(ii)Qur-an Yenyewe Inajieleza kuwa ni Ufunuo Kutoka kwa Allah (s.
(ii)Qur-an Yenyewe Inajieleza kuwa ni Ufunuo Kutoka kwa Allah (s.w) :
Ukiisoma Qur-an kwa makini utakuta kuna aya nyingi zinazojieleza kuwa Qur-an imeshushwa kutoka kwa Allah, kama inavyodhihirika katika aya chache zifuatazo:
Lakini Allah anayashuhudia kuwa aliyokuteremshia (kuwa ni haki) ameyateremsha kwa ilimu yake, na Malaika (pia) wana shuhudia. Na Allah anatosha kuwa shahidi. (4:166).
"Uteremsho wa Kitabu hiki hauna shaka kuwa umetoka kwa Muumba wa ulimwengu. Je, wanasema: "Amekitunga mwenyewe ". (Sivyo hivyo). Bali hicho ni haki itokayo kwa Mola wako ili uwaonye watu wasiojiwa na muonyaji kabla yako. Huenda wakaongoka." (32:2-3)
Na Kitabu tulichokuletea kwa wahyi ndicho cha haki, kinasadikisha (vitabu) vilivyokuwa kabla yake. Bila shaka Allah kwa waja wake ni Mwenye kuwajua vyema na kuwaona vizuri." (35:31)
Ni mwenye kuleta baraka (kweli kweli) yule aliyeteremsha Qur-an kwa mja wake, ili awe muonyaji kwa walimwengu wote. (25:1)
Uteremsho wa Kitabu hiki umetoka kwa Allah, mwenye nguvu, na mwenye hikima. (45:2)
Aya zote hizi na nyingi nyinginezo kama hizi zilizomo ndani ya Qur-an hujieleza wazi wazi kuwa Qur-an ni Kitabu cha Allah (s.w) alichowashushia wanaadamu kupitia kwa Mtume Muhammad (s.a.w). Pangelikuwa na haja gani Mtume kuandika kitabu kisha adai kuwa kinatoka kwa Allah (s.w) tukikumbuka kuwa yeye amekuwa mwaminifu na mkweli katika historia yote ya maisha yake.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya hapa chini kuipakua sasa!
Umeionaje Makala hii.. ?
Hukumu za kim sakina na tanwin ni idgham shafawiy, idh-har shafawiy, na Ikhfau shafawiy
Soma Zaidi...TAHADHARI KWA WASOMAJI WA QURAN Wasomaji wa qurani wawe na tahadhari katika usomaji wao.
Soma Zaidi...Kwa kuwa hakuna sababu mwalumu ikiyonukuliwa kuwa ndio chanzo cha kushushwa suravhii. Basi post hii itakujuza mambo ambayo huwenda hukuyajuwa kuhusu fadhika za surabhii na mengineyo.
Soma Zaidi...