image

ZIJUWE NYANJA KUU 6 ZA AFYA

Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote

ZIJUWE NYANJA KUU 6 ZA AFYA

NYANJA SITA ZA AFYA
Kama tulivyosema hapo juu kuwa afya ni kuwa mzima kimwili na kiakili. Hata hivyo nadharia ya afya haiishii hapa ila inaendelea hata kujengwa katika mambo makuu sita. Mambo haya wataalamu wa afya wanayaita components of health. Mambo haya nitayataja hapa chini kwa ufupi tuu kama ifuatavyo

1.afya ya kimwili (physical health); hapa ni kuwa mzima kimwili, na afya hii huweza kujenga kwa kula vizuri, kufanya mazoezi ya mara kwa mara, kuepuka unywaji wa pombe na uvutaji wa sigara na matumizi ya madawa ya kulevya. Ukifanya hivi unaweza kuboresha mwili wako na kuboresha afya ya kimwili.

2.afya ya kiakili (mental health); hapa tunaangalia kuwa salama kiakili. Mtu akiwa na afya salama ya kiakili anakuwa na uwezo wa kujiamini, anapenda kujifunza vitu vivya na anavifurahia. Mtu mwenye hali hizi tunasema ana afya ya kiakili. Uwoga wa kuogopa watu ni katika maradhi ya kiakili.

3.afya ya mawazo na hisia (emotional health); hapa mtu anauwezo wa kuelezea hisia zake na mawazo yake. Kama kuna jambo limemuudhi analisema. Matu mwenye afya hii anauwezo wa kutaka msaada kwa mtu mwingine bia ya wasi.

4.Afya ya kiroho (spiritual health); hii ni afya inayojengwa na kuwa na imani juu ya mambo fulani. Na mara nyingi hapa tunazungumzia kuwa na imani juu ya dini. Watalamu wa afya wanaonesha mahusiano makubwa kati ya dini na mtu. Wataalamu wanatuambia zaidi matu mwenye imani ya kuna uwezekano mdogo wa kupata maradhi ya moyo kuliko mtu asiye na imani ya dini. -->

5.afya ya kijamii (social health); hii ni afya inayojengwa na kuwa na mahusiano mazuri na jamii. Kusaidia watu, kuitikia watu wanapokuita na kucheka nao na kuzungumza nao ni katika mambo yanayojenga afya hii. Wataalamu wa saikolojia wanatueleza mengi kuhusu afya hii.

6.afya ya mazingira (environmental health); hii afya hujengwa na mazingira yanayotuzunguka. Mtu awe na uwezo wa kupata hea safi na maji safi. Hivi hujenga afya hii. Mazingira kuwa safi na salama huweza kutengeneza afyahii.


                   





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 183


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

hathari zitokanazo na uvutaji wa sigara ,pombe na madawa ya kulevya na mbinu za kujikinga nayo
Posti hii inahusu zaidi utumiaji wa pombe na sigara pamoja na madawa katika jamii. Soma Zaidi...

ZIJUWE NYANJA KUU 6 ZA AFYA
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

Dondoo za afya 1-20
Somo Hili linakwenda kukuletea dondoo mbalimbali za afya Soma Zaidi...

dondoo 100 za afya
Soma Zaidi...

darasa la lishe
Jifunze mengi kuhusu afya na lishe, ujuwe utaratibu wa lishe Soma Zaidi...

Kitabu Cha Kitabu Cha matunda
Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet. Soma Zaidi...

Habari za uzima,nimesoma makala yako tumbo linaniuma upande wa kulia Ila sisikii Sana yenyewe Ila nikibonyeza na mkono ndio inauma yaani ni Kama nimegongwa sehem flani alafu Kuna maumivu lakini ni mpaka upaguse ndio una experience maumivu Kama Kuna namna
Kama unasumbuliwana tumbo upande wa kulia, kushoto, kitomvuni ama kuoande wa kuliavkwachini, basi muulizaji huyu atakupa uelewa. Soma Zaidi...

Namna ya kutunza chumba cha upasuaji
Posti hii inahusu zaidi namna ya kutunza chumba cha upasuaji, chumba cha upasuaji ni tofauti na vyumba vingine kwenye hospitali kwa hiyo vinahitaji uangalizi wa hali ya juu sana ili kuepuka aina yoyote ya uchafu kuwepo kwenye chumba hicho, zifuatazo ni na Soma Zaidi...

VYAKULA
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

DONDOO 100 ZA AFYA
Pata dondoo 100 za Afya Soma Zaidi...

Kitabu cha Afya 03
Yajuwe mambo yanayoathiri afya ya miili yetu, jifunze mambo mengi kuhusu afya. Soma Zaidi...

kitabu cha matunda
Jifunze sifa na aina za matunda, vijuwe viruturubisho Soma Zaidi...