YANAYOATHIRI AFYA KATIKA VYAKULA

Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote

YANAYOATHIRI AFYA KATIKA VYAKULA

YANAYOATHIRI AFYA
Afya yamtu inaweza kuathiriwa kuwa njema au kuwa mbovu kwa kuzingatia mambo kadhaa wakadhaa. Hapa nimechagua mambo makuu matano ambayo nitakwenda kuyaangalia ambayo ni;-


A).vyakula
B)Mazingira
C)Shughuli za kila siku
D)Tabia na mazoea
E)Vizazi, familia ama kurithi.


1.VYAKULA
Vyakula ni katika sababu kubwa ambazo husaidia kwa kiwango kikubwa kuathiri afya za watu. Wataalamu wa afya leo wanaeleza na kutaja magonjwa mengi sana ambayoyo yanapatikana kwa kupitia vyakula. Pia yapo magonjwa ambayo huambukizwa kwa kupitia ulaji wa chakula. Hivyo magonjwa mengi na hatari zaidi yamekuwa na mahusiano na vyakula vyetu. Chakula kinaweza kuwa msaada kwako au kuwa ni chanzo cha matatizo ya afya yako. Mfano mzuri ni kuwa leo wataalamu wa afya anaeleza kuwa mamilioni ya watu wanakufa kwa ugonjwa wa saratani kila mwaka. Tafiti zinaonesha kuwa miongoni mwa sababu za ugonjwa huu ni vyakula. Vyakula ambavyo tunavila leo sio rafiki kwa afya zetu. Tumekuwa tukila vyakula ambavyo vimejaa kemikali nyingi na matatizo kadha wakadha.

Mfano wa pili ni ugonjwa wa kisukari, huu ugonjwa umekuwa ukienea kwa kasi sana duniani leo. Kuanzia watoto, vijana wazee na wajawazito wote wapo hatarini kuapata maradhi haya. Wataalamu wa afya wanataja kuwa vyakula ni katika sababu mjawapo ya kupata maradhi haya. Kuongezeka kwa uzito nje ya uzito wa kawaidi ni katika sababu za kutokea kwa kisukari. Wataalamu wa afya wanaeleza kuwa vyakula ni sababu ya kuongezeka kwa uzito mwilini na kutofanya mazoezi ijapokuwa zipo sababu zingine.

Magonjwa ya moyo kama shinikizo la damu (presha) pamoja na shambulio la moyo (heart attack) ni katika magonjwa yanayowapata watu weng duniani na kusababisha vifo vingi sana. Wataalamu wa afya wanaeleza katika sababu kubwa za kutokea kwa maradhi haya ni vyakula. Hususan vyakula vyenye mchanganyiko mkubwa wa mafuta ya viwandani.

Maradhi ya utapiamlo kama matege, baadhi ya matatizo ya macho, unyafuzi na kwashiakoo pamoja na kudumaa ni katika maradhi ambayo husababishwa na vyakula. Majeraha kutokupona haraka, kuchelewa kupona kwa vidonda na makovu, ngozi kupasuka na kutokwa na vidonda kwenye mdomo ni katika baadhi ya matatizo yanayosababishwa na vyakula Kwa ufupi ni kuwa vyakula ni katika sababu kubwa sana ya maradhia mabayo tuanayapata. Tutazungumzia kwa undani zaidi somo hili kwenye kurasa zijazo na tutaona kwa undani vipi vyakula vinaweza kusababisha yote hayo.


                   Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 57


Download our Apps
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-