Sera ya uchumi katika Uislamu
4.
4. Sera ya uchumi katika Uislamu
Kwanza, katika Uislamu utekelezaji wa mambo yote hutegemea zaidi ucha-Mungu wa mtu binafsi na kuogopa kwake kusimamishwa mbele ya Allah na kuhisabiwa, kuliko usimamizi wa vyombo vya dola kama sheria, mahakama, na askari polisi. Hii ni kwa sababu hisabu siku ya kiyama itakuwa kwa kila mtu binafsi. Hapana shaka vyombo vya dola vipo katika Uislamu na vinafanya kazi lakini msisitizo wa utekelezaji wa mambo yote upo katika uadilifu na taqwa kuliko katika kuogopa polisi na ma ha k ama.
Pili, uhuru wa watu binafsi kufanya wanalolitaka ndio sera inayofuatwa katika Uislamu. Yaani katika masuala ya uchumi Uislamu umempa uhuru kila mtu afanye lile analoliona linafaa. Na serikali ya Kiislamu haitaingilia uhuru wake huo isipokuwa tu pale ambapo haki haitatendeka iwapo uhuru huo hautaingiliwa. Mtume (s.a.w) amelielezea kwa ufasaha sana suala hili pale alipoyapigia mfano maisha ya watu katika jam ii na wasafiri waliomo chomboni baharini:
βHebu tuchukue mfano wa meli inayosafiri baharini ikiwa imejaza abiria ambao wamekaa katika sehemu zote za chini na juu. Sasa iwapo abiria mmoja aliyekaa katika sakafu hiyo ataamua kujipatia maji kirahisi kwa kutoboa pale alipoketi na iwapo abiria wengine watamzuia kufanya hivyo (na ni wajibu wa abiria wote walio juu na chini kumzuia) watamnusuru yeye na wao wenyewe na kufa maji. Iwapo watamwacha atoboe basi watazama wote waliochini na juu ya meli.β (Bukhari).
Mfano huu unatuonesha kuwa japo Uislamu unampa kila mtu uhuru wa kufanya alitakalo lakini uhuru huo una mipaka. Iwapo mtu atafanya jambo lisilo la haki basi serikali ya Kiislamu lazima iingilie kati kwa maslahi ya jamii nzima.
Tatu, wajibu mkubwa wa serikali ya Kiislamu ni kusimamia haki na kuzuia dhulma katika maisha ya jamii.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
π1 Dua za Mitume na Manabii π2 Bongolite - Game zone - Play free game π3 Kitabu cha Afya π4 web hosting π5 Kitau cha Fiqh π6 kitabu cha Simulizi
Post zinazofanana:
Mtazamo wa uislamu juu ya ndoa ya mke zaidi ya mmoja
Je jamii inachukuliaje swala la kuoa mke zaidi ya mmoja.
Soma Zaidi...Njia za kuzuia na kupunguza zinaa katika jamii
(ii) Hatua za Kuzuia Uzinzi JamiiUislamu pamoja na kutoa mafunzo ya maadii yanayomuwezesha mtu binafsi ajiepushe kwa hiari yake na kitendo kibaya cha zinaa, umechukua hatua mbali mbali ambazo huifanya zinaa isiwe kitendo chepesi katika jamii.
Soma Zaidi...