Faida za kula Faida za kula buluu beri
4.
4.Buluu beri (blueberry)
Ni katika matunda yanayotambulika kuwa na virutubisho vingi mwilini.. Tunda hili hutambulika kuwa na vitamini c kwa wingi, vitamini K na madini ya manganese. Pia tunda hili lina kambakamba yaani fiber. Itambulike kuwa vitamini C ni katika vitamini vinavyofanya kazi kubwa sana kulinda afya na kuupa mwili uwezo wa kupambana na maradhi kuliko aina nyinginezo za vitamini.
Pia tunda hili lina antoxidant kwa wingi. Hii husaidia katika kupambana na maradhi ndani ya mwili. Antoxidant huzuia mwili usipatwe na maradhi hatari shambulizi kama shambulizi la moyo, kisukari na mengineyo.
Tunda hili pia husaidia katika kufanya madhubuti mfumo wa kinga wa mwili yaani immune system. Wataalamu wamegundua kuwa tunda hili husaidia katika kuuwa seli yaani natural killer cell hali hii husaidia mwili katika kupambana na athari za stress yaani msongo wa mawazo pamoja na mashambulizi ya virusi yaani viral infections.
Pia tafiti za kisayansi zimeonesha kuwa tunda hili husaidia katika kuimarisha afya ya ubongo na utunzaji wa kumbukumbu. Husaidia tatizo la kupoteza kumbukumbu hasa kwa wazee. Tunda hili ni katika orodha ya matunda ambayo yanajulikana kwa uwezo wake wa kusaidia katika kutunza kumbukumbu na kuondoa tatizo la kusahausahau.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Dua za Mitume na Manabii 👉2 Simulizi za Hadithi Audio 👉3 web hosting 👉4 Madrasa kiganjani 👉5 Kitabu cha Afya 👉6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina
Post zinazofanana:
Vyakula vinavyosaidia kupunguza uzito
Posti hii inahusu vyakula ambavyo vinasaidia kupunguza uzito, ni baadhi ya vyakula ambavyo unaweza kutumia ili kuweza kuweka kwenye hali ya kawaida.
Soma Zaidi...Namna ya kuandaa mdalasini kwa ajili ya tiba.
Posti hii inahusu namna au njia za kuandaa mdalasini kwa ajili ya tiba ya homoni imbalance kwa wanawake.
Soma Zaidi...Faida za kula Pilipili
Usiogope kuwashwa, kula pilipili ni nzuri kwa afya yako ia virutubisho vingi sana
Soma Zaidi...Vyakula murajabu kea mwenye presha ya kushuka
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu vyakula murajabu kea mwenye presha ya kushuka
Soma Zaidi...Faida za kiafya za kula mihogo
Some Hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula mihogo
Soma Zaidi...