Hizi ni sifa za ziada za mchumba katika uislamu. Sifa hizi wengi hawazijui ama hawazingatii.
Kizazi, Rika na Elimu
Sifa nyingine za kuzingatia wakati wa kuchagua mchumba ni kizazi na rika. Kuhusu kizazi Mtume (s.a.w) anatunasihi:
"Oeni wale wanawake wenye upendo na huruma, wenye kizazi na hakika watakuwa ni wenye manufaa katika kuongeza idadi yenu miongoni mwa matafa." (Abu Daud, Nasai)
Kwa vijana ambao ndio mara yao ya kwanza kuingia katika maisha ya ndoa, pamoja na kuzingatia sifa za msingi zilizoelezwa, ni vema wakachaguana vijana kwa vijana kama alivyoshauri Mtume (s.a.w) katika hadithi ifuatayo:
Jabir (r.a) ameeleza: "Tulikuwa na Mtume (s.a.w) katika vita. Tulipokaribia Madina wakati wa kurejea nilisema: "Ee Mtume wa Mwenyezi Mungu, hakika nimeoa hivi karibuni." Akauliza, "Umeoa"? Nikajibu, "Ndio" Akauliza: "Bikra au mjane?" Nikajibu "Mjane" Akasema, "Kwa nini asiwe bikra ili uweze kucheza naye, naye aweze kucheza nawe..." (Bukhari na Muslimu)
Jambo lingine Ia kuzingatia wakati wa kuchagua uchumba ni Elimu. Kama mume na mke watakuwa na Elimu sahihi juu ya Uislamu na taaluma nyingine za mazingira yao watakuwa na nafasi nzuri zaidi ya kuwalea watoto wao kimaadili na kitaaluma. Katika kusisitiza hili tuzingatie mchango wa bibi Khadija (r.a) alioutoa katika kuupeleka mbele Uislamu kutokana na utajiri wake na mchango wa bibi 'Aisha (r.a) alioutoa katika kuufundisha Uislamu kutokana na Elimu yake ya Uislamu.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Kwa nini ni muhimu kuswali? Post hii itakwenda kukufundisha kuhusu umuhimu wa kusimamisha swala.
Soma Zaidi...Swala iliyosimamishwa vilivyo ndiyo nyenzo kuu ya kumtakasa Muislamu na kumpa sifa zinazomuwezesha kustahiki kufanya kazi takatifu ya kusimamisha Uislamu katika jamii.
Soma Zaidi...Katika post hii utakwenda kujifunza jinsi ya kutawadha kama vile ambavyo alitawadha Mtume
Soma Zaidi...