.Mazingatio muhimu katika uchumi wa Kiislamu

3.

.Mazingatio muhimu katika uchumi wa Kiislamu

3.Mazingatio muhimu katika uchumi wa Kiislamu Kanuni kuu za uchumi katika Uislamu ni:



(i)Kumwamini Allah kuwa ndiye Muumba na mfalme wa ulimwengu huu yaani kumtii Allah katika mambo yote.



(ii)Binaadamu ni Khalifa wa Allah hapa duniani, hivyo wajibu wake ni kusimamisha amri ya Allah.



(iii)Ili kumsaidia mwanaadamu kutimiza wajibu wake kama Khalifa, Allah amemdhalilishia kila kitu katika ulimwengu huu:


'Mw enyezi Mungu ndiye aliyekutiishieni bahari ili humo zipite merikebu kwa amri yake ili mtafute fadhila yake na mpate kushukuru '. (45:12).


'Je, Hukuona kwamba Mwenyezi Mungu amevitiisha kwa ajili yenu vilivyomo ardhini' (22:65)


'Je, Hukuona kwamba Mwenyezi Mungu amekutiishieni vilivyomo mbinguni na ardhini na anakukamilishieni neema zake zilizo dhahiri na za siri? ' (31:20).



'Yeye ndiye aliyefanya ardhi iweze kutumika kwa ajili yenu. Basi nendeni katika pande zake zote na kuleni katika rizki zake na kwake ndiyo marejeo.' (67:15).
Hivyo kuzitumia neema hizo za Allah si dhambi bali ni katika kushukuru.



(iv)Kutokana na wajibu wa Ukhalifa wa Allah, mwanaadamu ataulizwa kwa neema alizompatia na atahesabiwa kwazo, ikiwa ni pamoja na namna alivyochuma na kutumia mali.



(v) Kuwa na mali au kutokuwa na mali nyingi au kidogo si dalili ya ubora au udhalili wa mtu. Hali zote mbili ni mtihani. Anachotazama Allah ni nyoyo za watu. Misingi au kanuni hizo zikithibiti katika moyo wa mtu zinakuwa na athari kubwa sana katika shughuli za kiuchumi za Muislamu.



Kanuni ya kwanza kwa mfano humfanya mtu afuate maamrisho ya Allah na hivyo atafanya kila njia ajiepushe na makatazo yake.



Pili, kwa kujua kuwa yeye ni Khalifa tu atajua yeye si mmilikaji wa hakika, hivyo atafuata maagizo ya huyo aliyempa ukhalifa yaani Allah.



Tatu, atajua kuwa utajiri si kitu cha kukipigania, bali mtu apiganie maisha bora na afya katika kutafuta radhi za Allah (s.w).



Nne, kwa kujua kuwa atahesabiwa na Allah anayeshuhudia kila kitu ataendesha shughuli zake za kiuchumi kwa kumcha Allah.




                   




Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 135


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

nmna ya kufanya Talbiy kwa mwenye kuhiji
2. Soma Zaidi...

DUA 94 - 114
DUA ZA KUONDOA WASIWASI, SIHIRI NA UCHAWI 94. Soma Zaidi...

Hadithi inayokataza bidaa (bid's) uzushi katika dini
' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ': ': ' ' ' ' ' ' ' "... Soma Zaidi...

NAMNA YA KUSWALI
13. Soma Zaidi...

Hadithi Ya 21: Sema Namuamini Allah Kisha Kuwa Mwenye Msimamo
Soma Zaidi...

hatma
Soma Zaidi...

ndoto
Soma Zaidi...

tarekh 3
KUCHIMBWA UPYA KISIMA CHA ZAMZAMKwa kifupi ni kuwa Abdul-Muttalib alipata agizo kutoka ndotoni kuwa achimbe kisima cha zamzam, na akaelekezwa sehemu ya kupachimba. Soma Zaidi...

Haki na wajibu kwa mayatima
Soma Zaidi...

Masomo ya Dua na Faida zake Dua
Soma Dua mbalimbali hapa, Soma Zaidi...

fadhila za sura kwenye quran
FADHILA ZA BAADHI YA SURA Umuhimu na ubora wa baadhi ya sura na aya. Soma Zaidi...

Mambo ya kuzingatia kabla ya kugawanya urithi
Soma Zaidi...