Tutazungumzia: Makundi ya vyakula rafiki kwa mgonjwa wa kisukari. Namna ya kuchagua chakula chenye sukari ndogo kwa mwili. Mifano ya vyakula vya kula na vile vya kupunguza.
Mtu mwenye kisukari anahitaji kula vyakula vinavyoleta uwiano mzuri wa sukari kwenye damu, visivyopandisha kiwango cha sukari kwa haraka, na vinavyosaidia mwili kufanya kazi kwa utulivu. Hii huitwa kula vyakula vyenye glycemic index ya chini au ya kati.
Hivi ndivyo vyakula muhimu zaidi kwa mwenye kisukari.
Mfano:
Spinachi
Kabichi
Karoti (kwa kiasi)
Brokoli
Sukuma
Hivi vina nyuzinyuzi nyingi, vitamini na hupandisha sukari polepole sana.
Mfano wa nafaka rafiki ni kama:
brown rice
Oats
Uji wa mtama
Uwele
Ngano nzima (whole wheat)
Nafaka hizi huongeza sukari taratibu kwa sababu ya fiber nyingi.
Protini husaidia kushibisha bila kuongeza sukari.
Zingatia:
Mayai
Samaki
Nyama isiyo na mafuta mengi
Kuku bila ngozi
Maharage, dengu, choroko, kunde
Matunda yana sukari ya asili, hivyo kiasi ni muhimu.
Mifano mizuri:
Tikiti maji (kiasi kidogo)
Embe (kiasi)
Papai
Maembe mabichi
Mapera
Strawberries, blueberries, apples, pears
Epuka kula matunda kwa wingi kwa mara moja. Gawa mara mbili hadi tatu kwa siku.
Mafuta ya asili yana msaada kwa moyo na hupunguza sukari kupanda.
Mzuri kula kwa kiasi:
Avocado
Karanga
Mbegu (chia, maboga, alizeti)
Mafuta ya zeituni
Chagua:
Mtindi usio na sukari
Maziwa fresh bila sukari
Cheese kwa kiasi
Kunywa maji mengi kuliko vinywaji vya sukari. Epuka soda, juisi zilizoongezwa sukari na vinywaji vya kuongeza nguvu.
Kula kiasi na kupanga muda wa kula ni muhimu zaidi kuliko chakula chenyewe? Kwa mfano, mtu akila chakula kizuri lakini kingi kwa mara moja, sukari bado inaweza kupanda.
Vyakula bora kwa mwenye kisukari ni vile vyenye fiber nyingi na sukari ndogo.
Mboga, nafaka nzima, protini nyepesi na matunda kwa kiasi ndizo msingi wa mlo mzuri.
Epuka sukari nyingi, vyakula vilivyosindikwa na mafuta mengi mabaya.
Kila mlo ugawiwe vizuri: mboga nyingi, wanga kidogo, protini kiasi.
Kunywa maji ya kutosha kila siku.
Umeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi faida za apple kwa mama mjamzito, ni faida anazozipata mama akiwa mjamzito kwa sababu ya kuwepo kwa vitamini mbalimbali kwenye apple ambavyo usaidia katika makuzi ya mtoto.I
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi namna nzuri ya kuandaa mchai chai kwa ajili ya matumizi mbalimbali, Ili kutumia mmea wa mchai chai zifuatazo ni mbinu za kuandaa mmea huu.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu athari za ulaji wa protini kupitiliza
Soma Zaidi...