Madai ya makafiri dhidi ya quran na hoja zao
Madai ya Makafiri dhidi ya Qur-an
Waislamu wanaamini pasi na tone la shaka kuwa Qur-an ni kitabu cha Allah (s.w) neno kwa neno kama mwenyewe anavyothibitisha:
"Hiki ni kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake, ni uongozi kwa wamchao Mwenyezi Mungu." (2:2)
Pamoja na uthibitisho huu, makafiri wa zama za kale na za sasa wameibuka na upinzani dhidi ya Qur-an na kudai kuwa kitabu hiki amekitunga mwenyewe Mtume Muhammad (s.a.w):
"Au ndio wanasema kuwa hii Qur-an ameitunga (Muhammad)? Bali wao hawaamini lolote." (52:33)
Dai hili la kumpa Mtume (s.a.w) utunzi wa Qur-an limewakilishwa katika sura mbali mbali na makafiri wa zama mbali mbali. Kwa ujumla makafiri wamedai kuwa Qur-an ni:
1. Mashairi aliyotunga Mtume Muhammad (s.a.w).
2. Zao la njozi za Muhammad (s.a.w) zilizovurugika
3. Zao la mwenye kujidhania kupata ufunuo
4. Zao la mwenye kifafa na aliyepagawa na shetani.
5. Aya za shetani
6. Uandishi wa Muhammad (s.a.w) kwa msaada wa Mayahudi na Wakristo.
7. Utunzi wa Muhammad (s.a.w) ili kuleta umoja na ukombozi wa Waarabu.
8. Utunzi wa Muhammad (s.a.w) ili kurekebisha tabia ya Waarabu.
9. Utunzi wa Muhammad (s.a.w) ili ajinufaishe kiuchumi.
10. Utunzi wa Muhammad (s.a.w) ili kuwania madaraka na ukubwa.
Qur-an yenyewe inakanusha madai haya katika aya mbali mbali kama tunavyojifunza katika aya zifuatazo:
Basi naapa kwa mnavyoviona. Na msivyoviona. Kwa hakika hii ni kauli iliyoletwa na Mjumbe (wa Mwenyezi Mungu) mwenye hishima (kubwa). Wala si kauli ya mtunga mashairi (kama mnavyosema).Ni machache sana mnayoyaamini. Wala si kauli ya mchawi (kama mnavyodai). Ni kidogo kabisa kuwaidhika kwenu. Ni mteremsho utokao kwa Mola wa viumbe vyote. Na kama
(Mtume) angelizua juu yetu baadhi ya maneno tu, bila shaka tungalimshika kwa mkono wa kuume, (wa kulia). Kisha kwa hakika tungalimkata mshipa mkubwa wa moyo (69:38-46).
Na hapana yeyote katika nyie angeweza kutuzuia naye. Kwa hakika hii (Qur-an) ni mawaidha kwa wanaomcha Mwenyezi Mungu. Na kwa yakini tunajua kuwa miongoni mwenu wamo wanaokadhibisha. Na itakuwa ni sikitiko, (m ajut o) juu ya wanaokanusha. Na hakika hii ni haki ya yakini. Basi litukuze jina la Mola wako aliye Mkuu. (69:47-52)
Pamoja na aya hizi na nyingine nyingi zinazokanusha madai ya makafiri dhidi ya utunzi wa Qur-an bado Allah (s.w) ametoa changa moto kwa makafiri wa zama zote tangu ianze kushuka Qur-an hadi leo, kuwa:
"Na ikiwa mna shaka kwa hayo tuliyomteremshia Mtumwa Wetu (kuwa hakuteremshiwa na Mwenyezi Mungu) basi leteni sura moja iliyofanywa na (mtu) aliye mfano wake, na muwaite waungu wenu bighairi ya Mwenyezi Mungu (wakusaidieni), ikiwa mnasema kweli." (2:23)
Pamoja na changamoto hii ya Qur-an, hebu tuangalie kwa undani kidogo udhaifu wa hizi hoja kumi za makafiri dhidi ya Qur-an:
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Kitau cha Fiqh 👉2 kitabu cha Simulizi 👉3 Dua za Mitume na Manabii 👉4 Simulizi za Hadithi Audio 👉5 ai web app 👉6 web hosting
Post zinazofanana:
Sababu za kushuka surat an-Nas na surat al Falaq
Sura mbili hizi pia hujulikana kwa jina la al muawidhatain ambazo ni surat an Nas na surat al falaq.
Soma Zaidi...Sababu za kushuka surat al Mauun
Sura hii ni katika sura ambazo zinahitaji kusomwa kwa mazingatio sana. Wanaoswali bila ya kuzingatia swala zao, wameonywa vikali sana. Wanaowatesa na kuwanyanyasa mayatima wameonywa vikali. Wanaowanyima wenye haja na masikini huku wakiwakaripia nakuwasem
Soma Zaidi...Sababu za kushuka surat al Quraysh
Qurayh ni jina la kabila la Mtume Muhammad S.A.W. Sura hii itakwenda kukujulisha neema ambazo Maquraysh wamepewa na hawataoewa wao wowote baada ya wao.
Soma Zaidi...fadhila za sura kwenye quran
FADHILA ZA BAADHI YA SURA Umuhimu na ubora wa baadhi ya sura na aya.
Soma Zaidi...HUKUMU ZA TAFKHIIM NA TARQIQ
Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa
Soma Zaidi...Qur-an Yenyewe Inajieleza kuwa ni Ufunuo Kutoka kwa Allah (s.w)
(ii)Qur-an Yenyewe Inajieleza kuwa ni Ufunuo Kutoka kwa Allah (s.
Soma Zaidi...