Haki ya Serikali kuzuia Dhulma
Haki ya Serikali kuzuia Dhulma
Kwanza, serikali ya Kiislamu inao wajibu wa kuandaa mazingira mazuri ya kihuduma na kimawasiliano kuwawezesha raia kujiletea maendeleo na inao wajibu wa kuingilia kati ili kusimamia haki na kuzuia dhulma. Ni wakati gani kwa mfano ambapo serikali inaweza kuingilia kati. Allah ndiye aliyeziumba rasilimali zilizopo duniani na hivyo ni wajibu wa binaadamu kuzitumia rasilimali hizo kwa manufaa ya watu na kwa ufanisi. Hivyo serikali yaweza kuingilia kati iwapo rasilimali hizo zitatumiwa kuwadhulumu watu au hazitatumika kwa ufanisi.
Pili, baadhi ya kazi ni haramu katika Uislamu kwa sababu zimefungamana na mambo ya haramu, kama vile kamari, umalaya, uchawi, ulevi n.k. Ni wajibu wa serikali kuona kuwa mambo hayo hayapewi nafasi katika jamii.
Tatu, ni wajibu wa serikali pia kutoa fursa sawa kwa watu wote ya kuendeleza na kuvikuza vipaji vyao kwa kuwapa fursa sawa za elimu na mafunzo. Ni wajibu wa serikali kugharamia elimu kwa ajili ya manufaa ya watu wote. Elimu ni haki ya msingi kwa wanadamu wote.
Nne, ni wajibu pia wa serikali kuhakikisha kuwa hata katika zile kazi za halali kisheria zinafanywa kwa uadilifu pasi na dhulma yoyote. Yaani Serikali ihakikishe mathalani kuwa bidhaa zinazotolewa zimefikia ubora kwa wanaoizalisha, kuona kuwa uadilifu wa kitaalamu unadumishwa, kuona kuwa Wafanyakazi wanalipwa mishahara kwa haki.
Hata hivyo, Uislamu hauelemei upande mmoja tu wa kumtetea mfanyakazi peke yake wala kumtetea mwajiri peke yake. Wafanyakazi pia wakileta madai yasiyo ya haki ni juu ya serikali kuingilia kati.
Tano, ni wajibu wa serikali pia kuzuia mambo yanayoweza kudhuru watu, kwa mfano kama mtu akijenga kiwanda cha hatari katika makazi wanamoishi watu. Au hata mambo yanayoweza kuwatesa wanyama, kama kuwabebesha mizigo mizito sana hadi wanaanguka na kuvunjika miguu au kufa, au kuwafanyisha kazi kwa mateso makubwa na kutowapa chakula cha kutosha. Hali kadhalika serikali inaweza kwa mfano kuzuia magari au meli iliyopakia abiria au mizigo kuliko uwezo wake.
Sita, katika suala la usambazaji wa bidhaa, serikali inaweza kuingilia kati iwapo watu watahodhi vyakula na bidhaa nyingine muhimu kwa lengo la kupandisha bei.
Saba, ni wajibu wa serikali kujenga miundo mbinu (in-frastructures) na kuidhibiti, kwa mfano kujenga barabara, madaraja, reli, kusambaza maji ya bomba, kujenga mitambo ya umeme, simu n.k.
Wakati wa Ukhalifa wake, Ali (r.a) alimwambia Nahri, ambaye alikuwa mkuu wa jimbo la Misri; βUsifanye ukusanyaji wa kodi ya ardhi kuwa ndiyo kazi yako kubwa; kazi yako kubwa ni kuindeleza ardhi hiyo.β
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
π1 web hosting π2 ai web app π3 Kitau cha Fiqh π4 Tafasiri ya Riyadh Swalihina π5 Madrasa kiganjani π6 Dua za Mitume na Manabii
Post zinazofanana:
Warithi wasio na mafungu maalumu katika uislamu
Hapa utajifunza watu wanaorithi bila ya kuwekewa mafungu maalumu au viwango maalumi vya kurithi.
Soma Zaidi...Nini maana ya ndoa katia uislamu na ni upi umuhimu wake
Hapa utajifunza maana ya ndoa kulingana na uislamu na umuhimu wake katika jamiii
Soma Zaidi...msimamo wa uislamu juu ya kupanga uzazi na uzazi wa mpango
Msimamo wa Uislamu juu ya kudhibiti uzaziKama tulivyoona, msukumo wa kampeni ya kudhibiti kizazi, umetokana na mfumo mbaya wa kijamii na kiuchumi ulioundwa na wanadamu kutokana na matashi yao ya ubinafsi.
Soma Zaidi...Mgawanyo wa mirathi kutoka kwenye Quran
Quran imegawanya mirathi katika haki. Mgawanyo huu ndio unaotakiwa utumike na si vinhinevyo.
Soma Zaidi...Maana ya mirathi katika uislamu
Post hii itakufundishabkuhusu mirathi ya kiislamu, maana yake.
Soma Zaidi...Namna ya kutawadha hatuwa kwa hatuwa.
Post hii inakwenda kukugundisha jinsi ya kutawadha hatuwa kwa hatuwa.
Soma Zaidi...