image

Namna ambavyo mwili unapambana na maradhi

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu namna ambavyo mwili unapambana na maradhi

NAMNA AMBAVYO MWILI HUPAMBANA NA MARADHI

Tumeona huko juu kuhusu visababishi vya maradhi na namna ambavyo maradhi yanaweza kusambaa, sasa hapa tutaona namna ambavyo miili yetu unapambana na maradhi haya kwa ajili yetu. Mwili una njia nyingi tuu na namna ya kupambana na maradhi kama utakavyoona hapo chini

 

1.KA KUTUMIA KUTA ZUIZI (PHYSICAL BARRIERS

Itambulike kuwa ili mtu aumwe ni kwamba wadudu wa maradhi wanatakiwa waingie mwilini. Sasa mwili una vizuizi yaani kuna ukuta maalum ambao unakazi ya kuzuoa wadudu hawa wasipate njia ya kuingia ndani. Vizuizi hivyo ni;-

 

A).Ngozi:ngozi yenyewe ni ukuta wa kuzuia vijidudu hivi. Ngozi hutumia chemikali kama jasho na mafuta ili kuuwa vijidudu hivi.ngozi inatabia ya kujitibu kwa haraka zaidi kama itapata jeraha ili kuzuia wadudu wasiingie.

 

B).Utando wa utelezi: huu ni utando maalumu ambao unateleza na kunata. Utando huu unapatika na sehemu nyingi za mwili kama puani kwa ajili ya kunasa mavumbi na vijidudu hawa. Utando huu pia upo machoni kwa ajili ya kunasa vijidudu hivi na kuvitoa nje.

 

C)Vinyweleo: hivi ni njia nyingine ya kunasa wadudu wowote wanaoraka kuingia ndani. Kwa mfano ndani ya pua kuwa vinyweleo hivi kwa ajili ya kunasa wadudu na mavumbi kuingia ndani.

 

D)Kemikali: kwa mfano mwili huzalisha asidi ya hydrocloric ambayo husaidia kuuwa bakteria waliopo kwenye vyakula.

 

2.INFLAMATORY RESPONSE (YAANI KUVIMBA)

Inatokea wadudu hawa wanaingia mwilini kwa mfano mtu anpojikata. Hivyo inflammatory response hali ya mwili kupambana na ma majeraha ambapo sehemu husika huvimba, huwa njeundu na kuwa na maumivu. Kitendo hiki hufanya eneo hili liwe limoto na kusababisha vimishipa vidogo vinavyoleta damu vilete damu kwa wingi na hatimaye seli kutoka kwenye damu hupambana na wadudu walofanikiwa kuingia kwenye eneo lile.

 

3.IMMUNE SYATEM (MFUMO WA KINGA)

Njia zilizotajwa hapo juu pekee haziwezi kupambana na wadudu hawa. Hivyo kuna mfumo maalumu wa kuukinga mwili dhidi ya majambazi hawa (pathojens) mfumo huu huitwa immune system ambao unatengenezwa na seli hai nyeupe za damu na aina flani ya protin ambayo kitaalamu huitwa antibodies ambazo zipo kwenye mfumo wa lymph (lymphatic system).

 

Mfumo wa lymph huu umezunguka mwili mzima na unahusika katika kubeba majimaji mwilini. Katika kufanya hivi unafanya kazi ya kuwatowa bakteria na pathogen wengine nje ya mwili. Mfumo huu una seli hai nyeupe nyingi nna hizi ndizo ambazo zinapambana na pathogen na kuwauwa.

 

Seli nyeupe za damu, kazi yao kuu seli hizi ni kuulinda mwili dhidi ya wavamizi. Kuna aina fani ya seli hizi hutowa kemikali ziitwazo antibodies ambazo huwakamata pathogens na pitowa tahadhari kwa seli nyingine ili wawaue hawa pathogens. Pindi unapoumwa hutokea tezi za lymph zinauma kama mtoki ni kwa sababu seli hizi nyeupe zipo kwa wingi eneo lile kupambana na wadudu hawa.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 674


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Huduma ya Kwanza kwa mwenye kizunguzungu
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu mwenye kizunguzungu Soma Zaidi...

Vyakula vya madini
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za vyakula vya madini mwilini Soma Zaidi...

huduma ya kwanza kwa mtu aliyeingiwa na uchafu sikioni
Post hii inahusu huduma ya kwanza kwa mtu aliyeingiwa na uchafu au kitu chochote sikioni. Sikio ni mojawapo ya milango ya fahamu ambapo hutumika kusikia, Kuna wakati vitu uingia ndani yake na kuleta madhara Soma Zaidi...

HUDUMA YA KWANZ AKWA ALIYEPALIWA AMA KUSAKAMWA NA KUTU KOONI
Soma Zaidi...

Ambao hawapaswi kupata chanjo
Posti hii inahusu zaidi watu ambao hawapaswi kupewa chanjo, hawa ni wale ambao wana hali tofauti na ikitokea wakapata chanjo wanaweza kupata madhara badala ya kuwasaidia. Soma Zaidi...

Zijue hasara za magonjwa ya ngono
Posti hii inahusu zaidi hasara za magonjwa ya ngono, ni magonjwa yanayoambukizwa kwa kujamiiana bila kutumia kinga. Soma Zaidi...

Jinsi ya kutoa huduma ya kwanza kulingana na tatizo
Posti hii inahusu sana mambo ya huduma ya kwanza ambayo huduma ya kwanza inapatikana au inatolewa na mtu yeyote katika jamii . Soma Zaidi...

Huduma ya kwanza kwa mtu aliyeng,area na wadudu
Posti hii inahusu zaidi huduma ya kwanza kwa mtu aliyengatwa na wadudu. Wadudu ni viumbe vidogo ambavyo hukaa sehemu mbalimbali kama vile kwenye miti na sehemu kama hizo Soma Zaidi...

Nyanja sita za afya
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu nyanja sita za afya Soma Zaidi...

Vipi kuhusu kibofu kukaza sana na unapokula unahisi kama tumbo kujaa zaidi je hii nidall yamimba?
Dalili za mimba zinaweza kuwa tata sana kuzijua mpaka upate vipimo. Kwa mfano unaweza kupatwa na maumivu yakibofu. Je unadhani nayo ni dalili ya mimba? Soma Zaidi...

Umuhimu wa asidi iliyokwenye tumbo( kwa kitaalamu huitwa HCL)
Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa asidi iliyo kwenye tumbo kwa kitaalamu huitwa HCL, ni asidi inayofanya kazi nyingi hasa wakati wa kumengenya chakula. Soma Zaidi...

Aina za vidonda
Posti hii inahusu zaidi Aina mbalimbali za vidonda kwenye mwili wa binadamu, ni vidonda ambavyo utokea kwenye mwili wa binadamu kwa Aina tofauti. Soma Zaidi...