- Uislamu ulieneza nadharia kuwa wanaadamu wote ni sawa na wote ni watumwa mbele ya Mwenyezi Mungu (s.
- Uislamu ulieneza nadharia kuwa wanaadamu wote ni sawa na wote ni watumwa mbele ya Mwenyezi Mungu (s.w).
- Uislamu ulijenga uhusiano wa udugu na upendo baina ya watu bila kujali hadhi, nafasi, rangi, taifa la mtu.
- Uislamu ulisisitiza kuwa ubora wa mtu unatokana na ucha-Mungu wake na pia mtumwa au mtu huru anastahiki kuwa kiongozi na kutiiwa ipasavyo
Rejea Qur’an (49:13) na (4:25).
- Utumwa katika Uislamu ulikuwa jambo la kupita na sio taasisi ya kudumu inayojenga matabaka ndani ya jamii.
- Uislamu uliweka mikakati ya kulinda haki, utu na hadhi ya watumwa kwa kuwafanyia wema na ihsani kama wanaadamu wengine.
Rejea Qur’an (4:36) na (49:13).
- Watumwa walikuwa na haki ya kuamini na kufuata mila au dini waipendayo bila kushurutishwa.
Rejea Qur’an (2:256).
- Watumwa walikuwa wanapata huduma za kijamii kama mavazi na malazi sawa na mabwana au wanaadamu wengine.
- Mtumwa alikuwa akikosea alisamehewa badala ya kuadhibiwa, Mtume (s.a.w) alisema mtumwa asamehewe hata mara sabini kwa siku.
- Mtumwa alistahiki kuwa kiongozi na kutiiwa ipasavyo maadamu ni muislamu na Mcha-Mungu. Mtume (s.a.w) amesema “msikilizeni na mtiini kiongozi hata akiwa ni mtumwa wa kutoka uhabeshi, maadam anafuata njia ya haki”
- Uislamu unalinda hadhi ya mtumwa kwa kutomuita “Ewe mtumwa wangu” badala yake anaitwa “Ewe kijana wangu”.
- Watumwa walikuwa na haki ya kujikomboa na huru kwa njia mbali mbali zikiwemo:
1. Kulipa kiasi fulani cha pesa au mali yeyote inayokubalika.
2. Kubadilishana na mateka Waislamu waliokamatwa na maadui.
3. Kulipa fidia kwa kufanya jambo fulani lenye manufaa kwa jamii ya waislamu.
Rejea Qur’an (47:4).
- Mtume (s.a.w) na Maswahaba waliwaachia watumwa huru na kuwakomboa wengine kisha kuwaacha huru kama ifuatavyo:
1. Mtume (s.a.w) mwenyewe aliwaacha huru watumwa 63.
2. Bi Aisha (r.a) mkewe Mtume (s.a.w) aliwaacha huru watumwa 67.
3. Ibn Abbas aliwaachia huru watumwa 70.
4. Abdallah bin Umar aliwaacha huru watumwa 1,000.
5. Abdul-Rahman bin Auf alinunua watumwa 30,000 na kuwaacha huru.
Mpaka kufikia mwisho wa uongozi wa Makhalifah wa nne Waongofu, suala la Utumwa lilibakia kuwa historia katika ulimwengu wa Kiislamu.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Utangulizi:Uislamu unamuelekeza mwanaadamu namna nzuri ya kuendesha maisha yake katika kila kipengele cha maisha akiwa binafsi, katika familia na katika jamii.
Soma Zaidi...Nguzo za uislamu (EDK form 2; dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Sharti za SwalaSharti za Swala Sharti za swala ni yale mambo ya lazima anayotakiwa Muislamu ayachunge na kuyatekeleza kabla hajaanza kuswali.
Soma Zaidi...Sunnah za SwalaSunnah za Swala Vipengele vya sunnah katika swala ni vile ambavyo mwenye kuswali akivitenda husaidia sana kukuza daraja ya swala yake na kuipa nguvu na msukumo mkubwa wa kuiwezesha kufikia lengo lililokusudiwa kwa urahisi zaidi.
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukufundisha sunnah 9 za swala. Sunnah hizi ni zile ambazo ukiziwacha swala yako haibatiliki.
Soma Zaidi...