/p>

RANGI ZA MAJIMAJI YANAYOTOKA KWENYE UKE NA MAANA YAKE KIAFYA


Majimaji yanayotoka kwenye uke ikiwemo damu ya hedhi kitaalamu yanajulikana kama vaginal discharge yanaweza kuwa na rangi mbalimbali unaweza pia kujiuliza lamda utakuwa unaumwa, kwani muda mwingine unaweza kuona yanatoka yakiwa na rangi ya tofauti kabisa. Kama ulivyo mkojo hubadili rang halikadhalika hata majimaji yanayotoka ukeni huweza kubadili. Makala hii itakwenda kukueleza maana za kiafya kutokana na rangi za majimaji haya:-


Majimaji haya yana umuhimu mkubwa sana katika kulinda afya ya mwanamke na ujauzito. Miongoni mwa kazi zake ni:-
1.kuondoa uchafu mwilini mwa mwanamke
2.Kuondoa seli zilizokufa mwilini
3.Kulinda mimba dhidi ya bakteria, fangasi na virusi
4.Kulinda mwili wa mwanamke dhidi ya vimelea vya maradhi visiingie kwenye mfumo wa kizazi kwa kupitia ukeni
5.Kuweka mfumo wa kizazi katika usalama na ubora wake.


Kiasi cha majimaji yanayotoka ukei huweza kutofautiana kwa rangi kulingana na siku katika mzunguruko wake wa hedhi. Kwa mfano:-


1.siku ya 1 - 5 hapa ni mwanzo wa hedhi, kwa mwanake aliye katika umri wa kupata hedhi majimaji yanayotoka kwenye uke wake yatakuwa ni mekundu ama yenye damu.
2.Siku ya 6 - 14 hii ni baada ya kukata kwa hedhi, hapa mwanamke hataona majimaji mengi kwenye uke kwake. Ila kadiri siku zinavyoenda yataanza kubadilika na kuwa kama mawingu ama rangi nyeupe pia yanaweza kuwa na rangi ya nnjano na kunatanata.
3.Siku ya 14 - 25 hapa yai linakuwa limesha toka, hivyo majimaji yanaanza kuwa na utelezi mwingi na kufanana na yale majimai meupe ya yai baada ya kulivunja. Na baada yamuda yanarudi kuwa na mawingu, meupe ama njano.
4.Siku ya 25 - 28 majimaji haya ytakuwa mepesi sana na ni machache sana.


Ok tumeshaona mabadiliko hayo ya majimaji yanavyobadilika kulingana na siku. Sasa hebu tuone babadiliko haya ra angi yanatuambia nini kiafya:-


1.rangi nyekundu:-
Hii ni damu ya hedhi, mara nyingi damu hii inakuwa ni anga’vu na yenye kufanana na rangi ya kutu. Hii ni kawaida kwa wanawake wote hivyo inaashiria afya ya kawaida. Na endapo itatoka kwa siku nyingi zaidi ya wiki, kiafya haionyeshi usalama. Ni vyema kumuona daktari aliye karibu nawe.


2.rangi nyeupe
Majimaji meupe yaaweza kuwa na rangi kama ya cream ama njano iliyo pauka. Kama mwanamke hana dalili zozote basi rangi hii inaonyeka mwanamke huyo yupo katika afya njema.


Hata hivyo ikiwa majimaji haya ni meupe na yameshikamana kama maziwa ya mgando au yakiwa yana harufu kali inaweza kuashiria kuna maambukizi ya vimelea vya maradhi kama fangasi na bakteria.


Ila kwa mara nyingi majimaji meupe yakiwa mazito, yana harufu kali hali hii inahusiana na maambukizi ya fangasi. Hali hii inaweza kusababisha miwasho.


3.Rangi ya ngajo na kijani
Kama majmaji haya yana rangi ya njano huenda hakuna tatizo ila yakiwa ni njano iliyowiva ama njano iliyona ukijani ama majimaji haya yakiwa ni ya kijani hii huashiria maambukizi ya bakteria ama magonjwa ya zinaa, fika kituo cha afya kama yatakuwa yanatoa harufu mbaya.


4.rangi ya kahawiya
Majimaji ya rangi hii yanakuwa na damu kwa mbali. Hali hii ni kawaida kama itatokea siku chache kabla ya kuingia hedhi. Pia inaweza kuashiria mimba changa. Na majimaji haya yatakuwa yanatokea baada ya kukutana kimwili, hii inaashiria kuwa kuna michubuko imetokea kwenye uke na kusababisha mipasuko midogo iliyokuwa ikivija damu..


5.majimaji yaliyo safi.
Katika hali ya kawaida majimaji yanayotoka ukeni yana kuwa ni safi na yenye weupe na yenye kuteleza kama vile majimaji meupe yanayotoka baada ya kupasua yai.


6.rangi ya kijivu
Majimaji ya rangi ya ijivu sio ya kawaida hivyo yanaashiria kuwa kuna sida katika afya ya mwanamke na mara nyingi ji maambukizi ya bakteria wanotambulika kama bacterial vaginosis. Dalil nyingine za baktera hawa bi:-
1.Maumivu
2.Miwasho
3.Harufu mbaya
4.Kuwa na wekundu kuzunguka mashavu ya uke na kwenye mlango wa uke.