Navigation Menu



Wanaoongozwa na wasioongozwa na quran

Wanaoongozwa na wasioongozwa na quran

Wanaoongozwa na Qur-an:



Lengo la kushushwa Qur-an kama ilivyobainishwa katika Qur-an yenyewe ni kuwaongoza binaadamu wote katika njia iliyonyooka. Njia iliyonyooka ni njia sahihi ya maisha itakayomuwezesha binaadamu kufikia lengo la kuumbwa kwake. Pamoja na Qur-an kuwa muongozo kwa watu wote, haiwaburuzi kwa nguvu kwenye uongofu bila ya wao wenyewe kudhamiria kuongoka.Qur-an huongoza wacha-Mungu tu kama tunavyojifunza katika aya zifuatazo:


"Hiki ni kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake, ni uwongozi kwa wamchao Mwenyezi Mungu.Ambao huyaamini yasiyoonekana (maadam yamesemwa na Mwenyezi Mungu na Mtume wake) na husimamisha Swala na hutoa katika yale Tuliyowapa.Na ambao wanaamini yaliyoteremshwa kwako na yaliyoteremshwa kabla yako na wanaamini (kuwa iko) Akhera. Hao wako juu ya uongozi utokao kwa Mola wao, na hao ndio wenye kufaulu." (2:2-5)



Kwa mujibu wa aya hizi wanaongozwa na Qur-an ni wacha-Mungu wenye sifa zifuatazo:
- Waumini wa kweli wa vipengele vyote vya nguzo za Imani. - Wasimamishaji Swala. (Rejea juzuu ya pili).
- Wanaotoa yale aliyowaruzuku Allah (s.w) kwa ajili ya kuwahurumia wanaadamu wenye kuhitajia msaada na katika kusimamisha Dini ya Allah(s.w). Aliyoturuzuku Allah (s.w)ni kila tulichonacho ikiwa ni pamoja na mali, elimu, afya, nguvu,vipaji na kadhalika.


Wasioongozwa na Qur-an:
Tunajifunza katika Qur-an kuwa makundi mawili ya watu Makafiri (na washirikina) na Wanafiki hawataongozwa na Qur-an. Kuhusu makafiri na washirikina tunafahamishwa:


Hakika wale waliokufuru ni sawa kwao ukiwaonya (kwa hii Qur-an) au usiwaonye; hawataamini. (Kama kwamba) Mwenyezi Mungu amepiga muhuri juu ya nyoyo zao na juu ya masikio yao; na juu ya macho yao pana vifuniko; basi watakuwa na adhabu kubwa. (2:6-7)



Pamoja na Qur-an kuwa na sifa ya ukweli na uwazi kama majina yake yanavyodhihirisha, haiwezi kuwaongoza wapinzani (makafiri) wa wazi wa Mwenyezi Mungu(sw) na ujumbe wake. Haiwezi kwa sababu binaadamu amepewa uhuru na Mola wake wa kuamua na kufanya atakavyo. Akiamua kutii anaweza na akiamua kuasi anaweza. Hivyo mtu aliyeamua kuukataa mwongozo huu kwa makusudi huna namna ya kumuongoza.



Kuhusu wanafiki tunafahamishwa:


"Na katika watu, wako (wanafiki) wasemao "Tumemuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho" na hali ya kuwa si wenye kuamini. Wanataka kumdanganya Mwenyezi Mungu na wale walioamini, lakini hawadanganyi ila nafsi zao, nao hawatambui. Nyoyoni mwao mna maradhi, na Mwenyezi Mungu amewazidishia maradhi. Basi watakuwa na adhabu iumizayo kwa sababu ya kule kusema kwao uongo.(2:8-10)


Na wanapoambiwa msifanye uharibifu ulimwenguni Husema "Sisi ni watengenezaji." Hakika wao ndio waharibuji, lakini hawatambui. Na wanapoambiwa: "Aminini kama walivyoamini watu, "husema "Oh! Tuamini kama walivyoamini wapumbavu?" Hakika wao ndio wapumbavu lakini hawajui. (2:11-13)


