ZIJUWE FIGO, KAZI ZA FIGO NA NAMNA YA KULINDA FIGO DHIDI YA MARADHI
Je unatambuwa namna fgo inavyofanya kazi, unazijuwa kazikuu za fogo mwilini, na je unajuwa namna ya kujilinda dhidi ya maradhi ya figo?. Basi makala hii itakujuza kuhusu masomo haya1
ZIJUWE FIGO KAZI ZA FIGO NA NAMNA YA KULINDA FOGO DHIDI YA MARADHI
Kila mtu ana figo mbili kwenye mwili wake, ukubwa wa figo unakadiriwa kufukia ukubwa wa ngumi yako. Katika mwili wako figo hupatikana karibia na katikati ya mgongo chini kidogo ya mbavu. Ndani ya kila figo kuna mamilioni ya vichujio vya kuchuja damu vinavyojulikana kama nephron. Kazi yake kubwa ni kuchuja damu, kuondoa uchafu kwenye damu na kuondoa maji ya ziada kwenye damu na kupata mkojo ambao ni mchanganyiko wa majina na uchafu uliotoka kwenye damu. Baadaye maji haya ya mchanganyko yanakwenda kwenye kibofu na kuhifadhiwa kama mkojo.
Kati ya maradhi mengi ya figo huanza kuathiri hizi nephone. Na endapo hizi nephrone zikiharibiwa zinapelekea figo kuathirika na kushindwa kufanya kazi vyema na kushindwa kuondoa uchau kwenye damu. Katika sababu za tatizo hili la kuathirika kwa nephone inaweza kuwa matatizo ya kurithi, majeraha, ama matumizi ya madawa ambayo athari yake yanaweza kuathiri figo.
Unaweza kuwa hatarini sana kama una maradhi ya kisukari, ama kama una shinikizo kubwa la damu ama una ukaribu wa kifamilia na watu ambao wana tatizo hili. Maradhi hatari ya figo ni yale ambayo huathiri nephone kipolepole na huwenda hii kuchukuwa miaka kadhaa hadi kuja kuumwa. Matatizo mengine yanayoweza kuathiri figo ni kama saratani ya figo na vijiwe vya kwenye figo.
Katika njia za kulinda figo yako dhidi ya maradhi ni pamoja na kunywa maji mengi angalau glasi 8 kwa siku. Fanya mazoezi na punguza kula vyakula vyenye chumvi sana. Nenda chooni kila unapohisi kukojoa wacha kubana mkojo kwa muda mrefu. Hizi ni baadhi tu ya njia ambazo zitakusaidia kulinda figo zako dhini ya maradhi.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Kitabu cha Afya 👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉3 Simulizi za Hadithi Audio 👉4 Madrasa kiganjani 👉5 kitabu cha Simulizi 👉6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina
Post zinazofanana:
Njia za Kujikinga na Maambukizi ya UTI
Maambukizi ya njia ya mkojo (UTI) ni tatizo la kiafya linalowapata watu wengi, hasa wanawake. UTI husababishwa na bakteria wanaoingia kwenye mfumo wa mkojo na kusababisha maumivu, kuwashwa, na usumbufu mkubwa wakati wa kukojoa. Kwa bahati nzuri, kuna njia mbalimbali za kujikinga na maambukizi haya kupitia usafi wa mwili, ulaji wa maji ya kutosha, na mtindo bora wa maisha. Makala hii inaelezea njia muhimu za kuzuia UTI na ukweli muhimu kuhusu ugonjwa huu.
Soma Zaidi...Dua Sehemu ya 01
Zijue fadhila za kuomba dua, tambua umuhimu na mahimizo juu ya kuomba dua?
Soma Zaidi...ITAMBUE SARATANI CHANZO CHAKE, DALILI NA KUKABILIANA NAYO
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote
Soma Zaidi...