Kulipia Ramadhani
Mtu anapodaiwa siku alizo kula katika mchana wa mwezi wa Ramadhani,au siku ambazo swaumu yake ilibatilika, si lazima azilipe mara tu baada ya Ramadhani, japo ni bora mtu kumaliza deni lake haraka. Tunafahamishwa katika Hadith kuwa Bibi βAysha (r.a) alikuwa akilipia Ramadhani katika mwezi wa Shaaban:
Aysha (r.a) ameeleza: βNilikuwa na madeni ya swaumu ya Ramadhani. Sikuweza kulipa kadha ila katika mwezi wa Shaaban. (Bukhari na Muslim).
Hali kadhalika si lazima mtu kulipa mfululizo siku zote anazodaiwa, bali anaweza kuzilipa kidogo kidogo kutokana na Hadith ifuatayo:
Ibn Umar (r.a) ameeleza kwamba Mtume (s.a.w) amesema juu ya kulipa Ramadhani: (Mtu) akitaka na afarikishe; na akitaka na afululize. (Daru Qu tni).
Kama mtu amechelewa kulipa siku anazodaiwa mpaka Ramadhani nyingine ikaingia, basi kwanza ataifunga hiyo Ramadhani iliyomuingilia. Baadaye ndipo alipe hiyo deni yake wala halipi fidia; iwe kuchelewa huko ni kwa udhuru ama si kwa udhuru. Lakini ni vizuri zaidi kulipa siku anazodaiwa kabla ya kuingia Ramadhani nyingine.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Endapo mke na mume wameachana na hali ya kuwa mke ana watoto wachanga. Je uislamu unasemaje kuhusu taratibu za malezi?
Soma Zaidi...Maana ya elimuElimu ni ujuzi ulioambatanishwa na utendaji.
Soma Zaidi...Kwenye kipengele hichi tutajifinza vyanzo mbalimbali vya sheria ua kiislamu.
Soma Zaidi...Mwanadamu anatakiwa aishi huku akikumbuka kuwa ipo siki atakufa. Hivyo basi inatupata lujiandaa mapema kwa ajili ya kifo.
Soma Zaidi...(b) WarumiJamii ya Warumi nayo ni miongoni mwa jamii zinazohesabika kuwa zilianza kustaarabika mapema katika historia ya ulimwengu.
Soma Zaidi...