Menu



Vyakula hatari kwa mjamzito hasa mimba changa

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu vyakula vya hatari kwa mjamzito hasa mimba changa

VYAKULA HATARI KWA MJAMZITO HASA KWA MIMBA CHANGA

1.Mayai mabichi: Mayai ni chakula kizuri kila mtu anatambuwa hili. Hata hivyo si jambo jema kula mayai mabichi. Hii inaweza kuwa hatari kwa ujauzito hasa kwa mwenye ujauzito mchanga. Hivyo epuka kula mayai mabichi ama yasiyowiva vyema.

 

2.Maini ya wanyama kwa wingi: Maini ni katika vyakula ambavyo vina virutubisho vingi sana. Kama ijulikanavyo ini lina kazi nyingi mojawapo ni kuondoa sumu mwilini. Hivyo unahitajika kutokula maini kwa mjamzito.

 

3.Shubiri: shubiri hufahamika kwa uchungu wake. kwa mwenye ujauzito hasa mimba changa shubiri sio salama. Shubirilinaweza kutoa ujauzito kama litatumika kwa kulinywa. Onyo hili linaandamana na miti mingine michungu.

 

4.Viazi mbatata vilivyoanza kuota: onyo hili ni kwa nafaka zote zinazoanza kuota sio nzuri kula. Hasa hasa viazi mbatata ambavyo vimeanza kutoa miche sio salama kwa mwanamke mjamzito kutuia kama chakula.

 

5.Mapapai hasahasa mapapai yasiyowiva: Matunda nimuhmu sana kwa mjamzito kwa afya yake na ya mtoto wake. Hata hivyo kuna matunda sio mazuri kuyala kwa wingi kwa mwenye mimba changa. Mapapai ni mojawapo, hasa papai ambalo halikuwiva, yaani lile la kijani lililokomaa.

 

6.Mananasi: nanasi ni kama papai, kama mjamzito atatumia kwa wingi, inaweza kuwa hatari kwa mimba iliyochanga.

 

7.Vyakula ambavyo havijawiva vyema hususani samaki na nyama: sio samaki tu na nyama, chakula chochote ambacho hakikuwiva vyema ni hatari sana kwa mwenye uauzito. Hii ni sawa na nyama ya kuku na vyakula vingine.

 

8.Kutumia majani ya chai yenye caffein kwa wingi. Mjamzito hakatazwi kunywa chai ya majani ya chai. Kilichokibaya ni kuzidisha unywaji wa chai yenye majani ya chai kupitiliza. Majani ya chai yana kemikali inayoitwa caffein, hii ikiwa nyingi inakuwa hatari kwa ujauzito.

 

9.Chumvi kwa wingi10.Energy drink

Download app yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiw ana App yetu. Bofya liln hapo chini kuweza ku download

Download Now Bongoclass

           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu image Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Vyakula Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Views 8110


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉4 Kitau cha Fiqh     👉5 kitabu cha Simulizi     👉6 Simulizi za Hadithi Audio    

Post zifazofanana:-

Faida za kiafya za kula samaki
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula samaki Soma Zaidi...

Faida za kula bamia
Posti hii inazungumzia kuhusiana na Faida ambazo anaweza kupata mwanadamu Kama akila bamia Mara kwa mara. Bamia huliwa Kama tunda au Kama mboga pia na husaidia vitu vingi mwilini. Soma Zaidi...

Faida za kula parachichi
Somo hili litakwenda kukueleza na kukuelimisha kuhusu umuhimu wa kula parachichi kiafya Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula Zabibu
Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula Tango
Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula Nyanya
Soma Zaidi...

VYAKULA VYA PROTINI, FATI NA MAFUTA
Je! unatambuwa madhara ya vyakula vya protini na mafuta? ungana nasi kwenye somo hili Soma Zaidi...

Je miwa ina madhara yoyote?
Umetaja faida za matunda , mimi ninataka kujuwa Je miwa ina madhara yoyote? Soma Zaidi...

Faida za kula Ndizi
Kuna faida kubwa za kiafya kwa kula ndizi, soma makala hii mpaka mwisho Soma Zaidi...

Fahamu vitamini K na kazi zake, vyakula vya vitamini k na athari za upungufu wake
kuhusu vitamini K, wapi tutavipata, ni zipi athari zake na ni zipi kazi zake mwilini. Soma Zaidi...