picha

Ijue timu ya upasuaji

Posti hii inahusu timu ya upasuaji hii ni timu ambayo inahusika katika chumba cha upasuaji, kwa sababu ya kutunza usafi na usalama chumba hiki kinapaswa juwa na timu ya watu wanne na walio na elimu kuhusu kazi hiyo.

Timu ya upasuaji.

1. Kwanza kabisa tunapaswa kujua kuwa upasuaji ni hali ya kurekebisha sehemu fulani kwenye mwili au kutoa kiungo chochote kwenye mwili au kusafisha kutokana na uchafu ulio kwenye mwili wa binadamu kwa hiyo kazi hii inahitaji usafi wa hali ya juu kabisa ili kuweza kuepuka Maambukizi kutoka kwenye mwili wa binadamu kwenda kwa mgonjwa kwa hiyo wafuatao ni wahudumu kwenye chumba cha upasuaji.

 

2. Mhudumu wa kwanza ni yule anayefanya usafi kwenye chumba cha upasuaji.

Huyu mhudumu sifa ya kwanza anapaswa kuwa ni  nesi aliyesajiliwa na kupata mafunzo kutokana na kazi hiyo kwa hiyo kazi yake ni kuhakikisha kuwa chumba kinakuwa kwenye hali ya usafi na hakuna vumbi yoyote ambayo inakuwepo kwenye chumba hicho na kuhakikisha kuwa kuna hewa inayopaswa kuwepo kwenye chumba hicho cha upasuaji.

 

3. Mhudumu mwingine ni msafisha vifaa vya upasuaji.

Tunajua wazi vifaa vinavyotumika kwenye upasuaji ni vifaa ambavyo utumika kwa mgonjwa mmoja na mwingine kwa hiyo mhudumu huyu anapaswa kuwa na elimu ya kutosha kuhusu kusafisha vyombo hivyo kwa hiyo kabla ya kufanya upasuaji anapaswa kuhakikisha kubwa vyombo vyote vipo na vinafanya kazi kwa hiyo vyombo hivyo visiposafishwa vizuri usababisha maambukizi kwa mgonjwa.

 

4. Mtoa huduma ya  usingizi.

Huyu ni mmojawapo ambaye anapaswa kutoa dawa ya usingizi kufuatana na mda ambao dawa inapoisha kwenye mwili wa mgonjwa kwa hiyo huyu ndiye anapaswa kuwaambia wafanya upasuaji kutumia mda ili upasuaji uishe kabla ya dawa kuisha kwenye mwili kwa hiyo huyu pia uhakikisha kuwa mgonjwa anapumua vizuri na mapigo ya moyo yako sawa na kuhakikisha kuwa  upasuaji unaenda vizuri.

 

5. Mfanya upasuaji au kwa jina lingine ni daktari.

Huyu ni mhusika mkuu wa upasuaji ambaye ndiye anakuwa ana utaalamu katika upasuaji kwa sababu anakuwa na ujuzi kwa hiyo wahudumu wengine wanapaswa kumsaidia sana kwa sababu ya shughuli kubwa aliyonayo kwa hiyo huyu anapaswa kuwa na ujuzi wa kutosha kabisa

 

 

 

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Jifunze Main: Post File: Download PDF Views 2033

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉4 Kitau cha Fiqh     👉5 Bongolite - Game zone - Play free game     👉6 Madrasa kiganjani    

Post zinazofanana:

Nguo zinazovaliwa kwenye chumba cha upasuaji na kazi zake

Posti hii inahusu zaidi nguo za kuvaliwa kwenye chumba cha upasuaji na kazi zake, hizi ni nguo ambazo wahudumu wa afya wanapaswa kuzivaa wakati wa upasuaji kwa ajili ya kuwakinga na Maambukizi kati ya wahudumu wa afya na wagonjwa pia

Soma Zaidi...
Kauli za wataalamu wa afya

Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu kauli mbalimbali za wataalamu wa afya

Soma Zaidi...
Faida za kiafya za kufunga kusayansi

Katika somo hili utakwenda kuzinuwa faida za kufunga kitaalamu. Hapa hatutaangalia mtazamo wa dini yeyote

Soma Zaidi...
dondoo 100 za Afya

Basi tambua haya;- 61.

Soma Zaidi...
Kitabu Cha Kitabu Cha matunda

Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet.

Soma Zaidi...