HUDUMA YA KWANZ AKWA ALIYEPALIWA AMA KUSAKAMWA NA KUTU KOONI
Mtu aliyepaliwa ama kukwamwa na kitu kooni huwa anashindwa kuzungumza ama kupumua. Hali hii ikiendelea kwa muda inaweza kumsababishi amadhara makubwa hata kifo. Ubongo unaweza kufa ndani ya dakika chache sana kama ukikosa hewa ya oksijeni. Kama ukimkuta mtu amepaliwa ama kukamwa na kitu kooni na anashindwa kupumua unatakiwa umpe huduma ya kwanza:
Mtu anaweza kukwamwa ama kupaliwa na chakula, ama kitu kigumu kama kumeza pesa, jiwe barafu na kadhalika. Pia anaweza kupaliwa na maji, asali ama kimiminika chochote na kuzuia njia ya hewa. Hivyo kuathiri mfumo wa upumuaji.
Kama kupaliwa ni kwa kawaida amnapo mtu atakuwa na uwezo wa kukohoa, kulia, kuzungumza na kuhema, tambua kuwa anaweza kurudi katika hali ya kawaida hata bila ya kupata huduma ya kwanza. Ili kumsaidia mtu huyu kurudi haraka katika hali ya kawaida
1.Mwambie aendelee kuhohoa zaidi hii itasaidia kuondoa kilichokwama
2.Mwambe ajaribu kutema kicho kilichomkaba ama kilicho mkwama ama kusababisha kupaliwa
3.Katu usuthubutu kuingiza vidole vyeko kwenye koo lake eti kujaribu kukitoa kilicho mkaba
Kupaliwa kwa namna nyingine iliyo mbaya ni pale mtu anaposhindwa kusema, kukohoa, kulia ama kuhema. Bila ya huduma ya kwanza mtu huyu anaweza kuzimia na hatimaye kupoteza maisha. Huduma ya kwanza kwa mtu huyu ni:-
1.Muinamiche kifua chake kwa mbele, hii itasaidia kitu kilichomkaba kisiende ndani sana
2.Simama nyuma yake pembeni kidogo, weka mkono wako mmoja kwenye kifua chake na mgono wako mwingine anza kumpiga ngumi kwenye mgongo wake kati ya bega na bega, usawa na kifua kwa nyuma.
3.Angalia kama kilichomkaba kimeondoka
4.Kama hakijaondoka mpige tena kwa nguvu mapigo matano kama ni mtoto mminye kwa nguvu kwenye tumbo lake fanya hivi mara tano. Usifanye hivi kwa mtoto mdogo.
5.Kama hali inaendelea umpeleke kituo cha afya cha karibu.
Umeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi malengo ya kutibu ukoma, ni malengo ambayo yamewekwa na wizara ya afya ili kuweza kutokomeza ukoma kwenye jamii
Soma Zaidi...Posti hii inahusu njia mbalimbali ambazo utumika kupitisha chanjo, njia hizo utegemea na kazi ya chanjo kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa aliyeungua
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi sehemu ambazo zinapaswa kudungwa chanjo, hizi ni sehemu zile zilizopendekezwa kwa ajili ya kuchoma chanjo kwa kadiri ya kazi ya chanjo.
Soma Zaidi...Posti hii inaelezea kuhusiana na mbinu za kutoa huduma ya kwanza kwa walio na majeraha ya macho kutokana na aina mbalimbali ya jeraha
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu aliyekazwa na misuli
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mgawanyo wa matibabu ya kifua kikuu, tunajua kubwa kifua kikuu ni Ugonjwa ambao utumia mda mrefu kidogo katika matibabu kwa hiyo mgawanyiko wake uko kwenye sehemu mbili muhimu kama tutajavyoona
Soma Zaidi...Kwikwi sio hatari sana kwa afya, lakini inaweza kuwa hatari zaidi kwa mu aliyefanyiwa upasuaji kwenye tumbo.
Soma Zaidi...Hapa utajifunza kuusu vitamini D, kazi zake, upungufu wake na chanzo cha kupata vitamini D.
Soma Zaidi...