KUWAHI KUMALIZA TENDO LA NDOA MAPEMA

Hii ni hali inayowapata sana wanaume huwa wanamaliza hamu ya tendo la ndoa mapema kabla ya mwenza kuridhika. Hii hutokea pale mwanaume anapomwaga mbegu mapema sekunde chache ama muda mchache baada ya kuingiza uume ukeni. Wengi wenye tatizo hili humwaga ndani ya dakika moja na tatizo huwa baya zaidi kwa wengine ambao humwaga ndani ya sekunde 30 baada ya kuingi za uume. Hali hii kitaalamu hujulikana kama premature ejaculation.

 

Hali hii huweza kuambatana na mambo mengi hususani matatizo ya kisaikolojia, maradhi ama maumbile. Wakati mwingine hali hii humpata mwanaume yeyote hata kama sio muathirika wa tatizo hili. Ila hii huwa ni tatizo kama hali hii itakuwa inajirudia rudia muda mwingi.

 

Sababu za tatizo hili:

  1. matatizo kwenye mfumo wa homoni
  2. Maradhi na kuwepo uvimbe kwenye korodani
  3. Kurithi tatizo hili kwenye familia
  4. Kuwa na msongo wa mawazo
  5. Kuwa na tatizo la uume kunywea mapema
  6. Uwoga na msongo wa mawazo
  7. Kutokupendezewa na umbo la mwenza
  8. Mahusiano yaliyo mabovu
  9. Kuogopa kumaliza tendo mapema