MZUNGURUKO WA DAMU

6.

MZUNGURUKO WA DAMU

6.SAFARI YA DAMU KWA KILA SIKU.

picDamu ni tishu iliyopo katika hali ya kimiminika. Bila ya damu mwanadamu hawezi kuishi. Moyo ndio kiungo kikuu wenye mwili chenye kazi ya kuisambaza damu mwili mzima. Ukubwa wa kiungo hichi hufanana na ngumi. Moyo husafirisha damu kwenye mishipa inayokadiriwa kuwa na urefu wa kilomita elfu tisini na saba (97) na hii hufanyika ndani ya sekunde 20 tu. pic

Damu imeundwa kwa seli hai nyekundu za damu, seli hai nyeupe za damu, plasma, maji na seli sahani. Kila moja kati ya hizi ina kazi yake maalumu. Katika makala hii fupi tutaona vitu hivi kwa ufupi tu. Pia itambulike kuwa kuna viumbe hawana damu kama minyoo na baadhi ya samaki. Na hii ni kutokana na jinsi maumbile yao yalivyo. Asilimia 7% ya mwili wa binadamu ni damu na mtu mzima ana damu kuanzia lita 3.7 mapaka lita 5.6.

Seli nyekunsu za damu (red blood cell), hizi kitaalamu huitwa erythrocytes na hutengenezwa kwenye uroto wa mifupa yaani bone marrow. Kwa wastani seli hizi zinaweza kuishi kwa muda wa siku 120 tu baada ya kutengenezwa. Asilimia 40@ ya damu ni seli hizi na ndio ambazo zinaipa damu rangi nyekundu. Seli zina protini na haemoglobin (chembechembe nyekundu) na hizi ndio huipa rangi nyekundu. Kazi ya seli hizi ni kubeba heya ya oxygeni kutoka kwenye mapafu na kuipeleka kwenye moyo ili isambazwe zaidi mwilini. Ka kutoa hewa ya kabondaioksaidi kutoka kwenye moyo na kuipelekwa kwenye mapafu ili itolewe nje. Pia hubeba viinilishe (nutrients) kupeleka sehemu zingine za mwili.

Seli n yeupe za damu (white blood cell) kwa jina la kitaalamu huit wa leukocytes. Kazi kubwa ya seli hizi ni kupambana na maambukizi na wadudu wa baya wanaoshambulia mwili. Seli hizi zinaweza kuishi kuanzia siku moja mpaka mwezi mmoja tu baada ya kutengenezwa. Pia hutengenezwa kwenye uroto wa mifupa. Seli hizi zipo aina nyingi, kuna ambazo hupambana na kula bakteria na wadudu wengine wavamizi mwilini, kuna nyingine zinatoa antibodies kwa ajili ya kusaidia kupambana.

Seli sahani (platelets) kitaalamu huitwa thrombocytes pia hutengenezwa kwenye uroto wa mifupa. Sinaishi siku sita tu baada ya kutengenezwa. Kazi yao kubwa ni kugandisha damu pindi kunapokuwa na jeraha. Plasma sio seli ni maji ya njano ambayo husaidia damu huogelea vizuri kupita kwenye mirija ya damu. Asilimia 90 ya plasma ni maji, ila pia ina madimi, vitamin na viinilishe (nutrients).


                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Jifunze Main: Afya File: Download PDF Views 3000

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya    👉2 Kitau cha Fiqh    👉3 Dua za Mitume na Manabii    👉4 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉6 Madrasa kiganjani   

Post zinazofanana:

Fahamu mtindo mzuri wa maisha

Postei hizi inahusu zaidi mtindo mzuri wa maisha, yaani mtu ale ki vipi au afanyeni nini ili kuweza kuboresha afya yake.

Soma Zaidi...
Kauli za wataalamu wa afya

Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu kauli mbalimbali za wataalamu wa afya

Soma Zaidi...
kitabu cha kanuni 100 za afya

Zijue kanuni 100 za afya ambazo watu wengi hawazijui. Laiti wangelizijua kwa hakika wangefaidika sana.

Soma Zaidi...
MAZINGIRZ

Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote

Soma Zaidi...
Jinsi ya kuimarish afya ya meno

Katika post hii utajifunza namna ambavyo unaweza kuboresha afya ya meno yakom

Soma Zaidi...
NYANJA ZA AFYA

Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote

Soma Zaidi...
Zijuwe faida za kiafya za kula Zabibu

Kula zabibubkina faida nyingi kwa afya yako.

Soma Zaidi...
kitabu cha afya

Jifunze sifa na aina za matunda, vijuwe viruturubisho

Soma Zaidi...