Na wanapokutana na walioamini husema, "Tumeamini," na wanapokuwa peke yao kwa mashetani wao husema: "Hakika sisi tu pamoja nanyi, tunawacheza shere tu." Na Mwenyezi Mungu atalipa shere yao na kuwawacha katika upotofu wao wakitangatanga ovyo. Hao ndio waliokhiari upotofu kuliko uongofu, lakini biashara yao haikupata faida wala hawakuwa wenye kuongoka." (2:14-16)



Wanafiki pamoja na kujiita Waislamu na pengine wakawa ni wanachuoni wa Qur-an walio mahiri katika kuifasiri Qur-an kwa kutumia balagha, mantiq, sarfu, n.k; hawataongozwa na Qur-an maadamu wamekhiari maslahi ya dunia kinyume na mwongozo wa Mwenyezi Mungu(sw). Si tu hawa wasomi wa Qur-an wenye sifa hizo zilizoainishwa katika aya hizi hawataongozwa na Qur-an bali pia Allah (s.w) amewafananisha na mbwa katika aya zifuatazo:


"Na wasomee (Ewe Muhammad) habari za wale tuliowapa Aya zetu (kuzijua), kisha wakajivua nazo (wasizifuate). Na shetani akawaandama na, wakawa miongoni mwa waliopotea.Na kama tungelitaka tungeliwanyanyua kwazo, lakini wao waligandamana na ardhi (kutaka maslahi ya kidunia wakayapuuza ya Akhera) na wakayafuata matamanio yao. Basi hali yao ni kama hali ya mbwa; ukimpigia kelele (hukimbia na huku) anahema, na ukimwacha pia huhema.Hiyo ndio hali ya watu waliokadhibisha Aya zetu. Basi simulia hadithi, huenda wakatafakari. "(7:1 75-176)



Hivyo, kwa mujibu wa Aya hizi, mnafiki hata akiwa ni A’alim (Sheikh) wa Qur-an na Hadith, kamwe hawezi kuongozwa na Qur-an.




                   


Download app yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiw ana App yetu. Bofya liln hapo chini kuweza ku download

Download Now Bongoclass

           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu image Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Quran Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Views 856


Sponsored links
πŸ‘‰1 Simulizi za Hadithi Audio     πŸ‘‰2 kitabu cha Simulizi     πŸ‘‰3 Kitabu cha Afya     πŸ‘‰4 Kitau cha Fiqh     πŸ‘‰5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     πŸ‘‰6 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Aasbab Nuzul surat Ash sharh: sababu za kushuka alam nashrah (surat Ash sharh)
Makala hii itakwenda kukufundisha sababu za kushuka kwa alam nasharah yaani Surat Ash sharh. Soma Zaidi...

Sababu za kushuka surat al alaqa
Asbsb nuzul surat al alaqa, sababu za kushuka surat alaqa. Sura hii imeshuka Makka na ina aya 19. Ni sura ya 96 katika mpangilio wa Quran. Soma Zaidi...

quran na sayansi
YALIYOMONENO LA AWALI1. Soma Zaidi...

Saratul-humaza
Quran (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Sababu za kushuka surat al humazah
Sura hii inaonya vikali tabia ya kusengenya na kusambaza habari za uongo. Wameonywa vikali wenye tabia ya kujisifu kwa mali, kukusanya mali bila ya kuitolea zaka. Soma Zaidi...

IDGHAAM KATIKA LAAM
Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa Soma Zaidi...

Historia ya kushuka kwa quran
Soma Zaidi...

Sababu za kushuka surat an-Nas na surat al Falaq
Sura mbili hizi pia hujulikana kwa jina la al muawidhatain ambazo ni surat an Nas na surat al falaq. Soma Zaidi...

Fadhila za kusoma Quran na umuhimu wa kusoma Quran
Unazijua faida za kusoma Quran, na je ni faida gani utapata ukisoma Quran? Soma Zaidi...

Kwa nini quran ilishuka kidogo kidogo?
Kuna sababu nyingi za kuonyesha umuhimu wa Quran kushuka kwa mfumo wa kidogo kidogo Soma Zaidi...