Enyi mlioamini!
Enyi mlioamini! Msiingie nyumba ambazo si nyumba zenu mpaka muombe ruhusa, (mpige hodi) na muwatolee salamu waliomo humo. Hayo ni bora kwenu; huenda mtakumbuka (mkaona ni mazuri haya mnayoambiwa).
Na kama hamtamkuta humo yeyote, basi msiingie mpaka mruhusiwe . na mkiambiwa "Rudini," basi rudini; hili ni takaso kwenu. Na Mwenyezi Mungu Anajua mnayoyaatenda. Si vibaya kwenu kuingia majumba yasiyokaliwa, (yasiyofanywa maskani: kama mahoteli, maktaba), ( bila kupiga hodi), ambamo humo mna manufaa yenu; na Mwenyezi Mungu Anajua mnayoyadhihirisha na mna yoyaficha. (24:27-29)
Kutokana na aya hizi tunajifunza adabu za kuingia katika nyumba za watu kama ifuatavyo:
(i)Hairuhusiwi mtu kuingia nyumba ya mtu bila ya kubisha hodi. Hata kama utaukuta mlango uko wazi, huruhusiwi kuangaza macho ndani. Hivyo wakati wa kubisha hodi unatakiwa uwe pembeni mwa mlango, kiasi kwamba hata kama mlango umefunguliwa usiweze kumuona mtu au vitu vilivyomo ndani. Vile vile hairuhusiwi kubisha hodi kupitia mlango wa uani au madirishani. Hekima ya amri hii ya kubisha hodi, ni kulinda haki ya faragha (privacy) ambayo ni haki ya msingi kwa binaadamu katika mambo mema.
(ii)Hata baada ya kuruhusiwa kuingia katika nyumba za watu,hatutaingia mpaka kwanza tuwatolee salamu waliomo ndani.
(iii)Kama mtu atabisha hodi mara tatu bila ya kuitikiwa, hata kama atakuwa anawasikia watu wakiongea ndani, asiingie bali aondoke aende zake bila kinyongo.
(iv)Iwapo mtu ataitikiwa baada ya kubisha hodi na badala ya kukaribishwa ndani akaambiwa arudi, hanabudi kurudi kwa moyo mkunjufu bila ya manung'uniko yoyote.
(v)Hatuhitajiki kubisha hodi kwenye nyumba zenye kutoa huduma za kijamii kama vile hoteli, maktaba, msikiti, n.k.
Umeionaje Makala hii.. ?
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu mtazamo wa uislamu juu ya dini (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi..."Hakika wanaoamini kweli ni wale ambao anapotajwa Allah nyoyo zao hujaa khofu; na wanaposomewa aya zake huwazidishia imani na wanamtegemea Mola wao tu basi.
Soma Zaidi...Ni zipo njia wanazotumia Allah katika kuwasiliana na kuwafundisha wanadamu? (EDK form 1: Dhana ya elimu katika Uislamu).
Soma Zaidi...(i) Kutiishiwa Upepo Qur'an inatufahamisha kuwa Nabii Sulaiman alitiishiwa upepo akaweza kuutumia apendavyo kwa amri yake.
Soma Zaidi...Katika kipengele hich tutajifunza dhana ya ibada katika uislamu,maana ua ibada
Soma Zaidi...Mtu hawi Muumini wa kweli mpaka awe na yakini juu ya Mitume wa Allah (s.
Soma Zaidi...