KUKOSA NGUZU ZA KIUME NA SABABU ZAKE

Hii ni hali inayowapata wanaume kushindwa kuhimili tendo la ndoa. Hii huwenda kuwa uume unashindwa kusimama (kutisa) kwa kwa muda mrefu, ama unashindwa kabisa kusimama. Kitaalamu hali hii hufahamika kama erectile dysfunction. Hali hii haihusishi wale wenye tatizo la kumaliza hamu mapema (premature ejaculation) yaani wanaomaliza haja yao hata kabla ya mwenza kuridhika.

 

Sababu za tatizo hili:

 1. Kuwa na maradhi ya moyo
 2. Kuziba kwa mishipa ya damu (atherosclerosis)
 3. Kuwa na mafuta mengi mwilini (high cholesterol)
 4. Kuwa na presha ya kupanda (high blood pressure)
 5. Kisukari
 6. Matumizi ya baadhi ya madawa
 7. Uvutaji wa sigara
 8. Maradhi kwenye uume kama peyronie
 9. Unywaji wa pombe
 10. Utumiaji wa madawa ya kulevya
 11. Matibabu ya saratani ya korodani
 12. Upasuaji katika maeneo nyeti au ugwe mgongo
 13. Kuwa na mdongo wa mawazo ama woga
 14. Mahusiano yasiyo mazuri
 15. Kuwa na uzito kupitiliza