ijuwe namna ya kufanya ihram na Vazi la ihram

ijuwe namna ya kufanya ihram na Vazi la ihram

Jiunge nasi WhatsApp
Upate Update zetu

ijuwe namna ya kufanya ihram na Vazi la ihram

Ihram



Mwenye kunuia Hija au ‘Umra katika Miiqaat anakuwa katika hali ya kuchunga masharti kadhaa mpaka akamilishe matendo kadhaa ya Hija au ‘Umra. Hali hii ya kuchunga masharti hujulikana kwa jina la “Ihram ”.



Wanaume wanapokuwa katika Ihram hulazimika kuvaa vazi rasmi la Ihram.Vazi la Ihram kwa wanaume ni kuvaa shuka mbili nyeupe zisizo shonwa.Shuka moja hufungwa kiunoni na mkanda huweza kutumika ili kuhakikisha isivuke. Shuka la pili huvaliwa lubega kwa kufunika bega la kulia na kuacha wazi bega la kushoto. Katika hali ya Ihram, ni haram kwa mwanamume kuvaa nguo nyingine yoyote, ni haramu kufunika kichwa, ni haram kuvaa soksi au kuvaa viatu vinavyofunika miguu.



Wanawake hawana vazi rasmi la Ihram. Akiwa katika Ihram Hajat analazimika kama kawaida kujifunika mwili wake wote isipokuwa uso na viganja vya mikono na atavalia ushungi. Hijab yaweza kuwa ya rangi yoyote isiyovutia kama kawaida ya vazi la mwanamke wa Kiislamu lakini vazi jeupe ni bora. Mwanamke akiwa katika Ihram ni haramu kufunika uso au kuvaa soksi za mikononi(gloves). Pia wanawake katika Ihram hawaruhusiwi kuvaa soksi wala kuvaa viatu vinavyofunika miguu.



Yaliyoharamishwa kwa Mwenye kuwa katika Ihram
(i)Kujimai (kufanya tendo la ndoa) au kubusu au kukumbatiana au kufanya vitendo vingine vya kimapenzi kati ya mume na mke ambavyo vitawaletea fikra za kufanya ten do la ndoa.
(ii)Kusema maneno maovu na machafu kama vile kusengenya,kugombana, kugombanisha, kusema uwongo, kubishana, n.k. Na anayekusudia kufanya Hija katika (miezi) hiyo basi asiseme maneno machafu wala asifanye vitendo vichafu wala asibishane katika hiyo Hija ... (2:197).
(iv) Kunyoa au kung’oa nywele, kukata kucha au kukata au kupunguza sehemu yoyote ya mwili ila kwa matibabu kama vile kuumika, kutolewa damu kwa ajili ya matibabu na mengineyo.
(vi)Kuoa au kufanya mipango ya ndoa au hata kupeleka posa.
(vii)Kujipaka manukato
(viii)Kuvaa nguo ya rangi yenye kuvutia
(ix)Kwa wanaume kuvaa nguo iliyoshonwa, na kufunika kichwa.
(x)Kwa wanawake kufunika uso na kufunika viganja vya mikono kwa kuvaa glovu (gloves).
(xi)Kuvaa viatu vinavyofunika miguu na kuvaa soksi.
(xii)Kuwinda au kusaidia kuwinda angalau kwa kuonyesha mnyama anayewindwa.
(xiii)Kula nyama iliyowindwa au iliyopatikana kwa msaada wa mtu aliyekuwa katika Ihram.
(xiv)Kula mayai ya ndege waliopatikana kwa kuwindwa.




                   


Download Post hii hapa

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Vyakula Main: Afya File: Download PDF Views 1495

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi    👉2 Kitau cha Fiqh    👉3 Simulizi za Hadithi Audio    👉4 Madrasa kiganjani    👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉6 Bongolite - Game zone - Play free game   

Post zinazofanana:

Vitamini C ni nini, na vipo kwenye nini?
Vitamini C ni nini, na vipo kwenye nini?

Hapa utajifunza maana ya Vitamini C, mwaka vilipogunduliwa na aliyegundua vitamini C

Soma Zaidi...
Faida za juice ya tende.
Faida za juice ya tende.

Posti hii inahusu zaidi faida ya juice ya tende,ni juice inayotumiwa na watu wengi sana na wengine wanajua kabisa faida zake na kuna wengine hawajui wanaitumia kama mazoea tu, ila kuna ambao hawajui kabisa basi zifuatazo ni faida za juice ya tende kwa wal

Soma Zaidi...
Vyakula vya kuongeza nguvu za kiume.
Vyakula vya kuongeza nguvu za kiume.

Tatizo la nguvu za kiume linawwza kuzuiliwa ama kupunguzwa kwa kutumia muunganimo wa njiankadhaa kama kubaduki vyakula, kutumia dawa, kupata ushauri kwa wataalamu wa afya ya mahusiano ama kufanya nazoezi. Je na wewe unasumbuliwa na tatizo hili? Makala hii

Soma Zaidi...
UPUNGUFU WA VITAMIN NA MAJI
UPUNGUFU WA VITAMIN NA MAJI

Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote

Soma Zaidi...
Tufaha (apple)
Tufaha (apple)

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula apple/tufaha

Soma Zaidi...
Fahamu vitamini C na kazi zake, vyakula vya vitamini C na athari za upungufu wake.
Fahamu vitamini C na kazi zake, vyakula vya vitamini C na athari za upungufu wake.

kuhusu vitamini C, kuanzia chanzo chake, maana yake, upungufu wake na kazi zake kwenye miili yetu.

Soma Zaidi...
Virutubisho vya mwili
Virutubisho vya mwili

Posti hii inahusu zaidi virutubisho vya mwili, ni aina tano za vyakula ambayo ufanya kazi mbalimbali kwenye sehemu za mwili wa binadamu.

Soma Zaidi...
Orodha ya madini, chanzo chake na faida zake
Orodha ya madini, chanzo chake na faida zake

Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu orodha ya madini chanzo chake na faida zake

Soma Zaidi...
Faida za kiafya za kula miwa
Faida za kiafya za kula miwa

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula miwa

Soma Zaidi...