka mtu hadi mtu. Ukali wa dalili hizi hautegemei ukubwa wa tezi. Inaweza kuwa tezi ni kubwa lakini dalili zisiwe kali. Miongoni mwa dalili za tezi dume ni:-



1.Kukojoa mara kwa mara, ama kuhisi kukojoa mara kwa mara
2.Kukojoa mara kwa mara wakati wa usiku
3.Kupatwa na uzgumu kutoa mkojo
4.Mchirizi wa mkojo kuwa dhaifu
5.Mkojo kukatakata unapofika karibu a mwisho
6.Kujichafua wakati wa kukojoa
7.Kushindwa kumaliza mkojo kabisa.
8.Damu kwenye mkojo
9.Kushindwa kukojoa kabisa.
10.Kupata mkojo mchache sana


Kuwa na dalili tajwa hapo juu pekee hakuwezi kukupa uhakika kuwa una tatizo la tezi dume. Kwani dalili tajwa hapo juu zinaweza kuambatananna shida nyingine za kiafya kwa mfano:-
1.Maambukizi ya UTI
2.Kuvimba kwa tezi
3.Kupunguwa ukubwa wa mrija wa mkojo
4.Kuwepo na vijiwe kwenye kibofu
5.Kuwa na shida kwenye mfumo wa neva ambazo hudhibiti ufanyaji kazi wa kibofu
6.Kuwa na saratani
7.Kama upasuaji katika kibofu haukufanyika sawa.


Ni zipi athari za tezi dume kama haitawahi kutibiwa?
Tezi dume ni kama maradhi mengine, inatibika bila wasi. Hata hivyo endapo matibabu yatachelewa athari zifuatazo zinaweza kupatikana:-
1.Kushindwa kabisa kukojoa
2.Kupatwa na maambukizi ya UTI
3.Kupatwa na vijiwe kwenye kibofu
4.Uharibifu wa kibofu unaweza kutokea
5.Figo inaweza kuharibika


Mwisho
Mwisho napenda kumaliza kwa kusema kuwa tatizo la tezi dume linatibika bila wasi. Zipo dawa za hospitali mgonjwa anaweza kupewa. Kamatatizo lake ni kubwa zaidi anaweza kufanyiwa upasuaji. Usisite kutembeleabongoclass.com kwa makala nyingine za aya




Download kitabu cha Afya na Magonjwa
bofya hapa



                   


Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Uzazi Main: Afya File: Download PDF Views 5601

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio    👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉3 Madrasa kiganjani    👉4 kitabu cha Simulizi    👉5 Kitau cha Fiqh    👉6 Bongolite - Game zone - Play free game   

Post zinazofanana:

Kwa mjamzito kuumia wakati wa tendo la ndoa tatizo linaweza kuwa ni nini?

Je unaweza kunielezaKwa mjamzito kuumia wakati wa tendo la ndoa tatizo linaweza kuwa ni nini?

Soma Zaidi...
Mama mjamzito anapo hisi uchungu je mtoto huendelea kucheza tumboni?

Swali langi ni hiliMama mjamzito anapo hisi uchungu je mtoto huendelea kucheza tumboni?

Soma Zaidi...
Nini husababisha maumivu ya uume

Kama uume wako unauma ama unahisi kuwa unaunguza ama kuchoma choma, post hii imekuandalia somo hili.

Soma Zaidi...
Zijue mbegu za kiume zilizo bora.

Posti hii inahusu zaidi mbegu ambazo ni nzima na ambazo zina sifa ya kutungisha mimba kwa hiyo mbegu hizi utazigundua kwa kuwa na sifa zifuatazo.

Soma Zaidi...
Sababu za kuongezeka uzito wa wajawazito.

Posti hii inahusu zaidi sababu za kuongezeka uzito kwa wajawazito, Mara nyingi Mama akibeba mimba uongezeka uzito kutoka wiki ya Kwanza mpaka wiki ya mwisho ya kujifungua.

Soma Zaidi...
Ni ipi hasa siku ambayo nitafute ujauzito

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu siku za kutafuta ujauzito

Soma Zaidi...
Upungufu wa homoni ya estrogen

Posti hii inahusu zaidi upungufu wa homoni ya estrogen na dalili zake, aina hii ya homoni ikipungua mwilini uleta madhara na matatizo mbalimbali kwenye mwili.

Soma Zaidi...
Huduma kwa mama mwenye mimba Inayotishia kutoka.

Post hii inahusu zaidi huduma ambayo Mama anapaswa kutolewa pindi mimba inapotishia kutoka huduma hii utolewa kulingana na Dalili tulizoziona zinazohusiana na mimba kutishia kutoka.

Soma Zaidi...
Changamoto za ujauzito

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu changamoto za ujauzito na dalili zake endelevu

Soma Zaidi...