"Ewe mwanangu!
"Ewe mwanangu! Kwa hakika jambo lolote lijapokuwa na uzito wa chembe ya hardali, likawa ndani ya jabali au mbinguni au katika ardhi, Mwenyezi Mungu Atalileta (amlipe aliyefanya); bila shaka Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa mambo yaliyofichikana, (na) Mjuzi wa mambo yaliyo dhahiri"(31:16).
Aya hii inatuhakikishia kuwa kila mtu amekadiriwa jambo lake na hapana yeyote na hila yoyote itakayomzuia mtu asipate kile alichokadiriwa kukipata au kumuwezesha mtu kupata kile ambacho hakukadiriwa. Pia aya ifuatayo inatuweka wazi zaidi:
โNa hakuna mnyama yoyote (kiumbe chochote) katika ardhi ila riziki yake iko juu ya Mwenyezi Munguโฆ.. " (11:6)
Kutokana na aya hii tunajifunza kuwa lengo la maisha yetu si kutafuta rizki na maslahi ya dunia bali vitu hivi ni vitendea kazi tu vyakutuwezesha kulifikia lengo kuu. Lengo letu kuu ni kuusimamisha Uislamu katika jamii ili tuweze kumuabudu Allah (s.w) ipasavyo katika kila kipengele cha maisha yetu ya kibinafsi na ya kijamii ambalo ndilo lengo la kuumbwa kwetu.
Hivyo katika mchakato wa kuliendea lengo hili la kusimamisha Uislamu katika jamii, tusimchelee yeyote wala
tusichelee kupoteza chochote kwani hamna mwenye uwezo wa kutupokonya au kutuzidishia chochote kile kinyume na alivyotukadiria Allah (s.w). Katika hili ni vyema tukazingatia pia aya ifuatayo:
Hautokei msiba katika ardhi wala katika nafsi zenu ila umekwishaandikwa katika Kitabu (cha Mwenyezi Mungu) kabla Hatujaumba. Kwa yakini hili ni sahali kwa Mwenyezi Mungu." (57:22).
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Mambo ya faradhi kuhusu maiti ya muislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Takriban Mitume wote walitokea katika jamii zilizozama katika ujahili, lakini kamwe ujumbe wao haukuathiriwa na mitazamo ya ujahili kwa ujumla, walahawakuingizautamaduni wa kijahili katika dini ya Allah (s.
Soma Zaidi...ุนููู ุฃูุจูู ุฐูุฑูู ุฌูููุฏูุจู ุจููู ุฌูููุงุฏูุฉูุ ููุฃูุจูู ุนูุจูุฏู ุงูุฑููุญูู ููู ู ูุนูุงุฐู ุจููู ุฌูุจููู ุฑูุถููู ุงูููููู ุนูููููู ูุงุ ุนููู ุฑูุณูููู ุงููู...
Soma Zaidi...Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...โKatika kuumbwa mbingu na ardhi na mfuatano wa usiku na mchana,ziko alama (hoja) za kuonyesha kuwepo Allah (s.
Soma Zaidi...Ndoto za kweli ni moja kati ya njia ambazo Allah huwasiliana na wanadamu.
Soma Zaidi...