Wajawazito wamekuwa wakisumbuliwa sana na kiungulia, makala hii itakujulisha njia za kukabiliana na kiungulia, dalili zake na dawa zake
Dawa ya kiungulia kwa wajawazito.
Kiungulia ni moka katika matatizo yanayotokea katika mfumo wa chakula. Kiungulia si katika mambo ya hatari, ila huwa ni hali sumbufu sana hasahasa kwa wajawazito. Kama na wewe unasumbuliwa sana na kiungulia makala hii ni kwa ajili yako. Hapa tutaoa sababu za kiungulia, matibabu yake na njia za kuepuka kiungulia.
Nini husababisha kiungulia cha mara kwa mara kwa wajawazito?
1.Ni kuwa wakati wa ujauzito kuna mabadiliko mengi ya homoni yanatokea kwa mwanamke. Mabadiliko haya yanapelekea misuli ya kooni inayounganisha tumbo na koo, kujiachia mara kwa mara na hivyo kusababisha tindikali iliyopo tumboni kupanda juu, na kusababisha kiungulia. Hali hii huweza ktokea sana pale unapolala baada ya kula chakula kingi.
2.Kadiri mtoto anavyoendelea kukuwa na mimba inavyosonga mbele ndivyo mtoto anaongeza mkandamizo kwenye tumbo. Hali hii inapelekea tindikali iliyopo tundoni kusukumwa kupanda juu na hatimaye kusababisha kiungulia.
Je ujauzito unasababisha kiungulia?
Hapana, ujauzito hausababishi kiungulia ila unaongeza uwezekano wa kupata kiungulia. Kivipi?, ni hivi mwanzoni mwa ujauzito koo lako linachukuwa chakula kidogokidogo, na kwa kuwa kuna mabadiliko mengi yanatokea husababisha mmeng’enyo wa chakula kufanya kazi kidogokidogo hivyo kuchelewa kukimeng’enya chakula kwa haraka. Hali hii husaidia mwali kupata muda wa kutosha kufyonza chakula na kukipeleka kwa mtoto, ila kwa upande mwingine hali hii husababisha kiungulia.
Hata hivyo si kila mjamzito atakuwa anasumbuliwa na kiungulia, ni kwa sababu kuna mambo mengi yanafngamanna na kiungulia. Hali namna ambavyo mjamzito anaishi inaweza kuchangia kupata kiungulia. Namna mtu alivyo, vyakula anavyokula, namna anavyolala na hata mavazi pia yanaweza kuchangia kupata kiungulia.
Mjamzito afanye nini kuepuka kiungulia?
1.Kla kidogo kidogo mara kwa mara na hakikisha hunywi maji wakati wa kula
2.Kula kidogo na hakikisha unatafuna kila tonge kwa ufanisi zaidi
3.Wacha kula unapokaribia kulala
4.Punguza kula vyakula kama chokoleti, vyenye mafuta mengi, vyenye pilipili na vyenye uchachu
5.Usilale baada ya kula angalau unaweza kusimama ama kutembea.
6.Wacha kuvaa nguo za kubana sana
7.Unapolala hakikisha kichwa chako kinakuwa juu, unaweza kutumia mto ama mfano wake
8.Unapolala lalia ubavu wa kushoto
9.Tafuna bigji zisizo na sukari baada ya kula
10.Kunywa maziwa kama unayo unapohisi kiungulia
11.Kunywa asali kama unayo unapohisi kiungulia.
Dawa za kutibu kiungulia
Unaweza kutibu kiungulia kwa kutumia antacid kama vile Tums, Rolaids na Maalox.dawa ambazo zimetengenezwa kwa madini ya calcium carbonate au magnesium ni nzuri pia. Magnesium si nzuri kama ujauzito upo mwishoni.
Madaktari wengi wanakataza matumizi ya antacid ambazo zimechanganywa na sodium, ama zila lebo ya aluminium carbonate kwani zinawza kupelekea kukosa choo. Pia dawa hizi za kiungulia zinakatazwa kwa wajawazito Alka-Seltzer.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
 Posti hii inazungumzia kuhusiana na kuvimba kwa ovari kunakosababishwa na maambukizo ya bakteria na kawaida huweza kusababishwa na magonjwa sugu katika Maambukizi ya mfumo wa Uzazi wa mwanamke.
Soma Zaidi...Tezidume ni moja ya magonjwa hayari yanayotokea katika mwili wa mwanaume.Hapa nimekuandalia sababu za kutokea kwa tezi dume.
Soma Zaidi...Miongoni mwa dalili zamwanzo za ujauzito ni maumivu ya tumbo ama kupatwa na damu kidogo. Mabadiliko ya ute ute sehemu za siri ni katika baadhi ya dalili. Endelea na makala hii utajifunza zaidi.
Soma Zaidi...Je ni kweli kupima kimoja cha mloka kinaweza kupima mimba zaidi ya mara moka?
Soma Zaidi...Habari DoktaNikuulize kituu?
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi sababu za kuvunjika kwa mtoto wakati wa kuzaliwa, kuna wakati mtoto anapozaliwa anaweza kuvunjika kwenye sehemu mbalimbali kwa sababu zifuatazo.
Soma Zaidi...Maumivu ya tumbo kwa mjamzito huweza kuanaa kuonekana mwanzoni kabisa mwaujauzito, ndani ya mwezi mmoja. Ikabidi si dalili pekee ya kuwa ni mjamzito.
Soma Zaidi...Kichefuchefu ni moja katika dalili za mimba za mapema, Lucinda je upo uwezekano kwa mwanamke kuwa na ujauzito bila hata ya kuwa na kichefuchefu?
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi mambo muhimu ambayo tunapaswa kujua au kufahamu kuhusu mbegu za kiume, kwa kuwa mbegu za kiume usaidia katika utungaji wa mimba kwa hiyo ni vizuri kabisa kuzitunza Ili kuweza kuepuka matatizo mbalimbali ambayo yanaweza kutokea kwa s
Soma Zaidi...