Faida za kula Palachichi

Palachichi lina virutubisho vingi na vitamini, kula palachichi uiokoe afya yako

Faida za kula Palachichi

3.Palachichi (avocado)

Hili ni katika matunda yenye fat (mafuta). Itambulike kuwa si kila mafuta ni hatari ndani ya miili yetu. Tunahitaji vyakula vya fat yaani mafuta kwa ajili ya kutupatia joto kwenye miili yetu. Pia fati husaidia kuipa miili yetu nguvu. Katika tunda hili palachichi mafuta yake ni aina ya oleic acid yaani yapo katika aina flani ya asidi ambayo husaidia katika kupunguza uvimbe mwilini na kusaidia kuboresha afya ya moyo.

Palachici pia hutambulika kitaalamu kuwa lina lina madini ya potassium na magnesium kwa wingi sana. Pia ni katika vyakula vyenye kambakamba yaani fiber. Vyakula hivi vyenye fiber husaidia katika kuweka usalama wa tumbo yaani kuhakikisha chakula kinatembea ipasavyo ndani ya tumbo kutoka sehemu moja mpaka sehemu nyingine mpaka kufika kwenye njia ya haja kubwa.

Pia tunda hili husaidia kupungusa hatari za kupata maradhi ya stroke yaani kupalalaizi kutokana na kiwango kikubwa cha madini ya magnessium ambayo husaidia katika kupunguza shinikizo kubwa la damu. Hivyo palachichi husaidia katika kudhibiti afya ya moyo. Palachichi moja linaweza kutoa 28% ya mahitaji ya mwili ya madini haya.


                   



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 245


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-