picha

ukweli na sifa zake kwenye uislamu na sifa za mtu mkweli

Ukweli ni uhakika wa jambo.

ukweli na sifa zake kwenye uislamu na sifa za mtu mkweli
  1. Kuwa Mkweli

Ukweli ni uhakika wa jambo. Muislamu wa kweli hana budi kuwa mkweli na kusimamia ukweli. Allah (s.w) anatuamrisha tuwe wakweli katika kuendesha shughuli zetu zote.

 

“Enyi mlioamini Mcheni Mwenyezi Mungu na kuweni pamoja na wakweli.” (9:119).

Msema kweli ni mpenzi wa Allah (s.w) . Naye Allah (s.w) amewaandalia wakweli ujira mzuri kabisa kwa hapa duniani na huko akhera kama tunavyobainishiwa katika Qur-an” kuwa Allah (s.w) atasema katika hiyo siku ya hisabu:-

 

“Hii ndiyo siku ambayo wakweli utawafaa ukweli wao. Wao watapata bustani zipitazo mbele yake mito. Humo watakaa milele. Allah amewawia radhi nao wanaradhi naye. Huku ndiko kufaulu kukubwa. (5:119)

 

“... Na wanaume wasemao kweli na wanawake wasemao kweli... Allah amewaandalia msamaha na ujira mkubwa”. (33:35).

Msisitizo wa Muislamu kujipamba na tabia ya kuwa mkweli pia tunaupata katika Hadith ifuatayo:

‘Abdullah bin Mas ’ud (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: Utaongea ukweli kwa sababu ukweli unaongoza kwenye Ucha-Mungu na Ucha-Mungu unaongoza kw enye Pepo. Mja ataendelea kusema kweli na kubakia katika ukweli mpaka aorodheshwe mbele ya Allah kuwa ni miongoni mwa wakweli wakubwa.Tahadharini na uwongo! Uwongo unaongoza kwenye uasi na uasi unaongoza kwenye Moto.Mja ataendelea kusema uwongo na kubakia katika uwongo mpaka aorodheshwe mbele ya Allah kuwa ni miongoni mwa waongo wakubwa”.

(Bukhari na Muslim).



                   

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: General Main: Post File: Download PDF Views 2153

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
πŸ‘‰1 Kitabu cha Afya     πŸ‘‰2 ai web app     πŸ‘‰3 Simulizi za Hadithi Audio     πŸ‘‰4 Bongolite - Game zone - Play free game     πŸ‘‰5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     πŸ‘‰6 Dua za Mitume na Manabii    

Post zinazofanana:

fadhila za kusoma quran

Fadhila na umuhimu wa kusoma quran 1.

Soma Zaidi...
MAANA YA Quran

Maana na majina ya Quran Maana ya Wahyi.

Soma Zaidi...