Posti hii inahusu zaidi madhara mbalimbali ambayo yanaweza kutokea kwa watu wasiofanya mazoezi, mazoezi ni kama tiba kwa namna Moja au nyingine ila Kuna madhara ambayo yanaweza kutokea kwa wale ambao hawafanyi mazoezi.
1. Kuwepo kwa magonjwa mbalimbali ya kuambukizwa.
Kwa sababu ya kutofanya mazoezi Kuna hatari ya kuwepo kwa magonjwa mbalimbali yasiyoambukizwa magonjwa hayo ni pamoja na saratani mbalimbali, mshutuko wa moyo na kisukari hayo ni baadhi ya magonjwa ambayo yanaweza kutokea kwa watu ambao hawafanyi mazoezi.
2. Kuwepo kwa Uzito mkubwa na unene wa kupitiliza.
Kwa sababu ya kuwepo kwa mafuta kwenye mwili Kuna hatari ya kuwepo kwa uzito mkubwa na uliopitiliza kwa sababu kila kitu kinachoingia mwilini ukaa humo humo na hakitoki mwilini hali inayosababisha kuwepo kwa uzito mkubwa na unene wa kupitiliza.
3. Pia kutofanya mazoezi usababisha kuwepo kwa presha .
Kwa sababu ya kuwepo kwa kiwango kikubwa cha mafuta kwenye mwili usababisha mishipa kuziba na upelekea kuwepo kwa presha kw watu ambao hawafanyi mazoezi.
4. Pia kwa wale wasiofanya mazoezi wanaweza kuwa na matatizo katika upumuaji.
Kwa sababu ya kuwepo kwa mazoezi usaidia vile vile kuweka kifua kwenye hali nzuri na pia mapafu yanakuwa na uwezo wa kupitisha hewa Vizuri kabisa bila shida yoyote, ila kwa wale wasiofanya mazoezi ni vizuri kabisa kufahamu kwamba wanaweza kupata matatizo mbalimbali katika upumuaji.
5.vile vile kwa wale wasiofanya mazoezi wanaweza kupata matatizo ya kuwepo kwa cholesterol kwenye mwili kwa sababu cholesterol usababishwa na kuwepo kwa kiwango cha mafuta mwilini kwa hiyo kwa wale wanaofanya mazoezi hawawezi au ni vigumu kupata tatizo hili kwa hiyo ni vizuri kabisa kufanya mazoezi Ili kuepukana na tatizo la kuwepo kwa cholesterol mwilini.
6. Pia kwa wale wasiofanya mazoezi Wana uwezekano wa kupata na maradhi ya mara Kwa mara kama vile mafua, kikohozi vi homa homa vya kila wakati na magonjwa madogo madogo kwa hiyo ni vizuri kabisa kufanya mazoezi Ili kujiepusha na matatizo mbalimbali kwenye mwili.
7. Pia kwa wale wasiofanya mazoezi miili yao huwa mizito na pia mifsuli pamoja na mifupa huwa laini kwa hiyo ni vizuri kabisa kufanya mazoezi Ili kuweza kujiepusha na hali ya kuwepo kwa ulaini kwenye mifupa na misuli
8 . Kwa wale wasiofanya mazoezi jitahidi walau kutafuta kitu chochote cha kukufanyaa utoe jasho kwa sababu mazoezi ni dawa na pia mazoezi ni kinga ni vizuri kabisa kufanya mazoezi.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
AFYA YA UZAZI Afya ya uzazi huweza kufungamana na mambo mengi sana.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu baadhi ya mambo ya kujiandaa kwa ajili ya kumuona daktari
Soma Zaidi...Endapo tezi dume haitatibiwa ama itachlewa kutibiwa basi mtu anaweza kupata madhara. katika post hii utakwenda kuyajuwa madhara ya tezi dume kwenye Mwili
Soma Zaidi...Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote
Soma Zaidi...Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote
Soma Zaidi...Katika post hii utajifunza namna ambavyo unaweza kuboresha afya ya meno yakom
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi njia au namna ya kufanya ili ngozi iweze kuwa laini bila kuwa na make up yoyote.
Soma Zaidi...Tumekusha kuona na kujua kuwa mbu anaweza kuambukiza maradhi mengi na ya virusi kama zika.
Soma Zaidi...