TATIZO LA KUVIMBA KWA USO NA MIGUU KWA WAJAWAZITO

TATIZO LA KUVIMBA KWA USO NA MIGUU KWA WAJAWAZITO

KUVIMBA VYA MIGUU KWA WAJAWAZITO Kuvimba kwa miguu ni hali inayowapara wengi katika wajawazito.

Jiunge nasi WhatsApp
Upate Update zetu

TATIZO LA KUVIMBA KWA USO NA MIGUU KWA WAJAWAZITO

KUVIMBA VYA MIGUU KWA WAJAWAZITO
Kuvimba kwa miguu ni hali inayowapara wengi katika wajawazito. Kitaalamu hali hii hutambulika kama odema. Wakati mwingine si miguu tu ndio huvimba bali mikono, nyayo na uso huweza kuvimba. Ijapouwa huku kukuvimba kwa ghafla kwa uso na mikono ni dalili ya maradhi mengine kama preeclampsia.

Hali hii ya kuvimba kwa miguu huweza kuwapata wanawake katika kipindi chote cha ujauzito, iwe wajauzito ulio mchanga, ama kipindi cha katikati cha ujauzito ama kipindi cha mwisho cha ujauzito. Katika hali ya kawaida kuvimba kwa miguu kwa wajawazito sio jambo la kusumbua kiafya yaani kusema kuwa ni tatizo kubwa. Hapana hii ni kawaida kwa wajawazito.

Kuvimba huku kunaweza kuwa ni tatiko kama kutaweza kuambatana na baadhi ya matatizo mengine ya kiafya kama maumivu makali ya kicha, kizunguzungu, kutokwa na damu, kushinwa kuona kwa usahihi ama kushinwa kupumua ama kupumua kwa taabu, hali hizi kuweza kuashiria hatari. Ni vyema mjamzito awahi kituo cha afya kama ana hali hizi.

Sababu za kutokea kwa vimbe hizi ni mabadiliko ya mwilini yanayopatikana wakati wa ujauzito. Kuongezeka kwa damu mwilini na kuongezeka kwa mapigo ya moyo huweza kuchangia zaidi hali hii. Halikadhalika ongezeko la homoni maalumu zinazotolewa wakati wa ujauzito. Haya yote kwa pamoja huchangia kutokea hali hizi za kuvimba.

Tofauti na sababu hizi pia zipo nyingine kama mabadiliko ya hali ya hewa. Hapa tunazungumzia joto, ambalo pia ni sababu ya kuvimba. Sababu nyingine ni kutokunywa maji ya kutosha, matatizo ya homoni yaani homone imbalance. Kukaachini kwa muda mrefu ukaaji wa kukalia miguu. Ama kusimama kwa muda mefu.

Kupunguza ama kuepuka hali hii ni vyema kufanya mazoezi ya mara kwa mara, kukaa kivulini, kulalia upande kwa kushoto unapolala. Hakikisha unakula mlo kamili, hakikisha kuwa unakunywa maji ya kutoka kwa siku. Na hata ukizidisha ni faida kwako. Epuka kusimama kwa muda mrefu ama kukaa kwa kukalia mguu. Epuka kukaa kwa muda mrefu kwa staili moja. Kuna matatizo mengu ya kiafya yanayoambatana na ujauzito, ni vyema mjamzito akiwa makini.





                   

Download Post hii hapa

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Uzazi Main: Afya File: Download PDF Views 3531

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh    👉2 Simulizi za Hadithi Audio    👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉4 Madrasa kiganjani    👉5 Kitabu cha Afya    👉6 Bongolite - Game zone - Play free game   

Post zinazofanana:

Je? Naomba kuuliza mkewangu ali ingiya kwenye hezi siku tatu damu ikakata nikakutana nae siku ya nane je? Anaweza pata ujauzito
Je? Naomba kuuliza mkewangu ali ingiya kwenye hezi siku tatu damu ikakata nikakutana nae siku ya nane je? Anaweza pata ujauzito

Idadi ya siku hatari za kupata mimba hutofautiana kutoka kwa mwanamke mmoja namwinhine. Kinda ambao idadivyavsikuvzao za hatari ni nyingi kuliko wengine.

Soma Zaidi...
Maji ya Amniotic
Maji ya Amniotic

Posti hii inahusu zaidi maji ya Amniotic ni maji ambayo uzunguka mtoto na kufanya kazi mbalimbali kama ifuayavyo.

Soma Zaidi...
Njia za kiasili zilizotumika zamani kqtika kupima ujauzito
Njia za kiasili zilizotumika zamani kqtika kupima ujauzito

Somo hili linakwenda kukuletea njia za asili walizotumia zamani katika kupima ujauzito

Soma Zaidi...
Njia za kuzuia upungufu wa damu kwa wajawazito
Njia za kuzuia upungufu wa damu kwa wajawazito

Posti hii inahusu zaidi njia za kuzuia upungufu wa damu kwa wajawazito, ni mojawapo ya njia ambazo utumiwa na wahudumu wa afya ili kuweza kuzuia upungufu wa damu kwa wajawazito.

Soma Zaidi...
DARASA LLA AFYA na afya ya uzazi na malezi bora kwa jamii
DARASA LLA AFYA na afya ya uzazi na malezi bora kwa jamii

Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote

Soma Zaidi...
Upungufu wa homoni ya estrogen
Upungufu wa homoni ya estrogen

Posti hii inahusu zaidi upungufu wa homoni ya estrogen na dalili zake, aina hii ya homoni ikipungua mwilini uleta madhara na matatizo mbalimbali kwenye mwili.

Soma Zaidi...
Haya maji meupe hutokea wakat mimba ishatungwa au ukifanya tendo la ndoa lazima utokee?
Haya maji meupe hutokea wakat mimba ishatungwa au ukifanya tendo la ndoa lazima utokee?

Majimaji yanayitoka kwenye uke yanafungamana na taarifa nyingi kuhusu afya vya mwanamke. Ujauzito, maradhi, mabadiliko ya homoni na zaidi.

Soma Zaidi...
Njia za kuzuia ugumba
Njia za kuzuia ugumba

Posti hii inahusu zaidi njia za kuzuia ugumba, ni njia ambazo utumiwa na wapenzi ambao wameshindwa kupata watoto hasa kwa wale ambao wamezaliwa wakiwa na uwezo wa kupata watoto lakini kwa sababu tofauti tofauti wanashindwa kupata watoto kwa hiyo njia zifu

Soma Zaidi...
Imani potofu kuhusu uzazi wa mpango
Imani potofu kuhusu uzazi wa mpango

Post hii inahusu zaidi imani potofu kuhusu uzazi wa mpango, ni imani walizonazo Watu kuhusu matumizi ya uzazi wa mpango.

Soma Zaidi...
Sababu za kutoshika mimba kwa mwanamke
Sababu za kutoshika mimba kwa mwanamke

Post hii inahusu zaidi sababu za kutoshika mimba kwa mwanamke, kuna kipindi ambacho mwanamke hushindwa kushika mimba kuna sababu mbalimbali mojawapo ni kama zifuatazo

Soma Zaidi...