Zoezi hili linamaswali mbalimbali kuhusiana na swala na masharti ya swala.
Zoezi la 6.1
2.(a) Tofautisha kati ya ‘kuswali’ na ‘kusimamisha swala’
(b) Ni upi umuhimu wa kusimamisha swala katika Uislamu?
3.(a) Nini maana ya ‘twahara’ kilugha na kifiqih.
(b) Bainisha makundi ya maji yanayotumika kujitwaharishia.
(c) Orodhesha mambo yanayoweza kuharibu maji machache kutofaa kujitwaharishia.
4.(a) Toa maelezo mafupi juu ya
(i) maji safi (ii) udongo safi (iii) najisi (iv) hadathi
(b) Taja mgawanyo wa najisi na namna ya kujitwaharisha kwa kila aina ya najisi
5.Bainisha kati ya najisi kubwa na najisi ndogo.
(b) (i) Eleza maana ya hadathi.
(ii) Bainisha mgawanyo wa hadathi na namna (jinsi) ya kujitwaharisha kwazo.
6.(a) Kwa kutumia ushahidi wa aya, orodhesha nguzo za udhu.
(b) Eleza maana ya
(i) Tayammamu (ii) Qibla
(c) Eleza hatua kwa hatua namna ya
(i) kutia udhu (ii) kutayammamu
(iii) kujitwaharisha kutokana na hadath kubwa (janaba).
7.(a) Bainisha mambo yanayotengua udhu.
(b) Taja nguzo na masharti za tayammamu
8.Ainisha mipaka ya sitara ya mwanamume na mwanamke kwa mujibu wa Qur’an na Sunnah.
9.(a) Taja nyakati zilizoharamishwa kuswali
(b) Tofautisha kati ya ‘adhana’ na ‘iqama’
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Kwa nini Lengo la Funga halifikiwi na Wafungaji Wengi?
Soma Zaidi...Ni muda gani unatakiwa ufunge ramadhani, je kuandama kwa mwezi kwa kiona ama hata kusiki.
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukufundisha maana ya neno talaka katika uislamu kisheria na kilugha.
Soma Zaidi...Ni ipi raslimali ya halali kuimiliki katika uislamu.
Soma Zaidi...Posti hii inakwenda kukufundisha kuhush swala za sunnah.
Soma Zaidi...