Sababu za kutoshika mimba kwa mwanamke

Post hii inahusu zaidi sababu za kutoshika mimba kwa mwanamke, kuna kipindi ambacho mwanamke hushindwa kushika mimba kuna sababu mbalimbali mojawapo ni kama zifuatazo

Sababu za kutoshika mimba kwa mwanamke

1. Kutokuwa na uwiano mzuri wa homoni ambapo kwa kitaalamu huitwa hormonal imbalance, kwa hiyo ili mimba iweze kutungwa ni lazima kuwepo na usawa wa homoni yaani zote zilingane.

 

2. Ovari kushindwa kutoa mayai.

Kuna wakati mwingine ovary hazitoi mayai  hii ni kwa sababu ya kuwepo kwa Maambukizi au tatizo lolote kwenye mfumo wa uzalishaji.

 

3. Kuziba kwa mirija ya uzazi ambayo kwa kitaalamu huitwa follapiani tube kwa hiyo mishipa hii ikiziba usababisha mayai kushindwa kukutana na mbegu za mwanaume wakati wa urutubishaji.

 

4. Kuna wakati mwingine mirija ya uzazi kujaa maji, hali hii utokea kwa sababu ya kuwepo kwa Maambukizi kwenye mirija ya uzazi na ikishajaa maji usababisha mayai au yai kushindwa kukutana na mbegu za mwanaume.

 

5. Kuwepo kwa uvimbe kwenye kizazi.

Kuna wakati mwingine uvimbe kwenye uzazi usababisha mama kutozaa kwa sababu mtoto hawezi kupata sehemu ya kukaa na kukua.

 

6. Magonjwa mbalimbali na yenyewe usababisha mwanamke kushindwa kupata mimba, magonjwa kama kisonono, kaswende, kisukari na pia maambukizi kwenye via vya kiza, haya Magonjwa yakiwa sugu usababisha ugumba.

 

7. Kuwepo kwa msongo wa mawazo.

Kwa kawaida ili mimba iweze kushika mwanaume na mwanamke wanapaswa kuwa katika hali nzuri bila mawazo wakifanya hivyo ni rahisi kushika kwa mimba.

 

8. Utoaji wa mimba.

Kuna wakati mwingine kutoa mimba mara kwa mara nakwo usababisha kutoshika kwa mimba kwa sababu kuna wakati mwingine via vya uzazi vinakuwa vimechokonolewa vya kutosha na baadae mimba haiwezi kushika.

 

9. Matumizi ya pombe, bangi, sigara na ulevi wa kupindukia usababisha kutoshika kwa mimba kwa sababu baadhi ya vileo usababisha kupungua kwa homoni za uzazi.

 

10. Kuwa na uzito kupita kiasi.

Kwa kawaida uzito mkubwa nao ni sababu ya kutoshika mimba kwa sababu ili mimba ishike mwili wa mama unapaswa kuwa kwenye hali ya usawa .

 

11. Kwa hiyo baada ya kufahamu haya ni vizuri kurekebisha mtindo wa maisha kwa wale ambao wana changamoto za kutopata mimba ili waweze kupata watoto na ni vema kabisa kupata ushauri wa kitaalamu kama kuna tatizo la kukosa mimba.



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/06/06/Monday - 07:54:48 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 5294


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-