Namna ya kutibu kuharisha kwa mtoto ukiwa nyumbani.

Post hii inahusu zaidi njia za kutibu kuharisha kwa watoto wakiwa nyumbani, kwa sababu mara nyingine mtoto anaweza kuharisha si kwa sababu ya kuwepo kwa Maambukizi ila ni uchafu tu kwa hiyo njia muhimu zinazofaa kutibu mtoto ni pamoja na yafuatayo.

Njia za kutibu au kuzuia kuharisha wakiwa nyumbani,

1.Kwanza kabisa tunajua kuwa watoto wanaweza kupata matatizo mbalimbali ya kiafya hasa kuharisha ambapo wasipotibiwa mapema wanaweza kupoteza maji mwilini na kusababisha madhara makubwa kwa hiyo ikitokea mtoto akaanza kuharisha fanya yafuatayo.

 

2. Mpatie mtoto vitu mbalimbali vya majimaji.

Vitu vya majimaji kama vile kumnyonyesha mtoto mara kwa mara kumpatia mtoto Oral solution au unaweza kumpatia maji masafi, kumpatia vyakula vya majimaji kama supu, maji ya mchele, maziwa,na kama mtoto hajafikia wakati wa kula unampatia mda mwingi wa kunyonya.

 

3. Wakati wa kumlisha mtoto unapaswa kumpa kidogo kidogo kwenye kijiko na pia ukiona anatapika unapaswa kumpumzisha mpaka dakika kumi zipite na endelea kumpa vitu vya maji maji mpaka kuharisha kuishe ila hali ya kuharisha ikiendelea mpeleke mgonjwa hospitalini kwa matibabu zaidi.

 

4. Mpatie mtoto zink 

Zink anapaswa kutumia mtoto mwenye umri wa kuanzia miezi miwili mpaka mwaka mmoja , mtoto wa miezi miwili mpaka miezi sita wanapaswa kutumia wanapaswa kutumia nusu ya kidonge mpaka siku kumi na nne na kuanzia miezi sita mpaka na kuendelea wanapaswa kutumia kidonge kimoja kwa siku kumi na nne.

 

5.Kwa hiyo pamoja na kutumia tiba hii ikifanikiwa utaendelea kuitumia isipofanikiwa basi mtoto anapaswa kupelekwa hospitalini na kupata matibabu kwa sababu mtoto akiishiwa maji mwilini ni shida na tunaweza kupata matatizo mengine makubwa

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Uzazi Main: Afya File: Download PDF Views 16398

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio    👉2 Kitabu cha Afya    👉3 Bongolite - Game zone - Play free game    👉4 Madrasa kiganjani    👉5 Dua za Mitume na Manabii    👉6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina   

Post zinazofanana:

Je mjamzito Uchungu ukikata inakuwaje

Hutokea uchungu wa kujifunguwa ukakati. Unadhani ni kitugani kinatokea.

Soma Zaidi...
Dalili za kasoro ya moyo ya kuzaliwa kwa watu wazima

Ugonjwa wa moyo wa kuzaliwa nao (kasoro ya moyo ya kuzaliwa) ni hali isiyo ya kawaida katika muundo wa moyo wako unaozaliwa nao. utu uzima. Ingawa maendeleo ya kimatibabu yameboreshwa, watu wazima wengi walio na ugonjwa wa moyo wa kuzaliwa wanaweza wasip

Soma Zaidi...
Nimetoka kufanya tendo la ndoa ghafla tumbo likaanza kukaza upande wa kushoto na kutoka maji yenye uzito wa kawaida kama ute mengi je hii itakuwa ni nini

Maumivu yavtumbo huwenda yakachanganya sana, Keane yanahusianana sababu nyingi sana. Kina baadhi ya watu hupata na maumivu ya tumbo wakati wa tendo la ndoa ama punde tu baada ya kumaliza.

Soma Zaidi...
Utaratibu wa kushiriki tendo la ndoa kwa wajawazito

Jifunze muda ambao mjamzito hatatkiwa kishiriki tendo la ndoa. je kuna madhara kwa mjamzito kushiriki tendo la ndoa.

Soma Zaidi...
Zifahamu fibroids (uvimbe kwenye via vya uzazi)

Posti hii inahusu zaidi fibroids au uvimbe kwenye via vya uzazi hasa hasa utokea kwenye tumbo la uzazi ambapo kwa kitaalamu huitwa uterusi, uvimbe huu ulitokea watu wengine huwa hawawezi kutambua Dalili zake mapema kwa hiyo leo tunapaswa kujua Dalili zake

Soma Zaidi...
Jinsi ya kuongeza nguvu za kiume

Post hii itakwenda kukuletea orodha ya vyakla vinavyoaminika kuongeza nguvu za kiume.

Soma Zaidi...
Kuwepo kwa mabonge ya damu wakati wa hedhi

Posti hii inahusu zaidi kuwepo kwa mabonge ya damu wakati wa hedhi, tunajua kabisa wakati wa hedhi damu inapaswa kuwa nyepesi na ya kawaida ila kuna wakati mwingine inakuwa na mabonge zifuatazo ni sababu za kuwepo kwa mabonge ya damu wakati wa hedhi.

Soma Zaidi...
Ni ili sababu ya kutokea kwa tezi dume

Tezidume ni moja ya magonjwa hayari yanayotokea katika mwili wa mwanaume.Hapa nimekuandalia sababu za kutokea kwa tezi dume.

Soma Zaidi...