VYAKULA VYA KUONGEZA HAMU YA TENDO LA NDOA NA NGUVU ZA KIUME
Matatizo yahusianayo na nguvu za kume na kukosa hamu ya tendo la ndoa kwahuweza kuchangiwa sana na mpangilio mbovu wa vyakula pamoja na saikolojia ya mtu.
Vyakula vya kuongeza nguvu za kiume na hamu ya tendo la ndoa
Matatizo yahusianayo na nguvu za kume na kukosa hamu ya tendo la ndoa kwahuweza kuchangiwa sana na mpangilio mbovu wa vyakula pamoja na saikolojia ya mtu. Ni vyema kujiweka tayari kisaikolojia kabla ya kushiriki tendo la ndoa. Kwa upande wa vyakula ni vyema kuchaguwa vyakula vilivyo salama kwa afya. Vyakula vyenye mafuta kupitiliza vinaweza kuleta athari mbaya kwa afya ya nguvu za kiume. Katika makala hii nitakuletea vyakula vitano ambavyo husaidia katika kuongeza hamu ya kushiriki tendo la ndoa:
Vyakula hivyo ni:
1. Vyakula vyenye arginine . Vyakula hivi vina ni vyakula vyenye chembechembe itambulikayo kama arginine. Ndani ya miili yetu arginine huweza kubadilishwa kuwa oxide ya nitric (nitric oxide). Arginine ni chembechembe za asidi ya amono (amino acid). vyakula vyenvye arginine ni kama maharage ya soya, mbegu za maboga, karanga, korosho, samaki, nyama, kuku na samaki.
Arginine imafaida nyingi sana mwilini. Chembechembe hii huweza kutibu tatizo la kusinyaa kwa uume kabla ya kumwaga, ama kusinyaa mapema, ama kugoma kabisa kusiama. Kama tatizo hili linahusiana na mishipa ya damua kama kuziba kwa mishiba ya damu basi arginine ni msaada mkubwa. Pia husaidia kuimarisha afya kwa wenye kisukari na wenye maradhi ya moyo hususani yanayohusiana na mishipa ya damu kama kujaa mafuta ama kuziba.
2. Vyakula vyenye phytochemical: vyakula hivi ni kama maepo (apples),mboga za apricots, broccoli, Brussels sprouts, kabichi (cabbage), karoto (carrots), cauliflower, kitunguu thaumu (garlic), mimea jamii ya kunde (legumes), kitunguu maji (onion), pilipili kali (red peppers), maharage ya soya (soybeans), viazi vitamu (sweet potatoes), na nyanya (tomatoes).
3. Vyakula vya fati iliyo salama kwa afya ya moyo. Afya ya moyo huchukuwa nafasi kubwa katika tendo la ndoa. Uzima wa moyo huweza kufanya damu kutembea vyama maeneo yote ya mwili hususani maeneo yanayohusika katika tendo la ndoa.
Miongoni mwa vyakula hivi ni palachichi. Ndani ya palachichi kuna fat, vitamini B6 asidi ya folik (folic acid) kwa hamoja hizi husaidia kuongeza nishati mwilini na kuimarisha afya katika kushiriki tendo la ndoa. Vyakula vingine ni kama aina flani ya samaki, mayai, mbegu za chia, chokleti, bidhaa za maziwa kama siagi n.k
4. Vyakula vyenye citrulline aina ya asidi za amini (amino acid): hii ni chembechembe inayopatikana kwenye vyakula hivi, mwili hubadilisha chembechembe hii ni kuwa arginine. Faida za arginine tumeshaziona hapo juu. Chemikali hizi pia husaidia katika kuufanya mwili uweze kuwa shwari (relax) kama vile viagra inavyofanya kazi.
Miongoni mwa vyakula hivi ni tikitimaji. Tunda hili lina citrulline kwa wingi sana tofauti na matunda mengi. Vyakula vingine ni kama maboga, matang n.k. citrulline pia husaidia katika kutanua misuli na kuboresha mishipa ya damu kufanya kazi vyema hivyo ni nzuri kwa wanaofanya mazoezi. Kwa upande wa afya ya tendo la ndoa husaidia katika kupeleka damu kwenye maeneo nyeti.
5. Vyakula vyenye Indole-3-carbinol: hii husaidia katika kuboresha homoni hasa kwa wanaume. Huweza kupatikana kwenye mboga za majani kama kabichi, broccoli na mboga nyinginezo. Tofauti na faida hizi pia huweza kusaidia katika kuzuia na kupunguza athari za saratani ya matiti, tumbo, na nyinginezo.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Simulizi za Hadithi Audio 👉2 Kitau cha Fiqh 👉3 Madrasa kiganjani 👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉5 ai web app 👉6 Dua za Mitume na Manabii
Post zinazofanana:
Dalili za kuziba kwa mirija ya uzazi
Posti hii inahusu zaidi dalili ambazo zinaweza kutokea kwa sababu ya kuziba kwa mishipa ya uzazi, ni baadhi ya dalili ambazo ujitokeza kwa sababu ya kuwepo kwa tatizo la kuziba kwa mishipa ya uzazi.
Soma Zaidi...Kuwepo kwa maziwa wakati wa ujauzito.
Posti hii inahusu zaidi kuwepo kwa maziwa kwa akina Mama wakati wa ujauzito ni kawaida kwa sababu ya kuzaliwa kwa homoni ambayo usaidia kutoa maziwa.
Soma Zaidi...Dalili za Mimba ya Siku 7 kwa Mwanamke
Kipindi cha siku saba baada ya kurutubishwa kwa yai (karibu wiki moja tangu kutunga kwa mimba) ni hatua ya mwanzo kabisa ambapo kijusi kinaanza kujipandikiza kwenye mji wa mimba. Ingawa mara nyingi ni mapema mno kwa vipimo vya mkojo kuonyesha matokeo chanya, mwili wa mwanamke unaweza kuanza kuonyesha dalili fiche za kibaolojia. Makala hii inaelezea kile kinachotokea mwilini mwako katika kipindi hiki cha siku saba.
Soma Zaidi...Namna ya kutunza joto la mtoto mara tu baada ya kuzaliwa.
Posti hii inahusu zaidi njia ambazo zinaweza kutumika ili kuweza kutunza joto la mtoto mara tu anapozaliwa,tunajuwa wazi kuwa Mama anaweza kujifungulia sehemu yoyote ile kabla hajafika hospitalini kwa hiyo mtoto anapaswa kuwa na joto la mwili la kutosha i
Soma Zaidi...Je, wajua sababu zinazopelekea maumivu ya Matiti kwa wanawake?
Maumivu ya matiti ni malalamiko ya kawaida miongoni mwa wanawake yanaweza kujumuisha uchungu wa matiti, maumivu makali ya kuungua au kubana kwenye tishu zako za matiti. Maumivu yanaweza kuwa ya mara kwa mara au yanaweza kutokea mara kwa mara tu. Maumiv
Soma Zaidi...Dalili za tezi dume.
Posti hii inahusu zaidi Dalili ambazo anaweza kuzipata mwenye Ugonjwa wa tezi dume, sio Dalili zote mtu anaweza kuzipata kwa sababu dalili kama hizi zinaweza kujitokeza hata kwa magonjwa mengine.
Soma Zaidi...